Miriam Kiwoko profile. ~~~~~~~~~ Asubuhi - TopicsExpress



          

Miriam Kiwoko profile. ~~~~~~~~~ Asubuhi ilikuwa tulivu sana iliyopendezwa kwa mawingu ya rangi ya bluu yaipendezeshao anga achalia mbali ndege viumbe ambao kiujumla wanafurahia uwepo wao katika sayari hii; Miriam aliitizama saa yake ya ukutani chumbani mwake na kusitaajabu kwa kuchelewa kuamka kutoka kitandani kwake kwani ilikuwa ni jumatatu kwa wenzetu huiita blue monday na hii n kwa lugha ya kiingereza. Miriam alichoka sana kiasi kwamba hata kuinuka pale kitandani alikuwa akijifikilia sana na nikutokana na Kulewa sana jana yake akiwa na marafiki zake hivyo basi aliandaa uongo wat kumdanya bosi wake; aliinuka kinyonge kuelekea sebuleni kwake na kuiendea simu ya ukutani ili aweze kumpigia Mjungu ambaye ni bosi wake na aliamua kufanya ivyo kwa sababu simu yake ya mkononi haikuwa na vocha. ****** B & M ni kampuni ya kizawa inayojihusisha na uwekezaji hasa katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kama Magari toka nje ya nchi na kuwauzia wazawa, halikadhalika inajihusisha na uuzaji wa madini na utengenezaji wa simu nchini Tanzania, Kampuni ina ongozwa na bodi ya wakurugenzi na Bwana Mjungu Mwigamba ndiye mkurugenzi mkuu wa kampuni,.... Itaendelea...
Posted on: Fri, 18 Oct 2013 17:26:33 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015