Msimamo wa Mbowe kwa Polisi Una Akili; Ila Polisi ni Bunduki - TopicsExpress



          

Msimamo wa Mbowe kwa Polisi Una Akili; Ila Polisi ni Bunduki Tumuhoji Anayeitumia..!! Msimamo wa Freeman Mbowe wa kutotii amri ya jeshi la polisi ya kumtaka apeleke ushahidi wa polisi kuhusika na kuishambulia Chadema kwa bomu kule Arusha ni msimamo wenye akili na sina budi kumuunga mkono kwa msimamo wake huo, kwa vile ingekuwa upuzi na ujinga kama angelikubaliana na amri hiyo ya jeshi la polisi! Polisi wanashutumiwa kutupa bomu hilo ambalo liliuwa watu 4 na kujeruhi wengine 70 sasa wao kama watuhumiwa wanahitaji ushahidi wa nini!? Au ndiyo utaratibu ule ule wa Kikomunist wa mtu mmoja anakuwa mtuhumiwa, mwendesha mashitaka, mtetezi na hakimu kwa wakati mmoja!? Polisi wakajitetee mahakamani mbele ya chombo neutral! Hata hivyo siamini kama tuna mahakama huru inayoweza kusimamia haki za chama cha upinzani ambacho kinaonekana kuwa tishio kwa CCM! Hivyo pamoja na kuipeleka kesi hiyo kwenye mahakama za hapa nyumbani ambazo mahakimu wake na majaji wote wapo mfukoni mwa kitengo cha usalama wa taifa, hivyo si rahisi kupata uamuzi wa haki, bali hukumu itakayotolewa na mahakama hiyo utakuwa na ushawishi mkubwa wa kitengo hicho cha TISS! Kwa mtizamo wangu kwa vile vithibitisho vyote vipo ingelikuwa sahihi kama Chadema wangelifungua keshi hiyo kwenye mahakama ya kimataifa ya vitendo vya uhalifu ya ICC. Kauli na vitisho vya pilisi vinaleta kichefuchefu pale wanapomtishia Mbowe kwamba kama asipofika kituo cha polisi na uthibitisho wa mlipuko wa bomu ni kosa la jinai! Je, kitendo cha polisi kulipua bomu hilo na kuuwa raia 4 na kujeruhi wengine 70 siyo kosa la jinai!? Je, kitendo cha polisi kumuua Daudi Mwangosi kwa bomu siyo kosa la jinai!? Je, kitendo cha polisi kulipua bomu kwenye mkutano wa mbunge wa Chadema John Mnyika siyo kosa la jinai!? Je, rais anaposhindwa kuwachukulia hatua za kisheria polisi wanaofanya vitendo vya kigaidi siyo kosa la jinai!? Lazima tujiulize ujeuri huu wa jeshi la polisi unatoka wapi!? Ni lazima tujiulize hivyo kwa vile ni muda mrefu sasa jeshi hili limeendeleza ubabe wa kikatili wa kutoa watu roho kwa kutumia mabomu na rais amekaa kimya kama vile polisi wanawaua raia wa nchi nyingine ambayo yeye siyo jukumu lake kuhoji nini kinachoendelea! Rais na Serikali yake wamejikausha kimya kama vile siyo jukumu lao la kulinda maisha ya watanzania na hata pale polisi wanatuhumiwa moja kwa moja tena kwa ushahidi bado tu rais na Serikali yake wamekaa kimya na hata wanawatetea na kuwapandisha vyeo wale waliofanya ukatili huo! Sasa katika mazingira kama haya rais na Serikali yake wana maana gani kwa wananchi!? Tukumbuke ni hivi karibuni tu rais Kikwete aliahidi kwenye kile alichokiita kongamano la amani kwamba polisi wanawaua raia kikatili watashughulikiwa, lakini jambo la kushangaza ni kwamba maneno hayo tangu yatolewe hata mwezi mmoja haujapia lakini jeshi hilo la polisi limeendeleza ubabe wake ule ule wa kuwalipua raia kwa mabomu ya kivita! Na hii inadhihirisha wazi kwamba maneno ya Kikwete hayakutoka moyoni mwake bali yalikuwa na matamko ya majukwaani kama yalivyo matamko mengine ya kila siku! Nasema hivyo kwa vile hata mwezi mmoja haujaisha tangu atoe tamko hilo jeshi hilo hilo la polisi limelipua bomu lingine kwenye mkutano wa mbunge wa Chadema John Mnyika! Sasa lazima tujiulize kiburi na ubabe huu wa jeshi la polisi unatoka wapi!? Mungu nchi hii ni mmoja ambaye yupo juu ya sheria ambaye ni rais pamoja na kampuni yake ya ulinzi ya TISS! Sasa najiuliza umungu huu wa jeshi la polisi nao unatoka wapi!? Kwanza ni kwanini jeshi la polisi wawe na silaha za JWTZ!? Wanazipata wapi hizi silaha za kivita wakati silaha hizi kama vile mabomu wanayoalipua siyo mabomu yanayotumiwa na jeshi hilo la polisi!? Jeshi la polisi mabomu yao ni mabomu ya machozi, sasa haya mabomu ya vitani wanayapata wapi!? Tunafahamu kwamba polisi wanaweza kupata ruhusa ya kuyatumia mabomu haya kutoka kwa mtu mmoja tu ambaye ni rais kwa kupitia kitego chake cha usalama wa taifa! Hawa ndiyo wenye mamlaka ya kuchukuwa mabomu toka ghala la JWTZ na kuwakabidhi jeshi la polisi! Pia kitengo hiki cha TISS ndicho kitengo pekee kinachoweza kuwapa idhini jeshi la polisi kufanya kile wanachokiona ni muhimu kwa rais na Serikali yake! Huwa najiuliza ni kwanini jeshi la polisi wanapoenda kwenye mikutano ya Chadema wanabeba silaha nzito za kivita kama vile wanaenda kupambana na wananchi wanaowasikiliza viongozi wao kwa amani!? Mbona jeshi hili hili la polisi wanapoenda kwenye mikutano ya CCM hawabebi silaha nzito na wala hawalipui mabomu kwenye mikutano hiyo!? Nimekuwa nikisema kwamba bila ya kukiondoa kitengo cha TISS kwenye ofisi ya rais hakuna taasisi wala idara yoyote ya Serikali itakayokuwa huru na kufanya mambo yake kulingana na utaratibu uliokuwepo, bali kitengo hiki kitakuwa kinaingilia kila idara! Kitengo hiki kinaamini kwamba hakuna maisha Tanzania bila ya CCM kuwa madarakani hivyo yote haya yanoyotokea hayatokei kwa bahati mbaya hapana, ni mambo ambayo yanapangwa makusudi na kitengo hiki kwa makusudi ya kuwakatisha wananchi tamaa na kuwatishia kwamba kama wasipoikubali CCM hawana maisha. Mimi ninavyoelewa ukatili wote huu unaofanywa na jeshi la polisi dhidi ya wamnanchi wasiokuwa na hatia unafanywa kulingana amri inayotoka ofisi ya rais kupitia kitengo chake cha TISS na ndiyo maana polisi hawana hofu wala hawajali kuuwa raia kwa mabomu kwa vile wanaua kulingana amri ya mwenye nchi ambaye ni rais! Na kwa uthibitisho wa hili polisi wamekuwa wakipandishwa vyeo kwa kuuwa raia wasiokuwa na hatia badala ya kufikishwa mbele ya sheria! Jeshi la polisi ni watekelezaji wa mikakati ya kuilinda CCM lakini wabunifu na watoaji amri kwa jeshi la polisi ni ofisi ya rais! Msije mkashangaa polisi wakalipua mabomu mashuleni au mahospitalini au popote pale patakapoonekana kufanya hivyo ni kuilinda na kuinusuru Serikali ya CCM katika nafasi yake ya kubakia madarakani! Ndiyo maana nasema kwamba jeshi la polisi ni sawa na bunduki ambayo haina akili wala haisemi au kusikia, na bunduki hii hutumiwa na binadamu ambaye ni TISS! Hivyo itakuwa ni upuuzi na ujinga kuendelea kuilaumu bunduki kwanini inaendelea kuuwa watu ovyo bila sababu wakati mwenye bunduki tunamfahamu! Tumeshuhudia kila bunduki inapozitoa roho zetu, wakati tunailalamikia bunduki kwa kutufanyia ukatili, mwenye bunduki anaichukuwa bunduki yake na kuanza kuisifia kwamba ni bunduki nzuri sana! Na baada ya kusema maneno hayo huichukuwa bunduki yake na kuanza kuisafisha na hata kuiimarisha zaidi tayari kwa mauwaji mengine yajayo! Kitendo cha kuendelea kuilamu bunduki hakitatusaidia kusitisha mauwaji haya ya kinyama ya kupangwa, bali maamuzi mazuri ni kumng’ang’anie mwenye bunduki na hata ikiwezekana tumkamate na kumpekeka mbele ya haki..!! noordinjella.livejournal
Posted on: Thu, 25 Jul 2013 16:58:02 +0000

Trending Topics



-height:30px;">
Tomorrow should be an interesting day. Here is your Daily Tarot

Recently Viewed Topics




© 2015