Mukhtasari @ 1pm Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho - TopicsExpress



          

Mukhtasari @ 1pm Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amesema kuwa wafanyikazi wa baraza la kaunti ambao hawakuripoti kazini hii leo wamefutwa kazi,na kuwa wale walionekana wakitupa taka mjini watafikishwa mahakamani. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Maafisa wa polisi katika eneo la kwale wameanzisha uchunguzi kuwasaka watu watatu wanaodaiwa kumuua mwenzao na kuutupa mwili wake katika eneo la tiwi Bixa. ,,,,,,,,,,,,,,, Tume ya kuajiri walimu TSC imewasilisha kesi mahakamani dhidi ya wakuu wa KNUT kwa kukiuka agizo la mahakama la kuwataka kusitisha mgomo huo. ,,,,,,,,,,,,,,,,,, Jaji mkuu wa mahakama ya kikatiba nchini Misri Adli Mansour anatarajiwa kuapishwa kama rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya jeshi kumuondoa madarakani rais Mohammed Morsi, ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo.
Posted on: Thu, 04 Jul 2013 10:12:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015