Mwakani, katikati (sio mbali) kutakuwa na watu 6 watakaotaka - TopicsExpress



          

Mwakani, katikati (sio mbali) kutakuwa na watu 6 watakaotaka kwenda mikoa yote ya Tanzania, kwa gari (isipokuwa Zanzibar kwa meli). Chakula na malazi juu yao ila utawajibika kwa kila mkoa kutoa walau maelekezo na machaguo kadhaa ya sehemu watapolala/kula. Jukumu yako ni Usafiri kuwazungusha nchi nzima! Sehemu zisizo na vivutio ka Pwani unapeta tu, sehemu zenye vivutio unasubiri kwa muda walau wajionee. Nia ni kuijua Tanzania na vimijimimiji vyake vyote muhimu, ama vijiji mashuhuri, mfani Musoma lazima uwapeleke kwa Mwalimu. Andika travel plan yako na gharama utakazo toza, siku utazotumia na hasa sisitizia usalama wao, plan B gari ikifa na plan B dreva akisizi! Onesha vituo vikuu vya mapumziko, vivutio husika kila mkoa na kisha tuma document yako kwenda rmushi@efulusi, unaweza andika Kiswahili ama Kiingereza na si lugha nyingine. Atakayeshinda tenda, basi watakuBook kwa hizo tarehe husika. Uwe makini, Zingatia japo bei unatoa leo, tukio ni mwakani katika kati, usijetoa bajeti njaa ukawaacha watoto wa watu Kantalamba ukalikimbia gari lako!. Unaweza shawishi suala la Mvua, ili isiwe kipindi cha mvua
Posted on: Thu, 01 Aug 2013 14:19:12 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015