Mwambieni Barack Obama kuwa Watanzania wa kawaida tuna maswali - TopicsExpress



          

Mwambieni Barack Obama kuwa Watanzania wa kawaida tuna maswali magumu juu ya ujio wake Tanzania na Urafiki wake na sisi.... 1. Kwa nini aliposhinda Urais(2008), Rais Kikwete alikuwa rais wa kwanza kumtembelea,na wala haikuwa Mwai Kibaki wa Kenya wakati ule.? 2. Kwa nini anaitembelea tanzania wakati hajawai kutembelea Kenya kwao japo kwa saa moja? 3. Kwa nini jina lake la Kati "Hussein" Marekani na vyombo vya Habari vya kimataifa wanalificha? 4. Je ni kweli kuna vyama vya siasa hapa nchini wanavidhamini ili kufanya vurugu na mambo mengine kwa maslahi ya Marekani? 5. Eti na wao waliwai kuendelea kiuchumi kutokana uwekazaji wa kutoka nje ya nchi? Naomba pia tumjulishe haya yafuatayo ambao tunajivunia nayo sisi kama vijana na Watanzania.. 1. Tanzania ni Nchi ambayo ina utajiri mkubwa wa rasilimali lakini viongozi wake wanawadanganya wananchi kuwa Tanzania ni nchi masikini. 2.Pia ni nchi yenye mito mikubwa maziwa makubwa na ukanda mrefu wa bahari lakini bado tunashida kubwa ya maji kwa matumizi mbalimbali hasa ya nyumbani, kilimo,viwanda na usafirishaji. 3. Pia ni sehemu ambapo viungo vya Binadamu kama figo,nyeti, n.k vina soko kubwa na inasemekana wateja wakubwa ni wafanya biashara, viongozi na wanasiasa...lakini pia ni moja ya mikakati yetu ya kujinasua katika umasikini wa kipato uliopindukia. 4.Ni nchi ambayo inaongoza kwa wingi wa misitu ukiacha Sierra Leone, Gabon na Kongo lakini pia ni hapahapa tunapoongoza kwa wanafunzi wanao kaa chini madarasani kutokana na uhaba mkubwa wa Madawati. 5.Mwambieni pia tunaoongoza kwa vitu vingi ambavyo ni adimu katika nchi nyingine duniani, kwa mfano Mlima Kilimanjaro(5895m), Simba wanaopanda miti (Ngorongoro National Park) Madini ya Tanzanite (hayapatikani hata Marekani), n.k lakini hivi vyote havijaweza kutunufaisha kiwango cha kuvutia hata tukaweza kumshukuru kutuweka Tanzania. TUNAYO MENGI YAKUJIVUNIA LAKINI KUYATAJA HAPA NI AIBU KUBWA. NAIPENDA NCHI YANGU, NCHI YANGU TANZANIA.
Posted on: Thu, 27 Jun 2013 17:14:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015