Mwanamke aliemzaa mtoto na kumtupa kisimani Teso asakwa na - TopicsExpress



          

Mwanamke aliemzaa mtoto na kumtupa kisimani Teso asakwa na polisi Maafisa wa polisi wa Teso wanamsaka mwanamke ambaye alijifungua mtoto na kumtupa kwenye kisima cha maji eneo la Teso. Mwili wa mtoto huyo mchanga ulipatikana kwenye kisima kimoja cha maji katika eneo la Royco wilayani Teso kaskazini nyakati za asubuhi na mkaazi mmoja. Kulingana na wenyeji inaamini kuwa mamake mtoto huyo alimzaa usiku na kumtupa kwenye kisima hicho kabla ya kutoweka ambapo anasakwa na polisi. Aidha wameshutumu vikali kitendo hicho huku wakiwataka wasichana na wanawake kupanga uzazi iwapo hawataki kupata watoto. * * * * * *
Posted on: Thu, 18 Jul 2013 18:38:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015