Mwanamme mmoja amenyaganywa gari lake na majambazi waliokuwa - TopicsExpress



          

Mwanamme mmoja amenyaganywa gari lake na majambazi waliokuwa wamejihami kwa bunduki katika eneo la London viungani mwa mji wa Nakuru. David Kemboi ameambia Radio Amani kuwa alikuwa anaelekea nyumbani kwake akitoka mjini Nakuru mwendo wa saa mbili unusu wakati majambazi hao walipomvamia na kumweka katika buti lake. Sasa, anaomba yeyote atakayeliona gari lake leupe aina ya Premio lenye nambari ya usajili KAV 395W apige ripoti kwa polisi.
Posted on: Sat, 03 Aug 2013 11:31:51 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015