Mzalendo ninani? Mzalendo ni mtu anayejali maslahi ya Taifa lake - TopicsExpress



          

Mzalendo ninani? Mzalendo ni mtu anayejali maslahi ya Taifa lake na watu wake,mzalendo analitegemea, analipenda na kuliamini Taifa lake, mzalendo waweza kumjua kupitia tabia zake hizi 1. Anawawazia mawazo mema wananchi wenzake wote bila kujali makundi wanayotoka. 2. Anawatazamia mema wananchi wenzake wote bila kujali makundi wanayotoka. 3. Anawanenea maneno mema ya amani wananchi wenzake wote bila kujali makundi wanayotoka. 4. Anawatendea matendo mema ya upendo, anawaona kwa jicho jema la upendo na anahusiana kwa uhusiano mwema wa upendo na wananchi wenzake bila kujali makundi wanayotoka 5. Anawafanyia maamuzi mema ya haki na kuwasimamia kwa misimamo mema ya haki wananchi wenzake bila kujali makundi wanayotoka Mtu huyu ndiye mzalendo wa kweli, ni mtu wa amani, ni mtu wa upendo ni mtu wa haki anazo sifa zote za kuwa Rais wa Nchi ana sifa za kuwa mkuu wa mkoa anazo sifa za kuwa mkuu wa wilaya na anasifa za kuwa kiongozi wa jamii popote alipo.
Posted on: Fri, 29 Nov 2013 17:11:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015