NAIONA HATMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI..!! Leo kunafanyika - TopicsExpress



          

NAIONA HATMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI..!! Leo kunafanyika mkutano wa pili wa miondombinu kwa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki (the 2nd EAC Head of State Infrastructure Summit) mjini Mombasa katika Hoteli ya kifahari ya Whitesands Beach Resort. Mkutano huu ni wa pili baada ya ule wa kwanza uliofanyika Entebe Uganda mwezi June mwaka huu na kuwashirikisha Marais watatu tu ambao ni Yoweri Museveni (Ug), Uhuru Kenyatta (Ke) na Paul Kagame (Rw). Katika mkutano wa kwanza Rais Kikwete (Tz) na Rais Nkurunzinza (Bur) hawakushiriki japo baadae ilidaiwa kuwa hawakualikwa. Nilipata mashaka kidogo kuamini kama kweli Rais wetu na wa Burundi hawakualikwa. Nani alipaswa kuwaalika? Hao waliohudhuria walialikwa na nani? Na kama kweli hawakualikwa, nini lengo lao hao waliogoma na mwaliko? Kikao cha leo kimenifanya nizidi kutafakari hatma ya Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki. Kikao cha leo kinahusisha Marais wa nchi tano lakini kwa mara nyingine Rais Kikwete hajahudhuria. Sina hakika kama amenyimwa mwaliko tena au ameamua tu kughairi. Nchi zinazokutana Mombasa leo ni Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Sudani Kusini (ambayo inahudhuria kama mjumbe mwalikwa). Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili mambo matatu makubwa. La kwanza ni kurasimisha ushuru wa forodha mmoja kwa nchi wanachama (single custom duty), pili ni kuanzisha kitambulisho cha jumuiya kitakachomruhusu Raia wa nchi yoyote mwanachama kutembea au kuishi katika nchi nyingine bila kubughudhiwa. Hii inafuatia kufukuzwa kwa Wanyarwanda walioishi Tanzania zaidi miaka 30 kwa kuitwa wahamiaji haramu (illegal migrants). So kupitia vitambulisho hivyo issue ya illegel migrants haitakuwepo tena, mathalani una kitambulisho unaweza kuishi npopote. Hoja hii imeletwa na Kagame na amenukuliwa na Wolfgang Media akisema "This is due to the continuing expulsion of our citizens – thousands of Rwandans alleged living illegally in Tanzania and been driven across the border back into Rwanda" Kuna wasiwasi kuwa Kagame anatetea hoja hii ili kutimiza azma yake ya siri ya kupenyeza Wanyarwanda katika kila nchi wanachama wa EAC na kuhakikisha wanashika nyadhifa kubwa serikalini kwa manufaa ya Rwanda. Mpango huo wa Kagame unaonekana kufanikiwa kwa kiasi fulani nchini Tanzania kwani hadi sasa kuna wakuu wawili wa idara nyeti serikalini waliobainika kuwa ni Wanyarwanda na kwa sasa hawajulikani walipo. Wa kwanza ni aliyekuwa Mkuu wa mawasiliano Usalama wa Taifa ambaye ametoweka mwezi May mwaka huu, na wa pili ni Luteni Kanali Colestine Seromba aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Kompyuta kilichopo Dar es Salaam aliyetoweka December mwaka jana. Hadi sasa hajulikani alipo japo inadaiwa amerudi kwao Rwanda. Suala la tatu lililopewa kipaumbele katika mkutano wa leo ni ujenzi wa reli ya Afrika Mashariki na uboreshaji wa sekta ya bandari kwa manufaa ya nchi zote wanachama. Bandari iliyopangwa kuboreshwa ni ya Mombasa ili iweze kuzihudumia nchi za Rwanda na Uganda. Tayari nchi hizo zimeshatangaza kutotumia tena bandari ya Dar es Salaam kuanzia mwezi September mwaka huu. Mpango wa kuimarisha bandari ya Mombasa unadaiwa kuwa mkakati maalumu wa kuidhoofisha Tanzania kiuchumi kutokana na ukweli kuwa, bidhaa za Rwanda na Uganda zinachangia 19% ya mapato ya Bandari ya Dar es Salaam, hivyo kuhamia Mombasa ni kupoteza mapato hayo. Ikumbukwe kwenye mkutano wa AU mwaka 2009 Rais Kagame aliwahi kutamka kuwa anashangaa Tanzania yenye rasilimali zote lakini haiendelei, akasema yeye angepewa bandari tu hakuna nchi ya Afrika Mashariki ingeweza kushindana nae kiuchumi. Tayari Rais Kagame, Museveni na Kenyatta wameshatoa Dola za kimarekani mil.66 ($66.7 million) sawa na shilingi za kitanzania Bil.105 kuboresha bandari ya Mombasa kupitia kile kinachoitwa Berth number 19, Mombasa port Rehabilitation. Hii inafanyika ili kuiongezea uwezo bandari hiyo ili iweze kuzihudumia nchi za Rwanda, Uganda na South Sudan kwa ufanisi. MY TAKE..!! Mipango hii inayofanywa na Kagame na wenzie binafsi naona ni usaliti. Ni usaliti kwa jumuiya ya Afrika Mashariki na Usaliti kwa Tanzania. Ukifuatilia vizuri mipango hii utagundua kuwa wanatumia tu jina Afrika Mashariki kwa manufaa yao na si kwa kwa manufaa ya jumuiya kama wanavyodai. Mnatanua bandari ya Mombasa huku mkilenga kudidimiza bandari ya Dar es Salaam then mnasema ni kwa manufaa ya nchi wanachama. Kwani Tanzania sio nchi mwanachama? Mnapanga kuanzisha ID za Afrika Mashariki ili kuwe na free movement mkidai ni kwa manufaa ya nchi wanachama lakini ukweli ni kwa manufaa ya wachache. Mi nadhani Tanzania tunahitaji kuwa makini na hizi sinema za Kagame na Museveni. Tunahitaji kuchukua hatua zaidi, tunahitaji kujipima zaidi, tunahitaji kuwa wazalendo zaidi. VINGINEVYO NAIONA HATMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI..!!
Posted on: Wed, 28 Aug 2013 09:12:09 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015