NAIROBI Serikali ya Kenya inapanga kuwa na sarafu mpya ifikapo - TopicsExpress



          

NAIROBI Serikali ya Kenya inapanga kuwa na sarafu mpya ifikapo mwaka 2015 kama inavyotakiwa na katiba mpya inayopinga kuwepo kwa picha za watu kwenye sarafu ya nchi hiyo. Katibu Mkuu wa baraza la mawaziri Bw. Francis Kimemia amesema baraza la mawaziri limepitisha mapendekezo ambayo yatakuwa tayari mwezi Mei mwaka kesho. Aidha Bw. Kimemia amesema sarafu mpya zitaonesha urithi wa Kenya na zitazinduliwa ndani ya miaka miwili. Sarafu za sasa zina sura za Rais wa Kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta, Rais wa pili Be Daniel Arap Moi na Rais wa tatu Bw. Mwai Kibaki. Bw Kimemia amesema sarafu za zamani zitaanza kuondolewa kwa awamu mwaka 2015, na kati ya sarafu mpya zitakazotolewa kutakuwa na noti za shilingi 50, 100, 200, 500 na 1000.
Posted on: Tue, 20 Aug 2013 05:12:09 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015