NAMING AND SHAMING FOR THE BETTERMENT OF UZANZIBARI NA - TopicsExpress



          

NAMING AND SHAMING FOR THE BETTERMENT OF UZANZIBARI NA UTANZANIA. "Ulaani na Uukosowe Ubaguzi,kwa lengo la kujadidisha Umoja wa Wazanzibari. Unyamazapo ndipo Uleleyapo Ugonjwa Mbovu utakao kua na madhara makubwa. Somo hilo la kutokulaani Ubaguzi wa kale ndilo lililo sababisha Misiba Mikubwa iliyotokea wakati wa mivutano ya kisiasa ya 1960 hadi January 1964 Zanzibar. "Niliambiwa haya na Marehemu Mzee Wangu mmoja,mnamo mwaka 1973 wakati nipo IDM Mzumbe Kikazi.Siyasahau maneno haya hadi hii leo .. Hivi kaaribuni nilibahatika kusikiliza ukanda wa mazungumzo ya aliyekuwa Jaji Mkuu Zanzibar Ndugu Hamid MAHMUD yeyena Mkewe. Wazanzibari hawa wawili walikuwa wanaelezea yale yote waliyo yaishi,na waliyoyaona utotoni na ukubwani mwa Zanzibar. Nimeisikiliza kanda hiyo mara mbili-tatu,na nikayalinganisha na yale yasemwayo na yale yaandikwayo na watu kama Ibrahim Noor,au ajitae Virus 99 na Aretas Harith kwenye ukumbi wao wa Zanzinet.Nikatafakari na nikajiuliza masuali mengi, miongoni mwao ni haya yafuatayo: a) Kwa nini wengi wa generation yetu yaani wale wenye umri wa miaka 50 kuendelea juu wanakubaali kua Zanzibar palikuwepo ubaguzi,lakini kundi la Wazanzibari waiishio kule arabuni hakubalia jambo hili ? b) Jee palikuwepo Ubaguzi wa Kikabila na Ubaguzi wa Kupata nafasi za Elimu ya juu na nafasi Kazi ? c) Wizi wa kura na ubaguzi wa haki za upigaji kura ulikuwepo au hauja kuepo? (Hivi sasa inasemekana hayo yapo ,lakini hii haimaanishi kuhalalisha wizi wa kale au sasa). d)Kwa nini baadhi ya Wazanzibari hasa wale waiishio Arabuni hawwapendi uhusiano wa wa kijadi wa Zanzibar na Tanganyika ,lakini wanapendelea Uhusiano na kuiinasibisha nchi yetu iwe zaidi na uhusiano na Uaarabu na Arabuni ambako nndiko walikotoka utawala wa kuwatawala Wazanzibar asili wa visiwa vya Unguja na Pemba na sehemu za pwanni ya bara la Afrika?. e)Kwa nini Washihiri,Waomani, au Wahindi wakubalike kiurahisi kuwa ni "Wazanzibari Halisi", lakini Wanyamwezi,Makonde,Makua,na makabila mengine ya Tanganyika ,Kiafrika wapagaze majina majina ya kinamna na kukumbushwa uasiliya wao na ubara,ingawaje walikuja Zanzibar kabla ya hao wahamiaji wengine wa nje kabisa ya Afrika kutoka Persia,Uhindini na Arabuni ? Kuna wakati Ali Hassan Mwinyi baada ya Aboud Jumbe nayeye baada ya Karume wote hawa walikuwa wakisemwa kua eti si "Wazanibar Halisi " wa kushika madaraka hayo ya urais ,lakini Seif Shariff na Salim Rashid Maully ,ndio walio stahiki bila ya kunasibishwa na uasiliya wao Arabuni ,kwa nini? Wakati mwengine wapo Wanzibari raiya kizaliwa au kwa tajnisi kama wengine wengi ,lakini wao hutiliwa ukasoro wa Uzanzibari wao,kwa sababu ya Dini zao za Wakristo,na sio Magoa lakini hasa ikiwa ni Waafrika. La kustaajabisha jengine nikua Mabaniani,Maparisi na Masinga singa ambao si "Waisilamu" hawajapata kutiliwa ukasoro wa Uzanzibari wala hizi chokochoko na nyoko-nyoko za mambo ya Dini au ule Uasilia wao ,kwa nini ? Jee hili ni pendeleo la Kibaguzi wa Rangi Zao ? Ikiwa ni hivyo basi ,lazima lipo korofisho la kindani ya ubongo katika siasa hizi za ubaguzi wa hao wanaochagua na kubagua "Nani ni Mzanzibari Halisi kwa misingi hii ya Ubaguzi wa Rangi au Dini? Uisilamu ,Uaarabu na Uafrika . Mbona nchi kama Mali,Nigeria,Senegal ,Somalia,Gambia ,Guinea,etc ingawaje ni nchi za waisilamu lakini hawazinasibishi nchi zao au watu wao na "Uaarabu" kama baadhi ya Wazanzibari khasa wale waiiishio Arabuni jinsi wanavyo taka kuilazimisha Zanzibar "iarabishwe "kwa misingi ya tarehe za utawala wa kigeni wenye asili za Arabuni .Tawala ambazo zinahusika na ukatili wa Biashara ya Utumwa na Udhalilishaji wa nchi zetu . Inafaa kukumbuka kua hisia na hulka za "Uaarabu" kwa kweli zina nguvu kwenye baadhi ya sehemu na hasa mjini tu yaani Stone Town na Malindi Malindi yaani ni ile " One sq.Mile ya Zainaba Badawi wa BBC . Uaarabu sio = na Waarabu kama ni kikundi cha watu . Ninaposema "Uaarabu nina maanisha hasa ile "arrogance",kiburi na ule ubwenyenye wa dharau na udhalilishaji wa Wazanzibari wenye asili nyengine zisizookua za Arabuni na Asia. Na ninaposema sema Uaarabu sio sawa na Uisialamu.Kwa sababu vitu hivyo viwili ni tofauti. Lakini kuna watu wanataka kupenya kwa kutumia uisilamu ili kukamilisha shabaha zao za kisiasa - Kuiarabisha Zanzibar na Ku-promote arrogance ya Uaarabu. Historia ya Zanzibar na Arabuni ni historia ya baina ya "MTAWALA-MTAWALIWA" . Zanzibar si sehemu ya Arabuni wala Asia,bali ni sehemu ya kimilele ya bara la Afrika . Jengine la kueleweka ni kwamba binaadam kua Muisilamu haimaanishi kuwa mtu huyo huwa anabadilika uwa ni Mwaarabu kama vile Mkrito hawezi kuwa ni Mtaliana au Mbudist wa wa Burma Kuwa Mchina. MASUALA YA DINI NA UHUSIANO WA BINAADAM AU JINSIA ZAO NI VITU VIWILI TOFAUTI. DINI MBALI NA UTAIFA AU ASILIYA ZA KABILA NI VITU TOAUTI. Kuukanya Ukweli wa Historia ya Zanzibar na Ukweli wa ule Ukatili uliofanywa kwenye Mapango ya Watumwa,na Soko la Biashara la mfumo wa Siasa Utumwa ya Zanzibar,ni kama kutaka juwa lina kucha Mashariki badalaya Magharibi.
Posted on: Fri, 28 Jun 2013 14:05:33 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015