NDUGU MUISLAM:- 1. Usipoteze muda mwingi katika usingizi ukageuza - TopicsExpress



          

NDUGU MUISLAM:- 1. Usipoteze muda mwingi katika usingizi ukageuza usiku mchana na mchana usiku. 2. Jiepushe na kumuasi Allaah kwa kukesha mbele ya T.V. 3. Usizidishe ‘Ibaadah pasipostahili mfano Sunnah za qabliyah na ba’adiyah tumeambiwa jumla ni Rakaa kumi au kumi na mbili na ukiziswali vilivyo unajengewa nyumba peponi. 4. Jiepushe na maneno ya upuuzi; kusengenya, umbea, uchonganishi n.k. Utaharibu funga yako. 5. Jiepushe na kuitumia Ramadhaan kwa kuzunguka madukani na haswa katika kumi la mwisho. 6. Toa sadaka hata kama huna mali unaweza kujitolea hata nguvu zako katika kazi au kunyesha maji na kufuturisha waliofunga. 7. Usifanye israfu katika chakula pika kiasi na usimwage utakuja ulizwa kesho neema hii. 8. Ramadhaan ni fursa nzuri ya kuhama maasi kutubia jitahidi kuendelea na moyo huu. Usihudhurie hafla zenye miziki na michanganyiko ya wanawake na wanaume 9. Anayeswali msikitini asiende na watoto wachanga wanaolia au wanaoshawishi wanaoswali atakuwa mwenye kupata madhambi. 10. Msikitini ni fursa nzuri ya kuelimisha wasiojua hukmu za Swalah na mengineyo na hili ni jukumu letu sote. 11. Walio katika siku zao za ada au Nifaas (damu ya uzazi) wasiache kusoma vitabu vyenye manufaa, du’aa, adhkaar, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam), kusikiliza Qur- aan, kuleta istighfaar (kuomba msamaha), kujiunga na wanaofuturisha watu
Posted on: Mon, 15 Jul 2013 21:58:12 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015