NGARA Zaidi ya Wahamiaji haramu elfu 2 raia wa kutoka waliokuwa - TopicsExpress



          

NGARA Zaidi ya Wahamiaji haramu elfu 2 raia wa kutoka waliokuwa wakiishi katika wilaya mbalimbali za mikoa ya Kagera na Geita wanaendelea kurejea nchini mwao kupitia mipaka ya kata ya Mugoma, wilayani Ngara. Wahamiaji hao haramu wanarejea kufuatia agizo la la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho kikwete alilotoa hivi karibuni wakati wa ziara yake mkoani Kagera la kuwataka wote wanaoishi kinyume cha sheria kuondoka kabla ya kuchukuliwa hatua Baadhi ya raia wa Burundi wanaoishi mpakani mwa Tanzania katika wilaya ya Giteranyi nchini Burundi akiwemo Iman Odas wamepongeza serikali ya Tanzania kwa kuwarudisha makwao wahamiaji haramu waliokuwa wanaishi nchini Tanzania bila kufuata taratibu na sheria za nchi Kwa upande wake afisa uhamiaji wa wilaya ya Ngara Bw Marwa Nyaswi amewataka watanzania kutowahifadhi wahamiaji haramu na kwamba atakayebainika kuwatunza atachukuliwa hatua za kisheria
Posted on: Wed, 14 Aug 2013 10:01:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015