NIONAVYO MIMI JUU YA MECHI YA MCC VS YANGA. Mchezo umemalizika - TopicsExpress



          

NIONAVYO MIMI JUU YA MECHI YA MCC VS YANGA. Mchezo umemalizika kwa sare ya 1-1 ni matokeo fair kabisa.Mashabiki wa YANGA ndiyo waliokuwa wa kwanza kuanzisha chokochoko kwa kutoka upande wao wakiwa na ngoma na bendera zao na kuwafuata wale wa MBEYA CITY COUNCIL. Baada ya gari la yanga kuingia,fans wa city walipiga mawe sana BUS hilo,hii tabia sio ya kiuana michezo kabisa.Lazima wote tuipinge.mashabiki wa YANGA walifanya hii kitu dhidi ya Coastal union na leo fans wa MCC. Hali ya mchezo haikuvutia sana kwa sababu wote hawakutengeneza nafasi za kutosha,sub ya Tegete kwa yanga ilileta uhai sana.MCC waliche vizuri sana katikati lakini hawakuwa na madhara. Naomba leo niseme wazi tu,ukiondoa SIMBA NA YANGA TANZANIA,timu inayofata kwa mashabiki ni MCC.Nimeona hili kwenye mechi zao zote 3. Wengi mnabisha lakini trust me,MCC wana fanbase ya kutosha.pamoja na ukubwa wa YANGA jezi ya purple na nyeupe ilienda sambamba na ile ya kijani na njano.
Posted on: Sat, 14 Sep 2013 16:19:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015