NIONAVYO MIMI KUFUATIA TAARIFA YA SIMBA SC NA ADEN RAGE - TopicsExpress



          

NIONAVYO MIMI KUFUATIA TAARIFA YA SIMBA SC NA ADEN RAGE WAKE. Jana Tabora Mchezaji Tambwe na Kaze walizuiliwa kucheza mchezo huo kwa sababu ITC zao toka Burundi zilikuwa hazijafika TFF na hawakuwa na vibali vya kufanyakazi hapa nchini. Jana eti mwenyekiti Aden Rage kasafiri jioni kwenda Burundi kufuatilia jambo hili na kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba sc,tayari wamekamilisha kila kitu na wachezaji hao wataanza kucheza rasmi mechi ijayo. Ninachoshangaa hapa ni kwanini SIMBA walitaka kuwatumia wachezaji hao ambao hawajakamilisha taratibu zote kisheria pale TFF? Halafu mtu anakwambia Club inauongozi imara,upi?? Nadhani simba wangeandaa timu ambayo haina hao wachezaji wawili then mechi ikapigwa bila tatizo lolote na bila kupoteza kama ilivyokuwa jana pale Tabora. Sasa kama simba walikuwa kabisa na uhakika kwamba Tambwe na Kaze hawajakamilisha taratibu,walikuwa na nia gani walipotaka kuwatumia??? Ndiyo maana tunataka kila mtu ashangilie timu ya nyumbani kwao ili haya #majanga tuwaachie tu wazawa na wakazi wa Dar.
Posted on: Sun, 25 Aug 2013 12:36:25 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015