Naibu rais kwa mara nyingine tena amewanasihi walimu wanaogoma - TopicsExpress



          

Naibu rais kwa mara nyingine tena amewanasihi walimu wanaogoma kuketi kwenye meza ya mazungumzo na serikali ili kutoa fursa kwa serikali kutekelezwa mahitaji yao.Naibu rais ameelezea kusikitishwa kwake kuhusu msimamo mkali unaoshikiliwa na walimu wakiongozwa na chama cha KNUT badala ya kufanya mashariano na serikali ya Jubilee ambavyo wamekuwa wakifanya na serikali zingine zilizotanguliwa.Wito huu unajiri wakati ambapo walimu wamesema mgomo rasmi utaanza Jumatatu hii baada ya serikali kuharamisha mgomo huo na zaidi kutupilia mbali mwafaka baina yao na serikali ulioafikiwa mwaka 1997.
Posted on: Sun, 30 Jun 2013 08:39:51 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015