Najaribu kupanga kikosi cha Man Utd cha mauaji. Kikosi chenye - TopicsExpress



          

Najaribu kupanga kikosi cha Man Utd cha mauaji. Kikosi chenye uwezo wa kuifunga club yoyote duniani. Kila nikiumiza kichwa naona siwezi kupanga kikosi changu na kumuacha Valencia nje. Siwezi kabisa kucheza hii kamari, bora niliwe lakini siwezi kumuacha Valencia. KWA NINI VALENCIA?? -Anakaba na kushambulia.. Sifa hii inamfanya Rafael kucheza kwa kujiamini na kuamini uwepo wa Valencia unaweza kumzuia makosa yake pindi yanapotokea. Valencia anapougusa mpira basi Rafael upanda mbele kwa mwendo wa kasi kitu kinachosaidia kuongezeka kwa mashambulizi upande wa kulia. -Assist inaweza kutokea muda wowote. Mara nyingi mfumo wetu utegemea mawinga kufanya mashambulizi. Carrick anaweza kumchungulia wakati wowote na kumletea pasi ndefu. Rooney anapouchukua mpira kati mara nyingi akili yake inamuwaza Valencia. Mashambulizi haya yanaweza kutengeneza assist yoyote na kuwafanya mafoward wetu kufunga kwa urahisi. -Ujio wa Fellaini.. Valencia anakaba kulia, Fellaini anakaba kati. Valencia anashambulia kulia, Fellaini anashambulia kati. Valencia anafanya vurugu kulia, Fellaini anafanya vurugu kati. Mapacha wenye style moja. Pindi Valencia anaposhambulia basi Fellaini inakua rahisi kukimbilia kati kusubiri cross ili afunge kwa kichwa au miguu. -Anaweza kufit mifumo yote.. Iwe 4-4-2, 4-2-3-1, 4-3-3, 4-5-1 na mengineyo. Kama kocha atawapanga Carrick na Cleveley kwa pamoja dimba la chini na Fellaini akasimama peke yake dimba la juu basi Valencia anahitajika sana kwenye kuongeza mashambulizi. Fellaini atakua na kazi moja ya kugawa kulia na kushoto. Upande wa kulia utaluwa mwepesi kwa sababu Valencia pia upenda kusogea kati kuanzisha mashambulizi. -Anajituma na hachoki.. Akiwa kwenye hali nzuri Valencia ni mwiba sana kwa wapinzani. Pumzi na nguvu ni vitu vya kipekee alivyobarikiwa navyo. Sifa hizi zinaniaminisha anaweza kufanya lolote pindi wapinzani mpira wa kukamiana au anaweza kuongeza mashambulizi zaidi pindi wanapoanza kuchoka. *Binafsi hizi ndio moja ya Sababu ninazoziona bila ya Valencia, Man Utd huwa tunapata tabu kwa kiasi fulani. Wapo wengi wazuri kama Nani, Kagawa na Young ila sina uhakika kama wanaweza kucheza mechi 10 mfululizo kwa kiwango sawa kwenye upande wa kwake!! =/ D.P /=
Posted on: Sat, 07 Sep 2013 20:14:01 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015