Nampongeza Bernard Membe kwa hatua ya kwanza ya kukir kuwa Article - TopicsExpress



          

Nampongeza Bernard Membe kwa hatua ya kwanza ya kukir kuwa Article 41(1) ya mkataba wa kimataifa wa Vienna (Viena convention) ilivunjwa kama tulivyosema jana kuhusiana na balozi .Namnukuu ‘Wizara inapenda kutamka kwamba kitendo cha Balozi yoyote kuhudhuria mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kuvaa sare zenye nembo ya vyama vya siasa siyo sahihi na kinakiuka Kifungu cha 41(1) cha Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961, unaoongoza uhusiano wa kidiplomasia’’.He nailed it!Nampongeza kwa Kuisimamia Shahada yake ya Uzamili (M.A International Realations) aliyoipata pale Chuo kikuu cha John Hopkins Nchini Marekani,Ningemshangaa maana angefanana na Mwenzake aliyeshindwa kufuata sheria na kushindwa kusimamia mkataba mmoja tu wa RICHMOND pamoja na mamlaka makubwa ya Uwaziri mkuu. Sasa hatua kali zichukuliwe kuhusu hili ili tusimdharau na tuamini kwamba kweli ana weledi wa kutosha.Kilichovunjwa sio mkataba wa Vienna tu bali sheria zote za kimataifa(International law) zimevunjwa ikiwamo UN Charter,The Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961,Sheria mama ya nchi (Katiba ya Tanzania,1977) na Act No.5 of 1986(iliyotungwa kwa ajili ya kuhalalisha kinga za kidiplomasia baada ya ratification ya Vienna convention),hatua za kisheria zichukuliwe mara moja dhidi ya Balozi wa China.Aidha,Bwana Kinana na wenzake wawajibishwe kwa mujibu wa sheria za nchi ili iwe fundisho kwa wengine wanaoingilia mambo ya ndani ya nchi kinyume cha sheria za nchi na za kimataifa. Tuachane na na kauli za Nape kwa muda maana huyu ni msemachochote ila Naamini Katibu Mkuu wa CCM Bwana Kinana,amefanya makusudi kwa nia ya kujinufaisha chama chake kisiasa akidhani kuwa wasukuma ni watu wasiojua mambo.Hii haina maana kwamba hajui taratibu za kidiplomasia na sheria zake ukizingati kuwa amekuwa mbunge kwa muda mrefu,na hata kuwa Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC),ambapo alikuwa ana-enjoy immunity on the inviolability of premises under Article 22 of the Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961. Vijana wa CCM na Katibu wa itikadi na uenezi sitaki kuwakejeli kwa kuwa naamini hawa ni mojawapo wa wale wanaohitaji shule.Naamini tamko la Membe halitawafanya sasa muanze kutoa kauli za ovyo kwamba ni ‘mzee anayesubiri kufa’.Turudi sasa darasani . Kauli za Nape kuwa balozi alifanya vile kwa sababu ya uhusiano kati ya chama chake na CPC cha China ni kauli zinazoashiria mawazo mgandao na propaganda za kiwango cha chini zisizoendana na wakati huu wa siasa za kidigitali.Hata kama hajasoma International relations kuna njia nzuri zaidi ya kufanya spinning bila kuonyesha umbumbumbu wako katika Nyanja hizi.Balozi hawakilishi chama cha siasa.balozi anawakilisha nchi na masuala ya uwekezeja ni masuala ya kisera yanayohusu nchi.Angeuliza hata kwa Mama Migiro(katibu wa mambo ya nje wa chama chake) kuliko kuingilia kazi yake.Kijana mwenzetu huyu arudi darasani au ajikite kwenye kazi (anayomudu kama anavyoonekana pichani) Tunajua kuwa kuna aina mbili za immunities ambazo ni ratione persona(Hizi anazo balozi huyo) na ratione materiae ambazo ni kwa mujibu wa Article 27 of the Rome Statute, Vienna Conventions on Diplomatic Relations of 1961 and Vienna Convention on Consular Relations of 1963. Kauli kuwa Balozi huyo pia wakati mwingine anawapa ushauri ni kauli ya kijinga kuwahi kutolewa majukwaani.Kauli hii sasa itamuumiza Balozi wa China zaidi maana kwa mujibu wa ibara ya 31 ya mkataba wa Vienna(1961) imekataza kitendo hiki.Mwanadiplomasia yeyote haruhusiwi kufanya kazi kinyume na zilizoorodheshwa ibara ya 3 vinginevyo kinga hiyo itaondoka.Ushauri unaweza kuwa ‘consultancy’ na hiyo ni commercial activity.Mwaka 2007 Ethiopia ilifukuza wanadiplomasia 6 wa Norway,Sudani pia ilifukuza wanadiplomasia wa Canada. Kitendo cha balozi kitapelekea sasa turudi kwenye kipengele cha ibara ya 9 ya mkataba huo huo katika extreme measures cha kumtangaza persona non grata(neon la kilatini linalomaanisha ni mtu asiyetakiwa nchini).Ili hatua hii ifikie Nchi iliyomleta(katika hili maanake China) itaamua kumuita nyumbani haraka maana muda ukipita ataondolewa kinga na anaweza kushtakiwa na ikawa fedheha kwa Taifa husika. Kurt Weldheim aliyekua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baadae Rais wa Austria aliwahi kutangazwa Persona Non grata na Marekani kwa kosa moja kuu kwamba wakati akiwa madarakani alitambua uhalifu wa chama cha NAZI cha Ujerumani cha Adolf hitler lakini hakuchukua hatua. Mwaka 2008,Rais evo Morales wa Bolivia(Mwanamapinduzi ninayemhusudu) alimtangaza Balozi Philip Goldeberg wa Marekani kuwa ni persona non grata kwa kosa la kutoa ushauri wa kisiasa kwa baadhi ya vyama vya siasa na balozi Duddy akafukuzwa pia nchini Venezuela kwa Comrade Hugo Chavez kipindi hicho hicho Kwa mujibu wa sheria za Kimataifa na duru za kidiplomasia haihitaji sababu au maelezo katika hili.Sasa kwa hoja ya ushauri wa kisiasa aliyotoa Kijana Nape naomba sasa atafakari tena kauli yake wakati tunaendelea na mchakato wa kumwajibisha Balozi huyu.Hapa chini nimemuwekea ibara ya 31 ya mkataba wa Vienna pamoja na Ibara ya 42 inayokataza kujihusisha na commercial activity maana ushauri wa kitaalamu atakua analipwa Diplomatic agents “shall also enjoy immunity from civil and administrative jurisdiction,” except in the case of: (1) “A real action relating to private immovable property situated in the territory of the receiving State, unless he holds it on behalf of the sending State for the purposes of the mission,” art 31.1(a); (2) “An action relating to succession in which the diplomatic agent is involved as executor, administrator, heir or legatee as a private person and not on behalf of the sending State,” art 31.1(b); or, (3) “An action relating to any professional or commercial activity exercised by the diplomatic agent in the receiving State outside his official functions.” art 31.1(c). Of course, the diplomatic agent shouldn’t be involved in professional or commercial activity for profit per art 42. The United Nations Vienna Convention on Diplomatic Relations (1961) recognizes that there is no unilateral right to diplomatic relations between or among states. Such relation exists only by consent. And a receiving state can, without giving any reason, declare any member of a diplomatic mission a persona non grata, especially when the diplomat commits a serious offense that threatens the peace and security of the state, or where he or she interferes in the internal affairs of that state
Posted on: Tue, 17 Sep 2013 16:43:48 +0000

Trending Topics




© 2015