Naomba tusome hapa na tusaidiane: 1. Katibu mkuu wa ccm na - TopicsExpress



          

Naomba tusome hapa na tusaidiane: 1. Katibu mkuu wa ccm na katibu wa itikadi na uenezi taifa ccm waliambatana na balozi wa china katika kukitangaza chama, kinyume na utaratibu(Against the vienna convension of 1961)Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, akakemea vikali jambo hilo. Katibu wa uenezi akaja na kusema waziri alishauriwa vibaya, kwani balozi alikuwa sahihi. 2. Mwenyekiti wa wazazi taifa ccm akiwa mkoani Tanga alimshambulia mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Warioba kwa maneno makali, katibu uenezi taifa akasema sio msimamo wa chama. 3. mawaziri chikawe, wasira na lukuvi mara kadhaa wamenukuliwa wakisema serikali haina haja ya kukutana na wapinzani na kuzungumzia muswada wa sheria ya katiba, mwenyekiti taifa ccm, rais kasema serikali ipo tayari. KWA MIFANO YA MIKANGANYIKO HII TUMLAUMU NANI? TWAWEZA KUKAA NA KUPANGA MAMBO YA MAENDELEO NA KUYASIMAMIA?
Posted on: Sun, 06 Oct 2013 08:00:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015