Ndio maana Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) akasema, Kile ambacho - TopicsExpress



          

Ndio maana Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) akasema, Kile ambacho hakikuwa Diyn wakati ule (karne tatu), hakiwezi kuwa Diyn leo hii Anakusudia, kuwa chochote ambacho hakikufundishwa au kufanywa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake na karne mbili bora alizozitaja baada yake, basi hakiwezi kuwa ni jambo katika Diyn leo hii. Mfano wa mambo mengineyo yaliyokuja baadaye ni kama Khitmah, Talaqini, Kutazamia katika ndoa, na Mawlid ambayo yalianzishwa na Mashia karne ya nne na saba baada ya Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam). Mfano wa hilo la kuweka neno TAALA pasipo pahala pake, ni mfano wa kuweka neno SAYYIDANA kwenye Tashahhud wakati tunasema Ash-hadu Anna Muhammadan Abduhu wa Rasuuluh kwani sipo palipofundishwa kuwekwa neno SAYYIDANA. Lakini haikatazwi kwenye Khutbah, mawaidha au katika maongezi mtu anapomtaja Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) akasema Sayyiduna Muhammad. Na mifano ni mingi. Na huenda matatizo mengi ya kuzushwa mambo, kuongezwa, kuzidishwa na kuchomekwa katika Diyn, sababu yake kubwa ni watu kudhani wanapendezesha lile jambo, kulitia nakshi, kulivutia, kulifanya liwe la aina yake tofauti na mazoea, kudhani atapata thawabu zaidi n.k. n.k. Lakini hajui mtu kuwa kufanya hivyo ni kutumbukia katika Hadiyth hizi mbili nzito kabisa: Kutoka kwa Mama wa Waislamu Ummu ‘Abdillaah ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye alisema, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Yule anayezua kitu kisichokuwemo (kisichokuwa) katika jambo (DINI) hili letu kitakataliwa.” Al-Bukhaariy na Muslim “Yule anayetenda kitendo ambacho hakikubaliani na jambo (DINI) letu kitakataliwa.” Muslim Bila shaka hayo yatakuwa yameweka wazi utata wako katika matumizi ya TAALA’ katika Salaam.
Posted on: Sat, 19 Oct 2013 20:50:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015