Ni unafiki kususia vikao vya bunge kwa kisingizio kuwa CCM - TopicsExpress



          

Ni unafiki kususia vikao vya bunge kwa kisingizio kuwa CCM wamechakachua Muswada wa KATIBA, wakati Katiba ya chama chenu (CDM) mmeichakachua. Ni unafiki kukemea MAFISADI, wakati VIONGOZI wa CDM ndio MAFISADI wakubwa (RUZUKU,MISAADA na SADAKA). Unapata wapi ujasiri wa kukemea watu walioweka PESA Uswiss wakati kiongozi wako yumo kwenye list ya watu wenye PESA CHAFU. Unapata wapi ujasiri wa kwenda IKULU wakati humtambui Rais na ulimsusia kwenye kikao chake cha kwanza cha uzinduzi wa Bunge. Kama si ULAFI wa MADARAKA, uongozi wa CDM unasita nini kutangaza uchaguzi wa chama, wakati muda wa viongozi waliopo madarakani umeisha kwa mujibu wa KATIBA yenu…? Je kama leo hii mmeshindwa kuwatendea HAKI wana chadema mtaweza kuwatendea haki watanzania..?
Posted on: Tue, 05 Nov 2013 17:53:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015