Ni vigumu sana kuamini mpiganaji wetu, mzalendo wa maa na - TopicsExpress



          

Ni vigumu sana kuamini mpiganaji wetu, mzalendo wa maa na mwanaharakati mpendwa Oleparkipuny kuwa amefariki. Tumemteza mtu makini mwenye kujali utu wa binadamu, mwenye kujali maslahi ya wananchi wake, siku sote aliamini katika usisi badala ya umimi, sitoi sifa marehumu ila Oleparkipuny atabaki kuwa alama isiyosahaulika si tu kwa wilaya ya ngorongoro pia kwa Tanzania nzima na nje ya nchi. zaidi ya yote naomba tuige uzalendo wake na uhanarakati wake katika kutetea maslahi ya jamii yetu hasa katika kipindi hichi cha mageuzi kifira na jamii inayojali usawa. Kifo chake kimenihuzunisha sana ila fikra zake zitaishi mioyoni mwetu, Naamini fikra zake zitazalisha wazalendo wengi na ambitious kama yeye. Famalia ya mpendwa wetu tupo pamoja. Rest in Peace Mzee wangu.
Posted on: Mon, 22 Jul 2013 18:56:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015