Nilikuwa naangalia ukurasa wa kaka Mwalimu Dickson Cornell - TopicsExpress



          

Nilikuwa naangalia ukurasa wa kaka Mwalimu Dickson Cornell Kabigumila... Halafu nikapitia ukurasa wa dada Upendo Benson Nikarukia ukurasa wa Mchungaji Eresh Tchakubuta Sikukaa nikatua kwenye ukurasa wa Buberwa Mwemezi Muda ukaniruhusu kufika kwenye ukurasa wa kaka Enoce Lazaro.... Kwa mwendo wa pole nikajikongoja kwenye ukurasa wa Aron Makukura Nikapinda kona nikatokea kwenye kasri ya Bwana Rashid Tumbo.....nikakaa hapo kwa dakika kadhaa kasha nikaondoka kwa furaha maana IPO taarifa ya kumpa Mungu utukufu hapo.....dakika moja baadae nilikuwa kwenye milki ya Kaka mkubwa Adam Michael.....nikatoka hapo na kurudi kijijini kwangu.NAOMBA NIELEZE NILICHOJIFUNZA KWENYE ZIARA YANGU 1.Hiki ni kizazi kipya cha wokovu.Injili ya Yesu inatandikwa kila kona na majeshi ya Bwana yako sawa kila muda 2.Sote tunaandika,lakini hakuna anayeweza kukaa ndani ya upako wa mwenzie,Mungu anaachilia vitu na uweza wa ajabu kwa kila kijana mwenye kutii neno lake 3.Tunaweza kuitetemesha Dunia mno kama ikitokea siku moja vijana wote tuliookoka Tanzania tukiamua kufanya maombi ya MAPINDUZI kwa pamoja HEBU NA WEWE TUMIA MAJINA HAYO KAMA KIANZIO KUPATA MTAZAMO WA VIJANA KWA HABARI YA UFALME WA MUNGU HALAFU UNIAMBIE JAPO JAMBO MOJA ULILOJIFUNZA. BARIKIWA
Posted on: Sat, 05 Oct 2013 06:47:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015