Nilikuwa nawaza kuwafananisha Al-Shabaab na Driving Schools nyingi - TopicsExpress



          

Nilikuwa nawaza kuwafananisha Al-Shabaab na Driving Schools nyingi zinazowafundisha watu kuendesha magari jijini Dar es Salaam na miji mingine katika Tanzania yetu lakini nikaona walau kuna tofauti fulani. Utakuta mtu ndiyo kwanza anaanza kujifunza kuendesha gari, lakini ndani ya gari hilo kuna wanafunzi wenzake zaidi ya watano! Jamani, Mwanafunzi huyu anawezaje kupakia abiria wengi hivyo kama sio kuhatarisha maisha ya watu wengine! Kwa mfano ajali ikitokea hapo nani alaumiwe; Mkufunzi, Mwanafunzi, Abiria, Askari wa Usalama Barabarani au Mmiliki wa hiyo Driving School? Wahusika fanyeni tafakari na mchukue hatua kabla hatari haijatokea, vinginevyo "litakapotokea la kutokea" sentensi zenu hazitakuwa na mashiko.
Posted on: Fri, 27 Sep 2013 12:59:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015