Nilipokea huu ujumbe 30/10/2005 Nikadhani ni ishu ya uchanguzi - TopicsExpress



          

Nilipokea huu ujumbe 30/10/2005 Nikadhani ni ishu ya uchanguzi ndio italiibua hili, lakini ukiangalia haigusii uchaguzi ila kuitaka Tanzania itubu. TUKIWA KATIKA KULIOMBEA TAIFA 2005/2006 akatokea mwingine akasema UKIONA RWANDA WANAJIINUA JUU YA TANZANIA UFAHAMU HIYO HUKUMU IMEFIKA NA NI MKONO WA BWANA KUITAKA TANZANIA ITUBU. . Soma na upime na wewe ------- Nawaarifu ndugu zangu katika Mwili wa Yesu. Ghadhabu kuu ya Mungu imekalia taifa hili siku si nyingi zijazo. Kila atakayepata ujumbe awaarifu wateule popote waombe. Ni upendo wa Mungu kwamba hafanyi jambo kabla ya kuwaambia watu wake. Anazo sababu kuu tatu kwa nini anaipiga Tanzania. Watu wamezubaika kwa kuwaza kiko wapi kile cha Tanzania itubu! Kiko wapi nabii zilizokuja baadaye kuhusu taifa hili! Mungu anasema hatanii ghadhabu yake inakuja, inakuja na si muda mrefu tanzania haitasalia, amani haitakuwepo Kwanza: Ndani ya kanisa kumekuwepo na zianaa na uasherati ambao hata kwa mfano wa mataifa haupo. Viongozi wengi wamekuwa wazinzi hakuna mfano wake. Kondoo kwa kondoo ni zinaa na kutamaniana kusiko na mfano. Uovu umejenga nyumba ndani ya kanisa tanzania. Pili: Ibada za miungu zimekithiri katika taifa hili. Kiwango chake hakijawahi kuwa kikubwa kama ilivyo hivi leo. Watumishi wengi wanatumia nguvu za giza na wengi wanafikiria kwamba ni Bwana. Mungu anakwenda kupukutisha wote na kuweka yote wazi. Vikindi vingi vinavyojiita ni vya Kristo sivyo. vinawaongoza wengi kwenye upotevu, na ukengeufu mkuu. Wateule kanisa la kweli tupo na hatufanyi lo lote. Kanisa limeacha kusoma na kutafakari neno la Mungu. Watu wanaomba sana, lakini hawasomi neno. Mungu anawatafuta wale wanaoliangalia neno lake na kulitenda. Amemtuma yule yule aliye mtuma INDONESIA kuwaambia kwamba zinaa na uchafu unatendwa katika visiwa vile umekidhiri na anakwenda kuwafutilia mbali. Watalii walitumia kisiwa cha ACHE kwa zinaa za kila namna. Kisiwa hiki ndicho kilicho zamishwa kabisa na kutoweka. Kisha akamtuma kwa ile miji miwili ya USA iliyopigwa na vimbunga kwamba zinaa na usherati wake umefikia kikomo anakwenda kuwa piga. Hawakusikia na ikawa hivyo hivyo. Na anasema bado ataendelea kuleta maafa na mapigo sehemu sehemu katika maeneo ya amerika. Ametokea Pakistani alikokwenda kuwaambia kwamba Mungu anawapiga kwa sababu ya ibada za miungi na sanamu. Kabla hata hajaondoka huko tetemeko likapiga eneo ambalo limekidhiri kwa uovu huo. Amerudi atulie nyumbani kwao kenya Mungu akamwambia nenda Tanzania. NIMEFUNIKA ANGA LAO TAYARI KWA HASIRA YANGU, WATUBU. NAWAAMBIA YA RWANDA NA BURUNDI, KONGO NA UGANDA ZILIKUWA HERI. "Tanzania HAITASIMAMA." Tuko kwenye kuomba na kumlilia Mungu. naomba jiunga nasi NDUNGU Zangu. Weka mtandao yenu tayari kwa miezi hii hadi december mpokee kila tunachosikia. nawakutumia njia nzuri ya kuweza kuiosoma biblia na kuielewa. Nawakuomba msome neno kwa bidii, hii si hiari ni lazima, hakuna muda wa kungojea. Omba, omba omba hali ni mbaya. Wewe ni shahidi ya hayo anayosema Mungu yako kwenye kanisa. Uliwahi kuona wapi nyimbo za kumtukuza Mungu zinachezwa kama dansi, na wingi wa watu wanaohururia ni mkubwa kuliko hata dansi za kidunia! hushangai! tumeingiliwa kila mtu amombe kwa kumaanisha toba haswa. ------- ikazeiwacu.unblog.fr/2013/07/04/kagame-publicly-threatening-to-hit-president-kikwete/ . TUSIMAME KATIKA ZAMU ZETU KULIOMBEA TAIFA SI MZAHA
Posted on: Tue, 09 Jul 2013 21:26:44 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015