Nimeangalia maonesho ya Nane nane - Dodoma na nimepata wazo. Kwa - TopicsExpress



          

Nimeangalia maonesho ya Nane nane - Dodoma na nimepata wazo. Kwa kuwa haya ni maonesho ya wakulima na nia yake ni kumuendeleza mkulima na kumpeleka kwenye kilimo bora basi tuhamasishe wakulima halisi kuja kutemeblea maonesho hayo ili wapate elimu juu ya kilimo. Nimeyasema haya kwa sababu ukiangalia mazao ya mfano yanayooneshwa pale ni mazuri na yanavutia ila ukitoka kidogo nje ya viwanja takribani km 1 unakuta kilimo hafifu na kisichoweza kumkomboa mtanzania. Nini kifanyike : Tusiishie kwenye maonesho tu bali twende vijijini baada ya maonesho tuwafunde wakulima kutumia njia za kisasa kilimo. Nje kidogo ya viwanja vya nzuguni kuna wakulima wadogo wadogo wanaolima mboga mboga. Wateja wakubwa wa mazao yo ni wanachuo kilichopo pale. Wakulima hawa kama wangepewa elimu ya kutosha basi wangejikomboa. Pili; pale kuna wafugaji ila mifugo yao naiona haina afya bora (yaani mifugo ile si bora) Kama maafisa mifugo wakifika kijiji hicho na kuwapa mbinu za ufugaji bora hawa watajikomboa kwani wanafunzi wale watanunua maziwa na nyama. Eneo hili lina maji ya kutosha (chemi chemi) kwa hiyo wanalima muda wote/hawana majira maalumu ya kulima kwani wanategemea kilimo cha umwagiliaji. Pia wana soko la uhakika kwani chuo kile kina wanchuo karibu 800 na ni km chache kufika Dodoma mjini. Kutoka mjini kufika eneo hilo ni sh 400 hivyo inaghalimu sh 800 kwenda na kurudi, sijuhi kwanini maafisa kilimo wa manispaa hawaendi kule kutoa msaada. Sijuhi Almashauri hii inamsubiri JK ili awaamuru waende kule? Siamini kama Diwani wa eneo hili haoni njia za kuwakomboa wakulima hawa waliozungukwa na fursa nyingi kiasi hiki lakini wakiishi ktk lindi la umaskini. Maana hata ukifuga kuku unatoka kwani kuna soko la mayai kutoka kwa wanachuo. Nina mengi ya kuandika kuhusu eneo hili lakini sitaki kuwachosha wasomaji... Kwa hali hatutatoka kwenye kichwa cha UWENDA WAZIMU.
Posted on: Wed, 07 Aug 2013 13:14:53 +0000

Trending Topics



iry Alaa El Ghoul

Recently Viewed Topics




© 2015