Nimeshtushwa kuona kitendo alichokifanya mwimbaji wa kizazi kipya - TopicsExpress



          

Nimeshtushwa kuona kitendo alichokifanya mwimbaji wa kizazi kipya anaetambulika kwa jina la Diamond Platinum, limekuwa jambo la kuzungumzwa vibaya, na kubezwa kwa kweli huu si uungwana, na kuwakatisha tamaa vijana wenye moyo wa kujitolea kwa wazee wetu ambao wao ndiyo kandiri iliyowamulikia njia hata kufika hapo walipofika. Wenzetu wenye gazeti walioanza kumhukumu Diamond Platinum wanajua yale aliyoyapitia katika malezi yake mpaka kufikia hapo? Wanajua kipi kilichomfanya asiendelee na elimu? Nani asiyejua kuwa Diamond alipotokea? Mbona hatuwalaumu wale waliokuwa na dhima na ya kumlea Diamond? Kosa lake nini? Kwangu mimi vijana hawa wawili watabaki kuwa mfano wa kuigwa, kwa kitendo chao walichokifanya kwa kuonesha kuguswa kwa namna moja ama nyengine, namzungumzia yule Bint aliyekwenda kumlipia faini msanii mwenzake na kumweka huru, nani asiyejua kuwa jela mbaya? Wangapi wana mapesa kuliko hawa watoto na nini walifanya kuonesha utu wao kwa wengine? Mtake msitake bado watabaki kuwa mashujaa wa kizazi hiki walionesha njia kwa wengine, nao si wengine bali Wema Sepeku na Diamond Platinum. Acheni chuki na roho na mbaya aliyepewa kapewa hapokonywi, bure mtakesha mkiwadhalilisha na kuwaanika kwa mabaya, kama mabaya mazuri wangeyafanya hadharani, lakini kwa fahamu zao zilizosalimika hata pale wanapotaka kufanya mabaya yao hujificha iweje mkayaanike magazetini? Yaani hamna mazuri yao mkayaandika ila mabaya yao? Kama si chuki wivu na choyo ni kitu gani? Hii inaonesha kiasi gani wazazi wamejitahidi kuwafunza utu na uungwana, wanastahili pongezi na si kuwajengea hasama na nakama ndugu marafiki na jamaa zao, huo ni udhalimu na dhulma kubwa mnayowafanyia. Serikali ambayo imemtumia Mzee Chongo kwa miaka dahali hawakukumbuka kumpa japo sindano akashonee mashati yake pale yatakapotatuka, mnakimbilia kuwakatisha tamaa wale waliiona mchango wa Mzee Gurumo, ili wasijiyokeze wengine, au mlitaka alilete gari kwenu kisha mjitangaze kuwa mmeshirikiana kumtunza Mzee Gurumo kwa kutambua mchango wake? Acheni uhasidi Diamond ameonesha njia. Wanaokubeza na wakubeze lakini umma wa watanzania unatambua utu wako na histori itabaki kuwa hivyo kamwe haitafutika kwa nyoyo zao mbaya, wao wabaki kukuwinda mahotelini waone umeingia na nani wauze magazeti yao. HONGERA SANA DIAMOND KWA UKARIMU NA UUNGWANA WAKO
Posted on: Tue, 03 Sep 2013 06:00:32 +0000

Trending Topics



cursive writing and its
This is the Liberal Legacy and Utopia......we dont have to wait

Recently Viewed Topics




© 2015