OMBI MAALUMU:Ewe Mwenyezi Mungu uliye mwingi wa rehema,tunashukuru - TopicsExpress



          

OMBI MAALUMU:Ewe Mwenyezi Mungu uliye mwingi wa rehema,tunashukuru kwa ulinzi wako na kutupatia kibali cha kuamka salama,tunajua ni wengi walipenda waamke salama lakini wameshindwa.Si kwamba sisi tumekutenda sana mema bali ni kwa upendo wako tu.Tunakuomba uzidi kutupa maisha marefu,akili,upendo na mshikamano.Uwabariki viongozi wetu wa dini na serikali ili wazidi kutuongoza katika haki,kweli na amani.Uwape hekima na busara za kudumisha umoja na amani,uvibariki vyombo vya ulinzi na usalama,uwalinde askari wote wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ),ulinzi wa raia na mali zao.Uwakumbuke wale wote wenye kesi katika Mahakama mbalimbali,watendewe haki kwa mamlaka yako.Uwasaidie walio katika ndoa,mahusiano na uchumba wazidi kuwa waaminifu,wakiheshimiana na kupendana kwa dhati.Utumbuke hata tusiooa ili tuzidi kukuomba Wewe upate kutuchagulia wenzi wakweli na waaminifu huku ukituepusha na vishawishi mbalimbali.Kama tulivyo na mapungufu kwa udhaifu wa mioyo yetu,utupatie hata yale tuliyoyasahau.Amen Amen!
Posted on: Fri, 26 Jul 2013 04:42:07 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015