POLENI NA MAJUKUMU NDUGU WASOMAJI, NAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA - TopicsExpress



          

POLENI NA MAJUKUMU NDUGU WASOMAJI, NAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KUWALETEENI SEHEMU YA SABA YA TAMTHILIA HII YA GENIUS LOVER, HII IMESABABISHWA NA SHUGHURI ZA KIMASOMO, ATUMAHI MMENIELEWA. SEHEMU YA SABA YA TAMTHILIA YA GENIUS LOVER. SEHEMU YA SABA Paul Ernest ni kijana wa miaka 23 aneyefanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi jijini Dar es salaam, anaishi nyumba moja iliyopo mtaa wa Mabibo na rafiki yake Samwel. Paul ametokea kumpenda binti mrembo mwenye kila sifa za kuvutia anayeamini kuwa anaitwa JULIETH, Julieth ni binti mwenye uzuri usio elezeka na wakupitiliza. Paul ametambua kuwa Julieth ni ndugu na Anna, hali hii imemchukua Paul kufanya uchunguzi wa karibu ili apate kumtambua na kumjua mrembo huyo wa furaha ya maisha yake ili ikiwezekana awe wake maishani. Paul ameamua kumfata Anna hadi mtaa wao wa Mwananyamala kisiwani na akafanikiwa kuingia ndani kama malengo yake yalivyokuwa; Mlinzi ambaye alishatoka njee kumsevu Anna akiwa pembeni ya Geti akafungua mlango Anna na Paul wakaingia ndani, wakisindikizwa na bustani nzuri ya kuvutia iliyopambwa na maputo yaliyosinyaa yakionesha kuwa yapo nje kwa muda usiopunguwa siku moja. Basi Paul akakaribishwa ndani na Anna mpaka sebureni kisha akaketi kwenye sofa la ngozi lililofanana na rangi ya ukuta na mapambo ya mengine pale sebureni. Anna; unatumia kinyaji gani Paul? Paul; naomba maji tu. Anna akamtengea maji Paul kisha akamkaribisha. Anna; karibu. Paul; ahsante sana. (akanyanyua glass na kuielekeza mdomoni) Wakati Paul na Anna wapo sebureni, sauti ya viatu vya kike vilisikika vikishuka ngazi kuelekea sebureni, na Paul akanyayua macho kutazama ni nani mwenye mpishano wa atua nzuri hivyo kama inavyosikika masikioni mwao, mara akatokea msichana mzuri wakuvutia aliyemwacha Paul mdomo wazi na kumfanya ashindwe kumeza maji kwa mshangao. Mara sauti iliyo raini na yakuvutia inayofanana na mlio wa kinanda ikasikika. July; hoo Anna umesharudi, mbona sijasikia mlio wa gari? Au hujarudi na mama? Anna; ndiyo mama yupo kwenye kikao kwahiyo ameniambia nitangulie. July; okay arafu nimesikia yowe la mwizi maeneo ya karibu sijuhi nani yamemkuta? Anna; haa haa haa si unajua mtaa wetu nao, yaani we hacha tu ilikuwa kidogo simu yangu iende, yaani bila Paul sijuhi ingekuwaje? ( huku bado Julieth akiwa bado ajatambua kuwa kuna mtu sebureni zaidi ya Anna, huku Paul akiwa bado anaonesha uhodari wake wa kumshangaa mrembo Julieth). July; unasema ni wewe? Mh .. na huyo Paul wa kukusaidia wewe huku mtaani ametokea wapi? Husiniambie shujaa wako wa mtaani baada ya kukusaidia akakutajia na jina? Usije niambia pia akachukua na namba yako ya simu kisha akataka kukutoa out na…( sauti ya Anna ikasikika ikimkatisha Julieth). Anna; embu acha fikira zako dhaifu, naomba nikutambulishe kwa Paul.( Anna akanyoosha mkono wake wa kulia kuuelekeza maali alipokaa Paul, mara uchangamfu wote wa Julieth ukaishia tumboni na ukimya ukamtawara huku akigeuza sura kumtazama Paul). Julieth msalimie Paul basi! Kimya kilitawara kwa kitambo kidogo kisha sauti ndogo ya uchovu mithiri ya mtu mwenye kikoozi ikasikika. July; mambo! Paul; kimya ( akiwa bado ndani ya mshangao mzito uliotawariwa na kumbu kumbu za Mlimani City na ndoto nyevu ya usiku uliopita). Anna; sasa nyie naona mna yenu, hee Paul unaslimiwa!( Paul akakurupuka kutoka kwenye mshangao na kumtazama Anna). Paul; nam unasemaje? ( akiwa nje ya kumbu kumbu, Anna bila ya kujizuia kicheko kizito kilimtoka). Anna; we Paul nashindwa kabisa kukuelewa, ukiwaona watu wa familia yetu uwa unashangaa sana, kwani kuna nini? Mwanzo ilikuwa picha ya Sebastiani, Ofisini ukamshangaa July naona bado haujatosheka unaendelea tena kumshangaa hadi uku, ona sasa hadi maji ya mdomoni yamekumwagikia kwenye suruali kama umejikojolea, hahahaa( kicheko chepesi cha kumfanya Paul arudishe uimara wake). July; ( akamsogelea Anna na kumnong’oneza sikioni) unataka sema huyu ndio Paul uliyeniambia jana kuwa kakukonyeza? Anna;( kwa ishara ya kichwa akajibu) ndio. Paul; hooo akuna kitu Anna uwa ninatabia ya kufananisha watu, samahani kwa ilo. Mambo Julieth, nimefurahi sana kukutana na wewe?( huku Julieth akionesha kutokuwa na kumbu kumbu na sura ya Paul). July; safi tu Paul, poleni na kazi pia ahsante sana kwa kunifundishia mdogo wangu kazi na pia kwa kumsaidia kurudisha simu yake toka kwa mwizi. Paul; usihofu huu wote ni wajibu wangu na kama sio, basi ni faraja kwangu kutimiza furaha ya watu wa karibu yangu,( akamgeukia Anna na kumwambia) you are welcome. Muda si mrefu kutoka mazungumzo yale, mambo ya TANESCO yakajiri na umeme ukakatika, giza likatanda na watu wakashindwa kuonana, bali sauti zikasikika tu zikiyoyoma. Anna; samahanini jamani naombeni mcheke niwaoneni, natembea kwenda kwenye kochi, mbele yangu kuna mtu au..?(kwa makusudi akamkanyaga Julieth). July; unanikanyaga huko, embu tazama mbele. Anna; nimekwambia ucheke nikuone ukakataa, kwani hujijui kuwa wewe ni mwafrika alisi? Pole, lakini siku nyingine cheka ili nisikukanyage tena.( masihara yakazidi endelea) Anna; embu sister July naomba unichukulie begi lagu jeusi hapo kweye kochi. July akasogea na kumshika Paul masikio huku akiyavuta juu. July; umeweka nini humu, mawe nini? Mbona zito sana. Paul; auuhuu ( sauti ya maumivu kutokana na kufinywa masikio). July; hooo samahani Paul kumbe wewe, nilidhani ni begi la Anna.( wakati july anamwachia Paul masikio, Paul akamshika July mkono wa kulia na kumvuta kwake). Nini tena Paul. Paul; mkanda wa begi umenasa mkononi, kwa kuwa ni zito ndio maana limekuzidi nguvu. Wote wakacheka na kuanza rushiana mito midogo ya kochi, muda wa dakika kama tano hivi, taa zikawaka na mngurumo wa genereta ukasikika. Anna na July; (kwa sauti kubwa) huo heeeeee. Paul; hahahaaaaaa (kicheko kikali kilimkamata na kuwafanya wote wacheke kwa pamoja). Mara mlango wa sebureni ukasikika ukigongwa, kicheko kilikatika ghafra na kisha mlinzi akaingia. Mlinzi; madam July, mafuta ya genereta yamebaki machache sana kama umeme usiporudi hayatufikishi saa nne.( Anna akadakia mazugumzo). Anna; sawa sawa hata mama aliniiachia maagizo kuwa tununue mafuta tangu wiki jana, na leo ni tafrija ndogo ya ukumbusho wa kuzaliwa kwake atopenda kuona umeme umekata. July; sawa itanibidi nikanunue kwa makoma. Mlinzi akaaga na kugeuka kuondoka, wakati yupo mlangoni Anna akaita kwa sauti ya juu. Anna; Mtayabarwa njoo mara moja.(lakini mlinzi hakugeuka). Paul; hoo we ni genius sana, naona sio yeye kama angekuwa yeye asingeshindwa kugeuka. Umesema July kuwa unaenda kwa makoma au ..? July; ndio. Paul; okay naona muda umeshaenda acha na mimi nikapumzike home, tuongozane mpaka Mwananyamala A nikachukue usafiri wa kwetu. July na Anna; kwenu au kwako? Na ni wapi?(kwapamoja). Paul; inaonekana mmezoeana sana hadi mazungumzo yenu yana fanana? July; haaaa tumeshazoea kuwakosoa watu wanaosema kwetu… kwetu…, kwa msemo uho. Paul; okay mi ndio natokea kwetu lakini sikai na wazazi wangu. Anna; ki vipi ukai nao? Na kwenu wapi? Paul; wameshatangulia mbele ya haki. Mi ninakaa Mabibo relini. Anna na July; pole sana. Paul; ahsante, lakini mi ni mkubwa sasa, haina haja ya kupewa pole. Anna na July walionekana kufuraishwa na ujio wa Paul na muda ukazidi sogea kwa mazungumzo ya hapa na pale, basi Paul na July wakatoka kwa safari ya gari la July hadi maeneo ya Mwananyamala A, na Paul akamuhaga July na kushuka, wakati Paul anatembea kuelekea kituoni, sauti ikasikika. July; PAUL! Paul akageuka kumtazama July, July akampungia Paul mkono wa kwaheri, Paul naye akarudisha ukarimu. Paul akasogea kituoni na kusubiri gari la Mabibo Makumbusho, alikaa muda mrefu kiasi bila ya kupata usafiri, mara akaona gari haina ya staret imepaki mbele yake. July; twende nitakuacha hapo mapipa itakuwa rahisi kupata gari la Mabibo. Paul; okay. Paul akapanda na story za masihara na uongo ulio kithiri ulitawara mzaa wao ndani ya gari hakika wote walifurahi na safari ikawa fupi mara wakafika maeneo ya Mgomeni Mapipa, Paul akashuka na July akamuhaga Paul kwa mara ya pili. July; jioni njema. Paul; ahsante nawe pia. July; karibu tena kwetu. Paul; kwenu au kwako( akirudia msemo wao JULY na ANNA, July alicheka kwa ishara ya msemo wake leo umemshika na yeye pia) July; pale kwetu bwana, bado sijabahatika kufika kwangu. Paul; okay ahsante tena. July akaendesha gari na kwenda kunuua mafuta sheri ya Magomeni Mapipa karibu na Travetein Hotel. Paul alimtazama kwa uzuni ya kumwaga July mpaka gari yake ilipoishia mbali na upeo wa macho yake( mithiri ya mbwa mdogo anavyosikitika kwa kuachwa na mfugaji wake anayempenda sana). Paul akafunga safari ya kwenda nyumbani na kumuadisia Samwel mambo yote yaliyojili siku hiyo mchana mpaka jioni kwa furaha kubwa, akaamua kufungua ubao wa upererezi wa mambo yampendezayo na kumvutia July. Paul akachukua kipande cha cheap board( maarufu kama silingi bodi) wenye kipimo cha meta 2 kwa meta 2 na kuushikiza vizuri sana kwenye ukuta wa chumbani kwake, kisha juu akaandika jina la JULIETH PETTER kwa kuremba maandishi ya kiarchitect. Paul; ( moyoni mwake) Julieth anapenda sana masihara na utani, mcheshi akiwa na watu alio wazoea bali ni mkimya mbele ya wageni, anazoea watu kwa urahisi, mkarimu na pia ni msahaulifu wa araka sana. Paul akasimama pembeni na kuutazama ule ubao wa upererezi kwa muda wa dakika kama kumi hivi, kisha akaendelea kujiandaa kwa kula na kulala. Usiku haukuwa mrefu bali ulikwa ni usiku mfupi kuliko usiku mwingine wowote Paul alioweza kumbuka maishani mwake, kwani haukuwai kujisikia furaha na mwepesi wa nafsi kiasi kile tangu na tangu maishani mwake. Usingizi ulipambwa na ndoto nyingi zenye matumaini mazuri ya siku za baadae kati yake na Julieth. Ndoto nyingine nzuri ilikatishwa na mlio wa aramu, Paul akaunyoosha mkono na kuizima aramu kisha akarudi kulala ili ndoto iendelee, lakini haikufanikiwa. Ikambidi anyanyuke na kujiandaa kama ilivyokuwa kawaida yake siku zote na kisha wakaenda kazini yeye na swahiba wake Samwel. Kazini napo palikuwa furaha tu kati yake na Anna, mpaka wengine wakashangaa, kazi zilienda vyema na kwa kasi nzuri, kwa ujumla ufanisi wa Paul na Anna ulikuwa wakushangaza. Hali iliendelea mpaka ndani ya wiki moja siku ya terehe 8th August, 2013 siku ya nane nane, Paul akiwa nyumbani akaingia facebook na kuchati na watu mbali mbali, akaona bora amtumie friend request ANNA MARY PETTER, basi akasogeza kasa mpaka kwenye add friend kisha akabofya na ishara ya friend request sent ilionekana, Paul akaingia kwenye kikundi cha SCEM na kuchati na raiki zake wengine wakati anaendelea kuchati akaona kuwa kunanotification moja, akaifungua na kuitazama. Paul; hooo Anna amekubari urafiki nami, ngoja nimtumie sms. Paul akaandika utamburisho mfupi kujitamburisha kuwa yeye ni Paul wa kazini kwake. Paul; (sms chatting) hey Paul supervisor wako field. Anna; (sms chatting) hahaaa nimeshakujua kabla. Wapi mida hii. Paul; (sms chatting) home kwetu nimetulia. Anna; (sms chatting) hahahaaa kwenu kwako…? Paul; (sms chatting) okay kwangu. Karibu uje kutusalimia. Anna; (sms chatting) ahsante Paul, tupo home na mama tunampango wa kutoka kama familia siku ya leo. Paul; (sms chatting) okay ni vyema, vipi July mzima? Anna; (sms chatting) ndio nipo nae hapa naye anachangia majibu. Paul; (sms chatting) mpe nafasi basi naye nichati naye. Anna; (sms chatting) sawa huyu hapa, chati naye. Paul; (sms chatting) mambo July July via Anna’s fb account; (sms chatting) safi za tangu wiki iliyopita? Paul; (sms chatting) fresh tu, vipi baadae ni pande zipi? July via Anna’s fb account; (sms chatting) paradise hotel ndani ya Bagamoyo, karibu tujumuike. Paul; (sms chatting) ningependa kuja lakini nimesikia ni kifamilia. July via Anna’s fb account; (sms chatting) ndio lakini haitozuia wewe na sisi kufurahia. Paul; (sms chatting) pouwa mtanikuta basi muda ukifika. July via Anna’s fb account; (sms chatting) poa itapendeza tukionana uko, husikose kijana. Paul; pouwa tutakutana binti. (chatting ikaendelea baiana ya Anna na Paul) huku Paul akiendelea kujiadaa na kufanya mtoko wa kwenda Bagamoyo maeneo hayo ya Paradise Hotel.
Posted on: Sat, 17 Aug 2013 17:20:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015