RIO ADAI WAGENI WANAZUIA MAFANIKIO TIMU YA TAIFA ENGLAND! Rio - TopicsExpress



          

RIO ADAI WAGENI WANAZUIA MAFANIKIO TIMU YA TAIFA ENGLAND! Rio Ferdinand anaamini kuwa kujazana kwa wachezaji wengi Wageni kwenye Ligi Kuu England kunatibua mafanikio ya baadae ya England. Akiongea mara tu baada ya Mwenyekiti mpya wa FA, Greg Dyke, kudai hali inatisha kwa jinsi Ligi Kuu England ilivyokuwa na Wachezaji wachache wa Kiingereza, Rio Ferdinand, ambae yeye alikulia kwenye timu za vijana za West Ham, alitamka: “Kuwa na wachezaji wachache wa Uingereza kwenye Ligi Kuu kunapunguza nafasi ya mafanikio. Ukiangalia ule mchezo ya Man City na Newcastle, kulikuwa na wachezaji watatu tu wa England kati ya 22 walioanza! Ni aibu hii!” Beki huyo wa Man United alitaka kuwepo udhibiti ingawa hilo ni gumu kwa mujibu wa Sheria za sasa lakini alitolea mfano wa Turkey ambako alidai kuwa Klabu zinaruhusiwa kuwa na si zaidi ya wachezaji 10 Wageni lakini siku ya mechi Kikosi rasmi cha Timu hakiruhusiwi kuwa na zaidi ya wachezaji 6 wa kigeni.
Posted on: Sun, 08 Sep 2013 18:56:45 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015