RIWAYA: HATIA MTUNZI: George Iron Mosenya SEHEMU YA ISHIRINI NA - TopicsExpress



          

RIWAYA: HATIA MTUNZI: George Iron Mosenya SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO Usiku huo aliupitisha akiwa na Adrian, tayari alikuwa amemdanganya John Mapulu kwa njia ya simu kuwa alikuwa ameenda kumsalimia dada yake maeneo fulani nje kidogo ya jiji. Utu wa Matha ukawa unashuka kwa kasi sana alijiona kama hana umuhimu tena. Mtoto wake aliyekuwa tumboni pekee ndiye aliyebakia kuwa na umuhimu mkubwa. Umuhimu wa mtoto wake ndio ulisababisha apitie matatizo hayo laiti kama angekuwa hana umuhimu angeweza kuwa ameitoa mimba hiyo na kubakia bila msongo wowote wa mawazo. Matha akawa amefanya mapenzi na wanaume wawili, tena katika tofauti ya masaa machache. Matha alijua Joram kishaonja asali atataka kuchonga mzinga. Wakati anarejea Buzuluga nyumbani kwake wazo la kutafuta muafaka likamjia wazo kuu likawa ni kuua. Matha akanuia kumpa onyo lisilokuwa na nafasi ya pili kijana Joram. Roho ya kuua ikamwingia!!! Teksi ilimshusha, akalipia na kuingia ndani ya chumba chake!! Akalala!!! **** Michael alikuwa katika matembezi yake ya hapa na pale nje ya nyumba ya John, alikisogelea kibanda kinachouza magazeti akaanza kupitia vichwa vya magazeti mbalimbali. Macho yake yakavutiwa na gazeti la Ijumaa wikienda. Kichwa cha habari kilimshawishi akatoa pesa na kununua gazeti lile. Akarejea ndani upesi kwenda kuisoma habari ile. Kwanza alishtushwa na picha iliyofanana na mama yake, baadaye haikuwa inafanana alikuwa ni yeye na habari ilikuwa inamuhusu Michael mwenyewe, habari kwamba alikuwa amewekwa msukule na alikuwa ametambuliwa na Mtume maarufu jijini Dar kwa jina la JK yaani Jacob Komanya. Machale yakamcheza Michael, mchezo mchafu wa kitoto!!!! Alisema Michael huku akilazimisha tabasamu. Tabia za ajabu ajabu zilikuwa zimemuathiri na maneno ya John yalikuwa yamemkaa akaamini kuwa huo ulikuwa ni mchezo wa kumtia hatiani kirahisi. Kwa kipindi kirefu sana, Michael akawa amekumbuka kifo cha mwanadada Joyce Kindo ambaye alifia nyumba ya kulala wageni!!! Sikamatwi kirahisi!!! Alimaliza kwa kusema kisha akalihifadhi lile gazeti kwa ajili ya kuwaonyesha akina John pia!!! Hakuwa na wasiwasi!!! ******* Mariana alirejea nyumbani akiwa na matumaini tele aliamini kuwa hatimaye alikuwa amepata suluhisho sahihi la kumrejesha mwanaye katika mikono yake. Hakumshirikisha mtu yeyote kama alivyoshauriwa na mchungaji JK baada ya maombi. Alibaki kimya akiisubiri hiyo siku ya miadi iweze kufika aonane na mchungaji kwa ajili ya maombi mazito. Kila mara alimuombea afya mtumishi huyo wa Mungu asiweze kukumbwa na lolote baya. Siku ya kwanza ikapita hatimaye siku ya siku ikafika!! Mariana akajiandaa na kumuaga mume wake kuwa anaenda kwa mama yake mdogo, mzee Keto hakupinga lolote alimuamini sana mke wake akampa ruhusa. Mariana akaelekea nyumbani kwa Mchungaji Jacob Komanya. Mariana alipishana na msichana rika la Joyce ambaye ni mwanae akitokea nyumbani kwa mchungaji majira ya saa moja na nusu. Yaani nusu saa kabla ya muda aliokuwa ameahidiwa na mchungaji kuwa wakutane. “Bwana asifiwe…mchungaji yupo!!” Mariana alimsalimia na kuuliza. Yule binti alimkazia jicho la wasiwasi kisha akamuuliza, “Una shida naye??” “Ndio nina miadi naye!!” alijibu “Mh!! Haya yupo wala hakuna mtu zaidi ya mlinzi mlangoni…kaombewe” alijibu kwa sanifu kisha akaondoka. “Mh!! Atakuwa na mashetani huyu!!! Haleluya bwana niepushe na roho hawa wachafu!!” alikemea mwanamke huyu aliyekuwa amevaa nguo sawa kabisa na wanawake wa nchini Nigeria. Taratibu akagonga geti na kufunguliwa mlango, mlinzi alikuwa bado anamkumbuka hivyo hakumuwekea kipingamizi. Haraka haraka akatembea na kuufikia mlango, akaugonga akatokea mchungaji akamfungulia. “Oooh!! Glory be to God, Mariana ni wewe!!! Bwana apewe sifa” “Ni mimi ameeen!!!” alijibu Mariana. Uso wa mchungaji haukuwa na furaha ya kweli na alikuwa na wasiwasi. Mariana hakujua kuwa binti aliyepishana naye nje ya geti alikuwa ametoka kulazimishwa kufanya mapenzi na mchungaji Komanya. Lakini mashetani yake yaliwazidi ujanja mashetani wa Mchungaji hivyo hakufanikiwa. Jacob Komanya, alikuwa katika mtihani mkubwa sana kwani kwa siku hiyo alikuwa amefanikiwa kuzini na msichana mmoja pekee jambo ambalo lilikuwa kinyume na masharti aliyopewa nchini Nigeria wakati akiwa masomoni. Mariana hakuwa na kiburi cha kumuuliza lolote JK, aliingia ndani. Akakaribishwa kinywaji akaachwa peke yake sebuleni. Baada ya muda mrefu kidogo mchungaji alirejea alikuwa amevaa suti nyeupe iliyoukamata mwili wake vizuri. Mguuni alikuwa amevalia kiatu cheupe aina ya ‘four angle’, kifuani alikuwa na cheni nzito iliyotengenezwa kwa madini ya dhahabu, ndevu zake zilizochongwa katika mfumo wa herufi O zilimfanya apendeze sana, Mariana alikiri unadhifu huo kimya kimya. “Tunaweza kwenda Mariana!!” JK alizungumza Mariana akasimama na kumfuata. JK hakumuaga mlinzi zaidi ya kuwasha gari na mlinzi kufungua geti. Ndani ya gari la kifahari aina ya Hummer, Komanya alikuwa anaendesha mwenyewe, Mariana alikuwa kushoto kwake ametulia tuli huku akijaribu kupitia maandiko hapa na pale. Tayari ilikuwa saa tatu usiku!!! Gari lilikuwa katika mwendo wa kawaida kutokana na foleni za hapa na pale lakini baada ya kuiacha Mbezi mwisho, mwendo uliongezeka kidogo hadi liliposimama maeneo ya Kibaha. Mchungaji alichukua kichupa kidogo kilichokuwa kimehifadhi utuli, akajipulizia kidogo kisha akatabasamu, Mariana naye akajibu kwa tabasamu lakini hilo lilikuwa tabasamu la mwisho kabla ya pepo la ngono halijampanda mama huyu, alijikuta anarembua macho yake, aibu zilikuwa mbali naye, alijisogeza karibu na mchungaji. “Jacob nahisi baridi!!!” alisema kimahaba, JK akatabasamu na kuifanya ile staili yake ya kunyoa ndevu kuonekana vizuri!! Hakujibu kitu badala yake aliwasha gari na kuendesha umbali mfupi. Akalifikia bango dogo lililoandikwa Kibaha Yetu Lodge, akakata kulia na kukanyaga mafuta tena akawa ameifikia nyumba hiyo ya kulala wageni. “Karibu baba!!!” alipokelewa kwa shangwe. “Nilipiga simu, mmepewa maelekezo tayari!!!” aliuliza. “Ndio chumba namba 18 kipo tayari!!!” alijibiwa na msichana aliyekuwa muhudumu wa pale. “Naona upo na mama mchungaji!!!” alitania yule binti!! JK akacheka kwa staha, Mariana akajisogeza karibu yake akamshika kiuno wakaelekea chumba walichoelekezwa. Haikuwa mara ya kwanza kwa mchungaji huyu kufika eneo hili!!! Bila kujitambua Mariana akazini na mchungaji, bila shaka hiyo ndio ilikuwa sala ya kumuombea Joyce Keto huko alipo aweze kurudi. Fahamu zilimrudia Mariana wakati wakiwa wamemaliza kufanya tendo, alimkasirikia sana mchungaji lakini JK hakuzungumza kitu zaidi ya kumwambia. “Nenda ukatangaze na ndoa yako ivunjike!!!” maneno hayo yalikuwa kama kisu kikali kwa Mariana, yalipenya kama ubaridi na kisha uchungu ukalipuka akaanza kulia, mchungaji akacheka kwa sauti ya juu kidogo huku akivaa nguo zake. Kicheko hicho kikawa shambulizi baya kwa Mariana akajiona amebakwa katika mazingira ya ajabu tena uzeeni. Akaondoka haraka haraka pale chumbani akiwa na akili ya kurejea jijini Dar es salaam. Alipofika barabarani akagundua kuwa hakuwa na nauli, mwenyeji wake alikuwa ni Jacob Komanya peke yake eneo lile. Mariana hakuwa na namna nyingine akarejea kwa aibu kubwa sana akakutana na JK anatoka mapokezi kukabidhi chumba. “Ulitaka kurejea Dar kwa miguu” aliuliza kwa dharau kuu JK, Mariana akapatwa na kigugumizi cha kujibu. Jacob Komanya akatoa pochi yake ya rangi nyekundu na nyeupe akachomoa noti sita zenye rangi nyekundu. Akawa amempatia Mariana shilingi elfu sitini za kitanzania. “Nahitaji elfu mbili tu!!” alileta jeuri Mariana huku akishindwa kumkazia macho mchungaji!!! “Na hiyo ya kutoa mimba atakupatia mume wako??” Jacob aliuliza swali lililomshtua Mariana, akawa amezidiwa ujanja alitamani kupiga kelele lakini hakuwa na ushahidi wa kumwezesha kufanya hivyo. Akasonya kwa hasira na kisha akajiondokea!!! Huku nyuma JK akacheka kidogo halafu akasikika akisema, “Naenda hapo Mlandizi kwenye maombi!! Twende wote basi!!!” Mariana hakugeuka!!! Mariana hakuweza kurudi nyumbani kwake kwani alikuwa amemuaga mume wake kuwa atachelewa sana kurejea hivyo aliamua kuchukua chumba katika nyumba za kulala wageni. Hakuwa na hamu ya chakula alilala hivyohivyo!!! Saa nne kamili asubuhi alifika nyumbani kwake, hakukuta watu zaidi ya mfanyakazi wa ndani alisalimiwa lakini hakujibu salamu hiyo, akaingia mpaka chumbani akajifungia. Punde tu baada ya kuufunga mlango, alianza kuisikia nafsi yake ikitamka neno HATIA, akajiuliza lina maana gani kwa wakati huo, macho yake yakatua katika mkono wake, akakutana na pete ya ndoa, kumbukumbu ya usaliti ikamchukua na kumlegeza akakaa kitandani bado alikuwa anaiangalia pete ile. Picha ya Mchungaji JK akiwa anatabasamu ikajijenga mbele yake, Mariana akauma meno kwa uchungu, kisha akazivuruga nywele zake, uchungu ukapita kipimo. Akapatwa na hasira kali chuki nayo haikubaki nyuma lakini hatia ya usaliti ndio ilitawala kichwa chake. Mzee Keto na upendo wake atanielewaje?? Alijiuliza Mariana, mara bila kutegemea, ule uasili wa kabila lake uasili usioaminiwa na watu wengi lakini ni uasili wa asili, uasili wa kurithi kutoka kwa chifu Mkwawa, ‘kuliko kudhalilika heri kufa!!!’, Mariana akajikuta akiwaza kujiua tena kwa kujinyonga. Maneno machache yalichafua karatasi, kanga yake ilimtosha kabisa muhehe huyu, Mariana akajinyonga chumbani mwake!!! Hasira, mfadhaiko na uasili ukawa umemuua Mariana. Hatia yake ilikuwa nzito kujibu kuliko kuikwepa. Mariana kitanzini akapanda na hatia yake. ***** Kundi dogo la vijana lilikuwa limemzunguka kijana mwenzao ambaye alionekana kuwa katika hali tofauti kidogo ya maisha, walikuwa wanakunywa pombe huku wakilikubali kila jambo ambalo alikuwa akilisema kijana huyu. Alikuwa amevaa nguo zilizoonekana kuwa mpya lakini kwake hazikumkaa vyema, tumbo lake liliinyanyua shati yake na kuifanya kuwa fupi jambo ambalo liliruhusu mgongo wake kuonekana. Nywele zake zilizotoka kunyolewa siku kadhaa nyuma zilikuwa zinameremeta. Alikuwa anatoa noti kadhaa na kumlipa muhudumu, vijana wenzake walinyanyua glasi zao juu na kuzigonganisha ishara ya kumsifia, hakuna ambaye alikuwa amelewa. Mfukoni alikuwa na shilingi laki moja na nusu, elfu hamsini pungufu ya pesa alizokuwa amekuja nazo eneo lile la Villa Park akiwa ametokea nyumba ya kulala wageni aliyokuwa amehamia. Huyu alikuwa ni Defao akiwa ameisahau familia yake, akiwa amemsahau hadi Minja aliyekuwa amempa dili hilo. Defao alikuwa anaijaribu ladha tamu ya pesa, hakika ilikuwa tamu sana na ni ladha hiyo ambayo ilimuweka jijini Mwanza kwa siku kadhaa mbele. Heshima yake katika eneo la Villa Park ilikuwa juu sana, siku hiyo hiyo alipata mpenzi, akaondoka na kwenda kulala naye katika chumba alichokuwa amefikia. Ladha hiyo ya umaarufu ikamsahaulisha mengi akaisahau hatia yake ya kumdhulumu Minja mgao wake, pia hatia ya kuitelekeza familia yake ilikuwa imeenda likizo hakumkumbuka mgonjwa aliyekuwa mahututi. Defao alipachikwa jina la Papaa Defao na wanamuziki wa bendi baada ya kuwa amewatunza mara kwa mara katika nyimbo zao. Sifa zikaongezeka akapata wapambe. Kila penye wengi kuna jambo!!! Na hakuna rafiki mbaya kama rafiki anayepatikana wakati mtu ana pesa. **** Alidamka asubuhi akajikwatua na vipodozi mbalimbali akiwa mbele ya ‘dressing table’, akajigeuza huku na huko akauthaminisha urembo wake, akatabasamu. Alikuwa amependeza!!! Honi iliyopigwa ndio ilimkurupua kutoka pale na kuchukua mkoba wake mbio mbio akaanza kwenda nje, alipoifikia gari aliifuata ‘side mirror’ ya upande wa kulia mwa gari akautazama uso wake ambao ametoka kuuangalia sekunde chache mbele ya kioo kikubwa. “Mh!! Wasichana mna mambo?? Sasa huko ndani hujakiona kioo au” alizungumza kwa utani mwanaume huyu huku akiungurumisha injini ya gari yake, msichana huyu akajibu kwa kucheka huku akiweka sawa papi za mdomo wake kwa kuziumauma. Baada ya hapo mwanaume huyu aliyekuwa amejiwekea hifadhi yake ndani ya suti nyeusi iliyokuwa ya hadhi ya juu alimfungulia mlango binti akajitosa ndani ya gari na kuubamiza mlango ukawa umejifunga. Kabla yule binti hajafika marashi ya yule mwanaume yalitawala ndani ya gari lakini kufika kwa yule binti kulivunja utawala wake, utuli wa yule binti ukachukua nafasi. Geti likafunguliwa John Mapulu akawasha gari, ilikuwa ni safari ya kumpeleka Joyce Keto kliniki ambayo aliamua amuandikishe hospitali ya Agha Khan ya jijini Mwanza kwani huduma zake zilikuwa nzuri sana tofauti na hospitali za serikali. Zoezi hilo liliwachukua muda wa nusu saa baada ya kufika. Joyce akapewa ratiba ya kuwa anahudhuria kliniki. John akaahidi kuwa anamleta kila siku iliyopo kwenye ratiba. Joyce akashukuru wakarejea nyumbani. Wazo la Joyce kuwatafuta ndugu zake halikuwepo hata kwa mbali, sumu aliyokuwa amepandikiziwa na John ilikuwa imeathiri akili yake na kujihisi hapo alipo ndio mikono salama zaidi na si kwingine. “Mh!! Mhehe ajiua, hawa nao kwa kutuandama!!!” alisema Joyce wakati huo gari ipo kwenye foleni, baada ya muuza magazeti kupitisha katika dirisha lililokuwa upande wake. “Hah!! Kumbe muhehe wewe mh!!” aliuliza John, Joyce hakujibu!!! Alitoa noti ya shilingi elfu tano, muuza magazeti hakuwa na chenji hiyo, na John naye hakuwa na pesa ndogo, mataa yakawa yameruhusu gari likaondoka. Joyce hakufanikiwa kununua gazeti lile, alitegemea atanunua mbele ya safari, akasahau hadi wakafika nyumbani. John akamuaga Joyce wakaahidiana kuonana jioni!! Laiti kama angefanikiwa kuisoma habari iliyokuwa kwenye gazeti basi angetambua kifo cha mama yake mzazi katika harakati za kumwokoa. **** Penzi alilopewa Adrian na Matha kwa mara ya pili lilikuwa bora kuliko lile la kwanza alisahau kabisa suala la ndoa yake na Monica, akawa ameamua kujizatiti kwa mpenzi wake huyu wa zamani hizo. Na ili ampate ilikuwa lazima na yeye amdhulumu John Mapulu. Atamdhulumu vipi?? Hilo ndio lilikuwa swali gumu. Nina pesa!!! Pesa ndio kila kitu!!! Nitamrejesha Matha kwangu. Alipata muafaka Adrian. Wakati huo alikuwa amerejea nyumbani kwake baada ya polisi kuwa wamekamilisha upelelezi wao dhaifu kama kawaida na siku hiyo hakuwa ameenda kazini kwani msaidizi alikuwa ametangulia tayari. Hatia ya kumsababishia Monica kubakwa ilikuwa imesahaulika, sasa alikuwa anaingia katika jaribio la kurejesha kile kilicho bora kwake. Adrian akafikiria kutumia pesa aliyokuwanayo kumpa John onyo, kumpa maumivu makali kama ambayo aliyapata yeye baada ya John kumpokonya tonge mdomoni. Hasira ikamsababishia kukihesabu alichotaka kukifanya kuwa kisasi halali. Akanyanyua simu yake akapiga namba fulani simu ikapokelewa. “Za siku kaka!!!” “Poa ndugu yangu, nina shida kidogo” “Nini tena??” “Namuhitaji Nunda” “Kuna mshenzi gani amekusumbua??” “Yupo mpuuzi nahitaji kumpa somo!!!” “Tuonane mchana dukani kwako” Adrian alikubali na kukata simu, akasimama na kuongoza mwili wake bafuni, akaoga kisha akajiandaa akaelekea Makoroboi kwa usafiri wa daladala. Mida ya mchana akafika rafiki yake wa shule ya msingi aliyeitwa Mark ambaye aliacha shule kitambo na kujiingiza katika vitendo vya kihuni. Alikuwa ameambatana na mwenzake. Adrian alitoa maelekezo yote, akaeleweka, kisha akawatajia jina la muhusika kuwa ni John Mapulu. “Nahitaji apigwe na apewe onyo la kuachana na mke wake!!” “Laki tano unusu!!” alitaja bei Adrian akakubaliana nayo akatanguliza nusu. Akawa ameingia rasmi katika vita ya kumgombea Matha!!!! Msichana aliyeamini kuwa aliumbwa kwa ajili yake. **** ADRIAN ameamua kuingia rasmi katika vita ya kumgombea Matha..... DEFAO amenogewa jijini Mwanza.... ITAENDELEA KESHO SAA SITA MCHANA!!!!
Posted on: Mon, 26 Aug 2013 09:00:00 +0000

Trending Topics



BUSINESS PACKAGE worth
Lytecaster Steep Slope Reflector Trim 30-45 Degrees Finish: Gloss
MAJI = Majority Agency for Joint Intelligence All information,
#12161 - Trucks are probably the worst functioning automobile and
FYI I should be writing assignments right now, but whats the fun
Анекдоты о переводах и
- Tattoo Week Rio A Maior Convenção de Tattoo e Piercing do
☼ Good Afternoon Hello Everybody Has Been an Awesome Day. A
=>এই জান শুনো আমার না একটা
LASER PHYSICS AND TECHNOLOGY #9 - FIBER FABRICATION There is a

Recently Viewed Topics




© 2015