RIWAYA :NANI ANIFUTE MACHOZI? MTUNZI :CHARLES J LIGONJA SEHEMU - TopicsExpress



          

RIWAYA :NANI ANIFUTE MACHOZI? MTUNZI :CHARLES J LIGONJA SEHEMU YA TISA 0714 79 77 78 Walikaa chini wasijue wapi pa kuanzia kwani pesa ambayo wanadaiwa na benki ni zaidi ya milioni mia tano za kiTanzania,na wiki mbili zilizopita walisababisha ajali kwenye moja ya ghala na moto kulipuka hivyo kulazimika kulipa milioni mia saba,ghala lilikuwa na mazao ya wakulima zaidi na mia mbili. FRANK SAFARINI Baada ya kupanda basi saa kumi na mbili asubuhi pale Ubungo,Frank aliweka begi lake sehemu maalum na safari ilianza saa kumi na mbili na dakika kama mbili hivi,hali ya hewa ilikuwa tulivu kwani joto lilikuwepo la wastani na ubaridi pia,kila mtu alikuwa na mambo yake huyu kashika simu na kuongea na ndugu zake akimtaka ampokee akifika na mengineyo mengi lakini kuna wale wanaoongopeana. ‘Yani nishakumiss dear’ kazi kweli kweli ndio kwanza umeliacha geti kuu la kutokea mabasi pale Ubungo eti umemmiss mwenza wako kama sio uongo nini basi.Lakini kuna wale ambao hutama meseji tangu mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari eti akimtumia sana meseji sio rahisi kumsaliti,nani kasema!Unakuta mtu ana betri mbili za simu ili moja ikiisha basi anaweka nyingine ili aweze kusoma hadithi ya CHARLES LIGONJA aliyoiweka facebook,safi kwani safari huwa fupi sana kama unakuwa na kitabu au hadithi nzuri ikikuliwaza kichwani. Frank alikuwa kimya sana, muda mwingi alikuwa akiutumia kusoma hadithi matatani iliyokuwa kwenye ukurasa wa Charles Ligonja aliyoipa jina la “KWANINI UTAKE KUJIUA” na mengi ambayo alikuwa akiyasoma kwenye hiyo hadithi yalikuwa yanamgusa na kila mstari aliokuwa akiusoma alitaka kuendelea na mwingine ili tu ajue huyo Belinda anaetamani kujiua amekutwa na nini mpaka aamue kujitoa uhai. ‘ITAENDELEA….Ayaaaaaa Charles vipi unakanyaga waya’ Frank alijikuta akiongea kwa sauti mpaka majirani zake pembeni na hata nyuma ya siti kumsikia. ‘Vipi kaka Charles ndio nani na huo waya upi tena?’ ‘Kuna kijana mmoja nasoma hadithi yake hapa facebook sasa haijaisha na alipofikia patamu kweli duh’ ‘Ebu basi nione jamani kwani natuma meseji kwa mpenzi wangu but mtu mwenyewe hanijibu sijui nd’o busy!’ Frank bila hiyana alimpa simu jirani yake na kuanza kuisoma. ‘Kuna watu wanayafanya hayo kweli hapa chini ya jua?’ ‘Inawezekana, we acha tu kama una mume basi omba Mungu asikutende’ ‘Oya jamani jirani ni nani huyo anaandika hadithi huko nami nisome?’ ‘Charles Ligonja,ingia facebook na kurequest utaona vitu vyake’ ‘Wapuuzi tu hao yani kutwa wako facebook kuandika wazimu, siwezi poteza muda wangu huko,facebook wazimu mtupu’ ‘Hizo dharau sasa,kama hauko huko basi sisi tulioko naomba utuache,kuna vijana wanaandika vitu vizuri na vya kujenga,kaa hivyo hivyo’ Fank alionesha kukerwa na kauli ya mmoja wa abiria ambae aliongea kwa dharau kitu ambacho abiria wengi hawakukipenda kwani kuna watu walioko kule na wanapata pesa ingawa kuna wengine wako busy kutongozana na kuweka picha za uchi,hao ni wapumbavu tu wasiojua nini maana ya mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ikiwemo facebook kuna kurasa nyingi ambazo zinatoa mafunzo mbalimbali kama ufugaji wa kuku wa kisasa na kienyeji,ufugaji wa samaki na hata namna bora ya kula na kufanya mazoezi na hiyo ndiyo hasa Facebook bwana lakini kwa hao wanaoandika hadithi na kuweka kule kuna kitu wanalenga kuna wengine ambao wameanza kufanya ebook,soma hadithi ukiipenda basi unamchangia mwandishi kwa kumtumia pesa kidogo na yeye anakutumia hadithi yote online,kwa nchi nyingi zilizoendelea wamefanya na wanaendelea kufanya hivyo,kwa kufanya hivyo kuna kijana mmoja tayari kapata ajira kupitia huko huko na leo hii yuko Marekani anasomea namna ya kuandika script za filamu.Hayo ndio hasa matumizi bora ya facebook. Watu wote ndani ya lile basi walikuwa kimya wakimsikiliza Frank na mwisho wa siku kati ya abiria hamsini na tisa waliokuwa kwenye lile basi kumi na tisa tu hawakuwa na simu zenye uwezo wa internet lakini arobaini waliobaki walijiunga na facebook na wale ambao walikuwa tayari na account waliingia moja kwa moja na kuanza kusoma hadithi za kijana anayechipukia kwenye ulimwengu wa hadithi si mwingine ni Charles Ligonja.Basi lilitulia kila mtu alikuwa busy na simu yake akisoma mambo mbalimbali kwani mbali na hadithi kuna vitu vingine vingi ambavyo vilikuwa kwenye ukurasa wake na kufanya watu wasome na kufurahi. ‘Konda vipi watu wamelala mbona kimya sana?’ Dereva alihoji baada ya kutembea zaidi ya kilometa mia mbili ndani ya gari kukiwa kimya, madirisha yalikuwa yamefungwa hivyo kutosikia hata upepo ukiingia. ‘Wako macho,wamelogwa na facebook!’ ‘Hahahahahaha amewabamba kweli mwenye hizo hadithi haya ngoja nipige gia’ Safari iliendelea vizuri na ilipofika saa tano usiku basi lilikuwa nyegezo jijini Mwanza na abiria kuanza kushuka, siku hiyo Charles alipokea simu nyingi sana na kulazimika kuweka vipande vingine vitatu kwa siku hiyo hiyo ili wasomaji wake waendelee kupata burudani na kujifunza kitu fulani.Baada ya nusu saa kila mmoja aliingia kwake. Frank alikumbuka mengi sana , alitamani muda urudi nyuma awe karibu n nyumbani kwake na kwenda kumuona mtoto wake Wit ambae kwa kipindi hicho ilishapita miaka kumi tangu Witness afariki dunia,aljikuta akimkumbuka Patty baada ya kuona baadhi ya maeneo waliyokuwa wakikaa pamoja enzi za mapnzi yao na kunywa hata soda au juisi,alimkumbuka pia Alex ambae alikuwa akimsaidia kazi zake nyingi bila kujua ni mume mwenzake,wote siri yao ya utundu kitandani anaijua Patricia lakini hilo kwa Patty na Alex halikuwa tatizo kwani walikuwa na sababu maalum. ‘Frank!’ ‘Mwajuma upo?’ ‘Pole sana, umetoka lini?’ ‘Kama miaka miwili sasa, nambie bosi yupo?’ ‘Hatoamini,pita bosi yupo ndani’ Frank aliingia ndani na kukutana na bwana Bill Klerk ambae ndio bosi wa kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi hapo mwanzo,walikumbatiana kwa muda baada ya salamu. ‘Your wife is very stupid’ Frank anakutana na maneno makali yanayoelekezwa kwake kupitia yeye,Klerk alikuwa hajui lolote kuhusu ndoa ya Frank na Patty. ‘Kwanini bosi?’ Ni kweli Klerk ana haki ya kumuona Patty mpumbavu kwani mara baada ya Frank kukutwa na kesi alienda ili ajue namna gani ya kumsaidia ikiwemo kutafuta wakili na hilo lilitokana na mchango mkubwa wa Frank katika kampuni yake,kumkosa Frank ilikuwa pigo kubwa lakini cha kushangaza anafika pale hakupewa ushirikiano toka kwa Patty na kuamua kuondoka asijue wapi pa kwenda. ‘Mke wangu mpaka muda huu sijui yuko wapi,tuyaache hayo bosi kwani sitaki kukumbuka yaliyopita’ ‘Ukitaka kuanza kazi hata leo mlango uko wazi?’ ‘Sitaki kutoa jibu la moja kwa moja, nipe muda” ‘Hakuna tatizi ndugu yangu, karibu sana’ Frank alipokelewa vizuri sana na muda mfupi badae kengele ilipigwa na wafanyakazi wote kukusanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliokuwa ardhini na kuketi kusubiri dhumuni la wito. ‘Sijui kuna nini leo au kimeota?’ ‘Acha uoga Yasinta,kama kimeota unalamba mafao yako na kwenda kujikita kwenye kilimo,utafanya kazi wapi maika mitano upate milioni arobaini kama mafao?’ ‘Umeanza mwanasiasa,utataja walimu sasa hivi?’ ‘Kweli kabisa mwalimu anafundisha miaka thelathini lakini ukiangalia mafao yake eti milioni ishirini na tano au thelathini,jamaa wanaonewa wale’ ‘SURPRISEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!’Kwa mara ya kwanza bosi alitokeza hadharani na kukenua meno mpaka jino la mwisho na kumtambulisha Frank.Kila mtu alifurahi kumuona Frank eneo lile na wengi walionekana kutoamini kama aliyesimama mbele yao Frank au mwingine,siku hiyo kwa mara ya kwanza kazi zilisimama na kuandaliwa bonge ya sherehe kwa ajili ya Frank.Frank hakuamini kama angepata mapokezi makubwa namna ile aliamini kuishi vizuri na watu ndio hasa chachu ya yeye kupokelewa vizuri. ***KUMBUKA UKIWA SEHEMU YAKO YA KAZI HAKIKISHA UNAHESHIMU WOTE UNAOFANYA NAO KAZI HAIJALISHI NAFASI ULIYONAYO*** JE NINI KITATOKEA?
Posted on: Mon, 02 Sep 2013 07:28:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015