Rafiki zangu wa facebook, hasa wana Iringa, kwa mwezi wote huu wa - TopicsExpress



          

Rafiki zangu wa facebook, hasa wana Iringa, kwa mwezi wote huu wa Agosti 2103, GO Consulting tumeingia mkataba na radio Country FM ya Iringa, kudhamini kipindi cha Dira ya Vijana, na mimi Perecy Ugula nitashiriki kuandaa mada za kujadili kila Jumamosi kipindi kinapoanza saa 1:30 asbh hadi saa 3:00 asbh. Baada ya kutafakari sana na kujadiliana na waendesha kipindi cha Dira ya Vijana wa radio Country FM tumeona malengo ya kipindi ni mazuri, lakini ni namna gani radio Country wanapata feedback (mrejesho) wa mabadiliko chanya ya vijana kuhusu mambo wanayoyajadili katika kipindi husika? Kimsingi haiko wazi, na hakuna mtu amehangaika kufuatilia hilo. Kwa kuwa GO Consulting tumepata fursa hii, tumewaza kufanya hatua ya mbele kwa vijana wa Iringa kupitia kipindi hiki. Kuanzia Jumamosi hii ya tarehe 10/8/2013, nitashiriki katika kipindi hiki, tukijadili kwa mapana dhana ya DIRA YA VIJANA kwa mtazamo wa namna Umoja wa Mataifa na Sera ya Maendeleo ya Vijana ya Tanzania inavyoangalia vipaumbele katika mambo ya vijana; ikiwa ni siku ambayo nitafungua na kukaribisha vijana na wadau wa maendeleo ya vijana kuiunga mkono GO Consulting katika kile ambacho tutakiita: JUKWAA LA DIRA YA VIJANA IRINGA- JDVI(FORUM FOR YOUTH VISION IN IRINGA, FYVI) Lengo kuu la FYVI itakuwa kuwaleta vijana wa Iringa pamoja katika kujadili changamoto zinazowahusu vijana katika maeneo 10 ya vipaumbele vya UN na Tanzania kuhusu vijana; kuandaa program nzuri za maendeleo ya vijana na kuwashirikisha vijana kuzitekeleza program husika kwa matokeo chanya.
Posted on: Thu, 08 Aug 2013 10:06:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015