Raia wa Tanzania akamatwa na dawa za kulevya nchini Thailand, - TopicsExpress



          

Raia wa Tanzania akamatwa na dawa za kulevya nchini Thailand, alikamatwa Jumanne wiki iliyopita katika kisiwa cha Macau akiwa amemeza dawa hizo aina ya cocaine akielekea China. Dawa hizo zinakadiriwa kufikia kilogram 1.091, zikiwa na thamani ya dola za HongKong 900,000. Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, alipokuwa ziarani nchini alitiliana saini na serikali ya Tanzania kubadilishana wafungwa, mkataba huo utasaidia kwa watanzania wote waliyofungwa nchini Thailand, kutumia vifungo vyao nchini Tanzania. Wakati huko Thailand hali ikiwa hivyo, watanzania wawili waliyokamatwa na Madawa ya kulevya miezi miwili iliyopita nchini Misri, haijulikani watu hao wapo katika hali gani baada ya kuwa na tetesi za kunyongwa na baadae kukatika upatikanaji wa taarifa zao.
Posted on: Tue, 06 Aug 2013 09:58:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015