Relationship hazina adabu, ziko kama Bodaboda, ajali muda wowote - TopicsExpress



          

Relationship hazina adabu, ziko kama Bodaboda, ajali muda wowote tu. Usiachane na mpenzi wako wa sasa kwa mbwembwe kisa umepata Kipusa kipya unamwaga shombo na kashfa debe tano, Kisa umepata buzi jipya basi hatuhemi, unabreak up kwa kiherehere, nyodo na kisebusebu utadhani huyo mpenzi uliyempata Mwili wake umetengenezwa na Eat Some More Biscuits kwamba ukimbusu anatoa maziwa fresh au jasho lake linanukia juice ya Aloe Vera..... Hakuna jipya,ni mihemko tu ya kipya kinyemi, hana tofauti yoyote ni binadamu tu tena anaweza kuwa kimeo zaidi ya uliyemuacha. Ukishindwana na mtu muachane kwa amani, huwezijua utamkuta wapi akiwa nani na kwenye position gani... We endelea tu kubreak kwa matusi na kashfa na kuita watu Tumbili pori uje ukutane nae kwenye Interview ndo utajua kama kuna Tumbili ni HR Manager ana ofisi na hana mkia, sura itakushuka kama Pilipili Hoho iliyopauka. Aafu xaxa na huko unapopaona pazuri ukaachike xaxa ndo utaona mapenzi matamu, na ukitaaka kufoji maisha tutakukuta meeda pale unauza kudadex!
Posted on: Mon, 26 Aug 2013 06:56:15 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015