Rubani mmoja na mwanafunzi wa urubani wameangamia mapema leo baada - TopicsExpress



          

Rubani mmoja na mwanafunzi wa urubani wameangamia mapema leo baada ya ndege walimokuwa kuanguka na kuteketea ilipokuwa inatoka katika uwanja wa ndege wa Wilson.Inaarifiwa ndege hiyo ya shule moja ya urubani humu nchini aina ya Cessna 172 ilikuwa inatoka katika uwanja huo mwendo wa saa nne unusu kabla kuanguka na kushika moto.Wawili hao walichomeka hadi kufariki katika mkasa huo na ambao chanzo chake bado hakijajulikana.Afisa mkuu katika uwanja huo Joseph Ole Tito amesema wataalamu wa ndege wamefika kwenye uwanja huo kuchunguzi kilichosababisha ajali.Mwaka jana serikali ya kenya iliwaondoa kwa lazima wakaaji wa mtaa wa mabanda uliokuwa karibu kwa hofu kuwa huenda wakaathirika na ajali kama hizo. ………………….Taarifa yake Dauglas Omariba…………………
Posted on: Wed, 09 Oct 2013 11:39:46 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015