SHAIRI: CHURA NAMBA 20 MALENGA: GAMA Ibrahim SEHEMU YA KUMI NA - TopicsExpress



          

SHAIRI: CHURA NAMBA 20 MALENGA: GAMA Ibrahim SEHEMU YA KUMI NA MBILI 189 .”Sitochukuwa chochote, Nawe usinitafute, Tukikutana popote, Ruksa kunisalimia.” 190.”Ufunguo wa akiba, Ambao niliubeba, Nawacha kwenye bawaba, Ya karibu na mauwa.” 191. “Kaa na mtoto wako, Mimi sina mana kwako, Ninakwenda niendako, Ambapo nitaenziwa.” 192. “Nakuachia nafasi, Usiwe na wasiwasi, Ukitaka na harusi, Sina neno funga ndoa!” 193. “Kwa heri yakuonana, Pindi mwaka takutana, Naiepuka fitina, Isije ikaniuwa!” 194. Harufu yanigutua, Ya chungu kinoungua, Khalfani namtua, Jikoni nakimbilia. 195. Sasa ndiyo natambua, Kwamba naanza ugua, Chungu nilokiepua, Sina nilichokitia! 196. Si maji wala si unga, Vyote hivyo sikutenga, Hakika nimeboronga, Akili inasinzia! 197. Kwa nyingine sufuria, Na vitu vilotimia, Napika nimetulia, Hatimae naipua. 198. Naupoza namnywesha, Akanywa akabakisha, Nae ninamuogesha, Uji umemchafua! 199. Ninakwenda madukani, Na khalfani garini, Za bei ya wastani, Nguo namnunulia. 200.Ninaenda kituoni, Magomeni wilayani, Ninaegesha mwishoni, Nashuka kusalimia. 201. Mara kaja abiria, Gari yangu kaingia, Nami namkimbilia, “Wapi?” Namuulizia! 202. “Nipeleke Kiwalani, Mkabala na shuleni, Waenda kiasi gani, Usije kunilangua?” 203. “Hatuwezi kukosana, Sina bei kubwa sana, Wewe nipe tu bwana, Pesa ulodhamiria.” ITAENDELEA
Posted on: Mon, 15 Jul 2013 03:30:00 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015