SHAMBA DARASA TUJIFUNZE KUTOKA KWA MAJIRANI ZETU (Hapa Wavivu wa - TopicsExpress



          

SHAMBA DARASA TUJIFUNZE KUTOKA KWA MAJIRANI ZETU (Hapa Wavivu wa Kusoma Wakae Pembeni) Hosni Mubarak alikuwa rais wa Misri kuanzia 14 Oktoba 1981 hadi 11 Februari 2011.Alipata cheo hicho Baada ya Aliekua Rais wa Misri Anwar Saadat Kuuwawa kwa Kupigwa Risasi 1981.Aliiongoza Misri kwa Takribani Miaka 30 kwa Mafanikio Makubwa sana, Kuanzia 25 Januari 2011 wananchi wa Misri walianza kuandamana dhidi ya utawala wake wakimshutumu juu ya Ubadhilifu na Matumizi Mabaya ya mali za Umma na tarehe 11 Februari Mubarak alijiuzulu na kumkabidhi makamu wake madaraka yote. Mwaka 2012 Wamisri Walipiga kura na Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood Alichaguliwa kwa kura Nyingi kuwa Rais mpya wa Misri na Rais wa kwanza wa Kiraia. Miezi Sita Baadae, June 30, 2012 Wamisri waliianza Kuandamana nchi nzima, Kumshinikiza Rais Mohamed Morsi Kujiuzuru kwa Sababu ya Kujilimbikizia Madaraka Makubwa Kinyume na Makubaliano Utawala wa Morsi ulifupishwa ndani ya mwaka mmoja, Baada ya Jeshi nchini Misri Kumuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo Mohamed Morsi na Kumteuwa kiongozi wa muda Bwana Adli Mansour Aliekuwa Mkuu wa Sheria Katika Mahakama ya Juu ya Katiba ya nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali yake. Zaidi ya Wamisri 500 Wameuwawa na 1500 Kujeruhiwa tangu kuanza kwa vulugu za Kumuondoa Hosni Mubarak na hatimaye Mohammed Morsi madarakani. ` Maswali Je Unanishawishi namna Gani ya kwamba Mabadiliko ya Kisiasa,Yaani Chama cha Upinzani Kikipewa Dhamana Kinaweza Kuiongoza Tanzani Vizuri Zaidi ya Serikali CCM? Je Unafikili what are The Basic Criteria’s we Need to Consider for the Best Presidential Contestant? Je ni kweli kwamba Wamisri Hawakutambua Wanachokichagua?(Hawakumfahamu fika Mohamed Morsi?) Je Kiongozi Unaetarajia Kumchagua Anauwezo wa Kuendeleza Umoja na Mshikamano wa Taifa Letu? Je Huyo Unaetegemea Kumpigia Kura 2015 Anafaa? Ana Vigezo gani? Wamisri Wengi Walishinikiza Mohamed Morsi Ang’oke Madarakani na Wengi pia Waliandamana Mohaded Morsi Aludi Madarakani! Je Tuamini Kundi Lipi Kati ya Haya? Kwa Mazingira ya Namna Hii, Unawezaje Kunishawishi ya Kwamba Dr Slaa Anafaa Kuiongoza Nchi Hii?
Posted on: Tue, 29 Oct 2013 06:54:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015