SIMULIZI FUPI: NAJUTIA MAAMUZI YANGU. MTUNZI : - TopicsExpress



          

SIMULIZI FUPI: NAJUTIA MAAMUZI YANGU. MTUNZI : CHARLES LIGONJA J. “Phares usinione hivi,hapa nalia kila siku,sina raha na ndoa yangu,najuta kwanini nilikusaliti eti nilijifanya kufata pesa kwa Donald,kiko wapi,leo naletewa wanawake mpaka wawili ndani na kutambulishwa kama dada mtu,mwone vile Yule mwanaume,mbwa nakwambia mbwa kabisa” “Punguza ukali wa maneno basi” “He! we si humjui,jamani niache niongee,naomba unisamehe na uniache niongee,Phares natamani muda mwingine kujutia maamuzi yangu lakini hapana inawezekana nimeenda kule kujifunza kitu,sitaki kujutia maamuzi yangu na ndio maana leo niko mbele yako kuongea ukweli,na naomba nikimaliza kuongea nenda tengeneza CD nzuri na kuisambaza ili kama kuna wasichana wenye kutaka wanaume wenye pesa kama mimi na kukusaliti waliotoka nao mbali kama mimi na wewe kisa huna kipato basi wafute hilo kwani sina raha na kizuri zaidi pesa hutafutwa,na wewe leo unamiliki kampuni kubwa ya kusindika nyama ya ng’ombe ambayo unaiuza Afrika nzima,nilichofuata kule mpaka leo hata sioni faida yake,nimekalia masimango na dharau za kila aina.” “Hahahahahahaha Phares nilikuwa nakwambia soon naenda kutembelea makalio mume wangu akiwa pembeni (gari) wapi! sijawahi kupata nafasi ya kuendesha gari hata siku moja mume wangu akiwa pembeni” “Maneno yako bado makali sana, lakini kama unakutana na makali kama hayo mbona huzeeki?” “Najipa raha mwenyewe babu kwani sitaki kufa kabla ya kutoa ukweli huu,onesha sura yangu kwenye hiyo CD ili ujumbe ufike vizuri ” (hapo usiparushe kwenye hii CD) Scola alinong’ona. “Phares haya yanayonikuta nimeyataka mwenyewe ila sikati yawakute wasichana wengine hasa wanachuo kama nilivyokuwa mimi, wengi tunataka maisha mazuri mara baada ya kumaliza chuo,kweli sio dhambi lakini hatutakiwi kudharau waliojitoa kikwelikweli,waliobeba maisha yetu tukiwa vyuoni au popote ” “Katisha kidogo nilie” Alipohakikisha kamera imezimwa kweli alianza kulia na kuzungumza yote aliyoweza kuyakumbuka muda ule. “Phares how many times nilikuwa nategemea mfuko wako pindi tuko kidato cha tano, kila kitu nilikuwa Napata toka kwako na sio kwamba ulikuwa na pesa nyingi la hasha isipokuwa upendo,hukutaka kuona nakosa chakula,yote hayo ulinifanyia lakini hata siku moja sikukupa penzi nikikuahidi siku tukifanikiwa kuanza chuo basi nitakutunuka lakini wapi hukuwahi kulamba hata tulipoanza chuo lakini katu hukukoma,we au unataka kuniloga?,mtu gani usiyekata tama,kupenda gani huku?” “Umeamua kunitukana sasa!” “Hapana,sielewi kwanini?” Aliongea mengi sana mpaka giza likaanza kuingia lakini katu hakuona tatizo, aliendelea kuongea na kila nilipomtaka kurudi nyumbani kwani mume wake atafika nyumbani na kumkosa,hapo aliamsha mengine makubwa sana. “Nyamazaaaaaaaaaaaaaa! nani nimuwahi nyumbani ,sijawahi kukosekana nyumbani na kupigiwa simu kuulizwa niko wapi yani kwa kifupi hata kama nataka kulala huku hatonitafuta,kwa kifupi atafurahia kunikosa nyumbani ili avushe mtoto na hata nikirudi na kumkuta yeye amesharudi hana muda wa kuniuliza lakini pia ikitokea nimerudi na kukuta mlango wa chumbani umefungwa basi nisijisumbue kugonga,nimwache afanye yake…Donald mbwa niamini” “Bado sitaki kuamini kwani hayo bado madogo” “Una wazimu wewe, madogo hayo,sawa una haki ya kusema hayo kwani nimekutenda sana” “Natania” “Natania, unatania nini? mi naumia we unafurahi au unanikomesha kwasababu ya kukutenda vibaya,Phares naomba unisamehe na naomba ieleweke nasikitika kukufanyia vile na nakuombea heri kwenye ndoa yako,mpende na kumheshimu mkeo,mkeo ndio atakusikiliza na kukushauri mambo mengi kuhusu maisha yenu na familia yako,mkeo ni kila kitu,sikiliza hii nayo uone kama namuonea ama la!” SAA MOJA USIKU. “Nilitoka kazini na kupitia buguruni sokoni kununua mahitaji ya nyumbani,siku hiyo nilitoka mapema sana kazini na kupata gari lililonifikisha nyumbani mapema,nilipofika nyumbani niliacha mizigo na kurudi saluni kwani nywele zangu zilikuwa zinaniwasha sana,nilipita njia za mkato toka nyumbani maeneo ya Ukonga Magereza mpaka karibu na kota za polisi pale Magereza,nilipovuka reli tu nikakutana na gari ya mume wangu imepaki pembezoni mwa reli,kuona vile niliamua kulifuata,nilichokikuta huwezi amini,nilimuona Donald akiwa na mwanamke wakifanya ngono…unaamini kama Donald mbwa,nakuuliza wewe unaamini na kukubali nikimwita Donald mbwa?” “Kidogo” “Haya endelea kuamini kidogo kidogo….nililiendea lile gari na kugonga kioo,walishtuka sana lakini alipoona ni mimi aliendelea kufanya uchafu wake,Yule mwanamke alishtuka sana,nilitaka afungue kioo nikambulia kutukana na kuoneshwa kidogo cha tatu toka kidole cha mwisho (dole) niliumia sana kutukanwa na mume wangu na badae Yule mwanamke nae alinionesha nae kidole kama alivyokuwa akifanya mume wangu,hasira zilibanda na kuchukua tofali la mchanga lililokuwa karibu na reli na kulirusha kwenye kioo cha mbele” “Shaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,kioo kilimwagika na walipoona vile walitahamaki na kukaa sawa,nilimshika Yule mwanamke na kumtoa nje akiwa nusu uchi,sikukoma nalimvuta nje mume wangu,lilikuwa kosa kubwa sana kwani nilipigwa sana na mume wangu akisaidiwa na Yule mwanamke” “Kwani huyu nae nani ?” “Si nilikwambia nina mke , ndio huyu” “Jamani hataki kuona ukipeleke mwanamke nyumbani sasa huku nako kimemuwasha nini mpaka akufuate?” “Namshangaa!” Baada ya kusikia wawili hao wakiongea wakati nikiwa chini naugulia maumivu ghafla hasira zilipanda na kumvamia Yule mwanamke lakini kabla sijampiga vizuri nilishikwa na mume wangu na kuingizwa kwenye gari kama mzigo na yeye kuingia na kuniambia nisimsumbue kwani kama huyo msichana nimuone hapo ameanza kabla ya kunioa mimi hivyo basi nimheshimu na sasa tunaenda wote nyumbani kwani nimeyataka mwenyewe” Kweli Yule dada niliyekuja fahamu jina lake anaitwa Subira aliingia na kuondoka,nlitamani kuua mtu lakini sikuwa na namna. Walipofika nyumbani moja kwa moja waliingia ndani na baada ya muda waliamua kutoka na kuniacha,sijui walienda kulala wapi wawili hao,nilibaki nyumbani nikalia sana,nilijiona mkosefu sana lakini badae nikaona mbona sina kosa,kwanini yanikute yote hayo au kwasababu ya kumkataa Phares ? “Phares sioni raha ya mapenzi,ndoa hii kwangu imekua shubiri,nimeteswa sana,mwanamme ambae nilimkuta akiwa na uchafu wake na kumshawishi kwenda hospitali akatoa mkono sweta leo ananiona mimi sio kitu,Donald…Donald wewe!” “Na pesa zote alizokuwa nazo alikuwa bado na mkono sweta, tohara ilimpitia mbali?” “Usimwone vile,vitu vingi tumefanya pamoja lakini leo ananiona sina jpya eti sijui kufanya mapenzi labda lakini kama kujibinua najibinua sana nikiwa nae mpaka mwenyewe ananisifia sasa sijui huko nje anapewa nini mpaka ananiona sijui kitu,mwanzoni mengi nilikuwa siyajui lakini badae nikaonana na shosti yangu nae akanipa darasa la namna ya kumfanya mwanaume apagawe lakini wapi sio Donald!,eti kuna kitu gani mnapewa huko nje?” “Unamuuliza nani?” “Wewe huyo au niko na nani hapa?” “Sina hizo mambo” “Hongera kwa kuwa mume bora” “Asante sana,endelea” “Nilimpenda sana mume wangu lakini anayonifanyia kwa kweli sijui nilie na nani,mtu gani asiye na heshima hata kidogo kwa mkewe kama kumpenda nampenda sana au anatumia upendo wangu kunitesa,nyie wanaume wapuuzi sana unajua mwanamke anaweza kukuua sekunde tu…ngoja aendelee nitamuua” “Unasemaje wewe?” “Hapana ulimi umeteleza lakini kanitesa sana, Donald kisha niua” “Kakuuaje, mbona unanichanganya, sitaki kusikia kama una maambukizi” “Hapana sina UKIMWI isipokuwa moyo, Phares moyo unauma sana,s ikuwa na presha lakini kuzimia nimeshazimia sana kutokana na maumivu anayonipa huyu mwanamme” “Phares unakumbuka tulipokuwa mwaka wa pili wakati unataka kupeleka posa nyumbani nikakuambia muda bado,hapana haikuwa bado isipokuwa tayari Donald alishapeleka posa nyumbani na nilipokuwa naaga kwenda Morogoro kusalimia wazazi sio kweli nilikuwa naenda kwa Donald,nilikuwa nakudanganya kwamba mimi bado bikira kumbe siku nyingi nilishatolewa bikira yangu na huyu mbwa,alifaidi sana kunikuta bikira!nimeitunza bikira yangu kwa maana ya kuja kukupa hiyo zawadi wewe lakini badae nikakusaliti,nisamehe sana na nakutakia kila la kheri wewe na familia yako” “Nilishapoa mpen…” “Unasita nini kabla ya mkeo mimi ndiye mwenye mali, mimi ndiye uliyekuwa ukiniita mpenzi ,kataa?” Ni ukweli usiofichika kwani hakuifurahia ndoa yake, alijutia maamuzi yake,hakutaka kuolea na mwalimu,hakuwa tayari kuona yeye analeta laki tatu ndani mwisho wa mwezi na mume wake analeta kiwango hicho hicho. “Nilisahau,tulipokwenda mafunzo kwa vitendo mwaka 2007 nilikutana na Maua,unamkumbuka?” “Yule alikubeba hall two?” “Basi bwana nikafikia kwake, siku moja katika stori mara akanionesha salary slip (karatasi ya mshahara) yake yani baada ya makato ya lazima ikiwemo kodi, hela ya mkopo, bima ya afya nikakutana na makato ya NJAA yaani mikopo mara NMB,Bayport,B-blue,Faidika n.k nikachoka kwani kiasi anachopokea mwisho wa mwezi mh,aibu 50000/= bado nyumba ya kupanga alipie” “Hilo nalo lilichangia kuona hutafaidi kuolewa na mimi?” “We acha tu nilidharau ualimu kwa kiasi kikubwa sana,ni kweli lakini walimu wengi wana maisha magumu kwani mbali na madeni ya taasisi za fedha kuna mengine,kwa mpemba nako anadaiwa mchele,sukari n.k,jamani maisha gani haya!” “Mh!” “Basi kiboko mwalimu Kamwela yani amekopa mpaka mshahara unabaki hasi (negative),unajua kilichomkuta?” “ Nambie ? ” “Alimpa mimba mwanafunzi,wazazi wake wakaja juu na kumpa mapendekezo mawili,moja kama anataka kuendelea na kazi basi amalizie nyumba ambayo baba yake na huyo msichana ilikuwa hatua ya kupiga bati na la pili basi amuoe binti yao,kumalizia nyumba kulimtoa 10 milion,ukimwona jamaa leo akilia haiku sawa kisa madeni ama kweli ualimu huu usipokuwa makini utaishia shikamoo nyingi toka kwa wanafunzi! Na kama atakataa basi atamfunga ikabidi akubali kuingia kwenye hiyo gharana..kuna wazazi noma kweli” “Ngoja niweke memory card nyingine kwani hii imejaa,kulikuwa na vitu vingine” “Hapana nimemaliza, ole wako uchakachue baadhi ya mambo,nataka utoe LIVE” ****** “Donald kumbuka mimi ni mke wako, kumbuka kiapo chetu kanisani, sikukatazi kufanya hayo lakini niheshimu kidogo basi, unaniletea ndani? Kila siku nilikuwa namwambia hayo lakini katu hakunisikiliza na leo naongea tena kokote uliko ukiiona hii CD basi ujue nataeska sana kwa unayonifanyia” “Imeshafika saa nne usiku,nimechoka” “Lazima uchoke lakini hutoki mpaka nimalize,Phares bado kidogo…basi bwana siku moja nimetandika vizuri kitanda na kujiandaa kumpa penzi moto moto mume wangu kwani alikuwa ameanza likizo,kilichonikuta sasa…aliporudi nilitenga maji akaoga na badae akala chakula na kuingia chumbani nami niliingia na kutoa nguo zote kwani nilimmiss sana,akaniuliza” “Vipi night dress umeifua” “Kwanini?” “Naona uko hivi hivi?” Nilijizoa na kupanda kitandani,mwenzangu akajifunika shuka hadi kichwani na kuniambia amechoka sana hivyo nilimwache alale na nisimguse mpaka asubuhi,mbona nilikoma na libido langu koma na siku ya pili yake akaniletea night dress kumi ili nisimkalie tena uchi” “Nimekuletea hizi ili moja kama umeifua basi utavaa nyingine sio kukaakaa uchi kama mtoto mdogo kwani nikikuhitaji nitakueleza mapema ujiandae, sawa?” “Phares kidogo nizimie kwa hayo niliyoyasikia,Donald hajali hisia zangu” Scola alimuuliza Phares “No comment!” ASANTE KWA KUFUATILIA KIPINDI HIKI. MWISHO ***SIMULIZI HII NI YA KUBUNI IKIWA NA LENGO LA KUBURUDISHA NA KUTOA ELIMU****
Posted on: Tue, 20 Aug 2013 07:15:39 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015