SIMULIZI FUPI: USINIACHE MTUNZI : CHARLES LIGONJA - TopicsExpress



          

SIMULIZI FUPI: USINIACHE MTUNZI : CHARLES LIGONJA J. “Unaenda wapi?” “Sina niendapo zaidi ya kusubiri mteja” “Sawa panda twende” Sandra aliingia kwenye gari ndogo aina ya Ford escape na kuondoka mara baada ya kukubaliana na mteja wake,wakiwa kwenye gari waliongea mambo mengi sana lakini kikubwa ni kwamba Eric hakuridhiki na biashara aliyokuwa akiifanya Sandra. “Mwaka wa ngapi uko kwenye hii biashara?” “Hayakuhusu,mbona unaniuliza maswali mengi namna hii,twende nikakupe huduma nirudi kazini” “Sina maana mbaya kuuliza,lakini we ni mrembo sana na elimu unayo kwanini usitumia elimu yako kutafuta namna nyingine ya kupata pesa?” “Nanmna ipi tena,nimeenda kwenye kila ofisi kutafuta kazi kila nimuonae huko anataka penzi na kati ya niliowapa penzi hakuna hata mmoja aliyekuwa mkweli kwangu,nasikitika kuwaamini wanaume na kuwapa mwili wangu ambao wameutumia wapendavyo na kuniacha namna hii,we acha nawachukia sana” “Mbona uko na mimi sasa kama unatuchukia?” “Sina namna nyingine ya kupata mkate wangu wa kila siku ndio maana unaona niko kwenye hii kazi,nina wadogo wanaonitegemea,Eric please!” Sandra aliongea kwa uchungu,alionesha kukata tamaa ya maisha na hakuna namna nyingine ya kupata pesa zaidi ya kujiingiza kwenye biashara ya kuuza mwili wake. “Unafikiri ukipata kiasi gani cha pesa unaweza kufanya biashara na kuachana na hii kazi?” “Mh!na wewe tena,kuna wengi wameniuliza hivyo lakini hakuna hata mmoja aliyenipa pesa nifanye biashara ije kuwa wewe?” “Najua kuamini sio rahisi lakini ndiyo hali halisi,nambie nini unataka kufanya?” “Ngono na wewe basi?” “Sandra come on!” “Haina come on hapa!” Eric alibaki kimya kwa muda mrefu akitafakari nini afanye au amwambie huyo binti lakini hakupata namna.Safari ilikuwa ndefu sana mpaka Sandra akapata mawazo na kuuliza wapi huko kusikofikika ni wapi na saa ngapi atamrudisha eneo lake la kazi kwani kufanya na yeye peke yake haitoshi.Sandra alikuwa akilala na wanaume zaidi ya watano na kujipatia mpaka elfu ishirini kwa siku lakini kulikuwa na siku biashara huwa mbaya na kurudi na pesa ndogo au asipate kabisa. “Unanipeleka wapi?” “Mbali sana,vipi kuna shida” “Ipo ndio,saa ngapi utanirudisha kijiweni nikasake wengine” “Kwanini hutaki kuniamini,Sandra sitaki uendelee na kazi hii” “Utanilisha wewe na familia yangu je?” “Niko tayari kukusaidia,naomba nielewe” Sandra alimuangalia Eric kwa muda asijue amwambie nini lakini mwisho wa yote alimwambia hataki kusikia hadithi zake tena na kama hana nia nae basi amlipe na kumrudisha eneo lake la kazi. “Sikurudishi” “Nini?” “Umenisikia vizuri,zaidi ya mara tano napita pale nakuona lakini naishia kukuangalia na kuondoka,nashukuru kwani huwa napokea matusi toka kwako na wenzako,sijui kwanini mko vile au mtu akija sokoni lazima anunue?” “Kwahiyo unakuja kutuchora au?” “Nakupenda sana Sandra,sitaki uendelee na hii kazi,nakumbuka mengi nikikuona” “Ukumbuke mengi yapi?” Eric alikaa kimya kwa muda na badae aliinua shingo na kuanza kumueleza yaliyomkuta mama yake,aliongea akiwa na majonzi wakati huo gari ilikuwa imepaki pembeni ya barabara maeneo karibu kabisa na Pugu shule ya sekondari. “Mama yangu aliingia kwenye hii biashara baada ya baba kupoteza maisha baada ya nyumba yetu kuungua moto,hakuwa na namna ya kutusaidia kwani tulikuwa wadogo kwa umri na hakuwa na wa kumkimbilia ndio chanzo cha yeye kuingia huko” “Sasa kwanini unishangae mimi wakati stori zinafanana?” “Mama alikata tamaa na kuingia kwenye biashara ya ukahaba,hakuwa na mshauri na hakuwa na mtu wa kumpatia mtaji na kibaya zaidi mara baada ya baba yangu kufariki dunia hakukuwa na msaada toka kwa mtu yeyote” “Kilitokea nini badae?” “Alirudi siku moja usiku wa manane na kulia sana mara baada ya kuingia ndani na nilipomuuliza kwanini analia akaniambia yeye wa kufa tu, kwa kweli sikumuelewa anamaanisha nini?” “Ikawaje?” “Alikufa kweli usiku ule ule” “Unanichanganya mbona” “Sikuchanganyi,mama alienda kupima UKIMWI na kugundulika anao na hakuwa tayari kuishi kwa matuamaini ndio hasa sababu ya yeye kujimaliza kwa kunywa aspirin ishirini ambazo zilipunguza mapigo ya moyo wake haraka na kukata roho,inauma sana” Baada ya kumaliza kuelezea Sandra alibaki kimya akimuangalia Eric aliyekuwa akibubujikwa na machozi. “Sitaki na wewe ufe kwa mtindo wa mama yangu” “Acha uchuru basi,nani afe hivyo” “Kama mama yangu alishindwa kuhimili ile hali wewe utawezaje ?” “Jamani mbona leo kazi mteja gani wa kunisomea risala” “Sina maana mbaya kukueleza hilo na naamini mama yangu angekuwa na mtu wa kumshika mkono basi mpaka leo angekuwepo” “Pol e lakini Eric” “Niahidi hutoendelea na hii kazi?” “Mapema sana kusema hivyo,Eric nitaishije?” Kabla hajatoa jibu,Eric alifungua mkoba wake na kutoa burungutu la pesa na kumkabidhi. “Hesabu hii pesa” Akili ya Sandra iliruka baada ya kuona ile pesa alihesabu na baaa ya robo saa alifikisha milion kumi za KiTanzania. “Chukua mbili kalipe ada za wadogo zako na moja kaanzishe biashara ambayo itakufanya uachane na hii biashara” “Nichukue milion tatu?” Wakati wakiongea hayo tayari walikuwa wamefika Majohe kwa Ngosoma alikokuwa akiishi Eric na kuingia ndani,Sandra alimshukuru sana Eric kwa kujitoa kwake na kupanga kumpa zawadi motomoto usiku huo. “Sijui nikulipe nini?” “Unakijua nipendacho toka kwako?” “Penzi? Nitakupa mpaka ukimbie mwenyewe,milion tatu!!!” “Sio penzi peke yake” “Nini tena?” “Acha hiyo kazi ndio zawadi kubwa kwa sasa na badae” “Mh!” “Unataka kufanya nini?” “Jamani nataka kukupa zawadi” “Siko tayari kufanya hivyo kwa leo” “Kwanini tena?” “Ingia bafuni kaoge uje tule tukalale” Baada ya saa moja badae kweli wawili hao walikuwa kitandani lakini cha kushangaza kila mmoja alilala kwenye kitanda chake,mwanzoni Sandra aliamini hiyo ni danganya toto lakini ndicho kilichotokea kwani baada ya muda tayari Eric alikuwa kwenye usingizi mzito na kila alivyojaribu kushawishishawishi katu hakufanikiwa zaidi ya Sandra kujikuta akijiwa kwa kifupi “Siku nyingine” **************** Wiki moja badae tayari Sandra alishawalipia wadogo zake ada na kubaki na milioni mbili tofauti na alivyoagiza Eric, Ilipita miezi sita bila wawili hao kuonana na kibaya zaidi ile pesa hakuiingiza kwenye biashara kama alivyokubaliana na Eric,alinunua tu nguo na nyingine kulipia kodi ya nyumba na baada ya miezi mitatu akabaki hana kitu,maisha yalikuwa kama zamani,hakuwa na pa kukimbilia zaidi ya kurudi kwenye biashara yake ya kuuza mwili. Wiki mbili badae Eric alimuona Sandra akiwa kazini kama ilivyokuwa hapo awali,aliumia sana kumuona kwenye ile hali kwani aliamini pesa aliyompa angeweza kuanzisha biashara na kuachana na ile kazi lakini wapi? Hakumsemesha wala nini na kitu kizuri zaidi Sandra hakumtambua Eric. “Ngriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii”Siku ya pili yake asubuhi na mapema simu ya Sandra ikaita na alipopokea alikutana na sauti ya Eric “Biashara inaendeleaje?” “Mh!....sij.lak..we uko wapi?”Sandra hakuwa na jibu la moja kwa moja kwani hakuna chochote alichoweza kukifanya kwa kipindi chote na kibaya zaidi aliamua kurudi kwenye biashara yake ya kuuza mwili maarufu kama Uchangudoa. Eric alipiga simu akiwa anajua kila kitu kwani tangu amerudi hakutaka Sandra ajue kama yupo ili aweze kumfuatilia kwa ukaribu. “Biashara imegoma bwana” “Kwanini?” “Hata sijui” “Maisha magumu sana hivyo basi unapopata pesa kidogo lazima uwe mwangalifu jinsi ya kuitumia na kama kufanya biashara lazima uwe na ari toka moyoni ya kufanya hiyo biashara,ukishindwa katu huwezi kufanikiwa” Eric aliona kabisa kwamba Sandra hakuwa wa kufanya biashara lakini nini basi afanye na hataki kumuona akiendelea kujiuza kama afanyavyo sasa. “Kaa chini fikiri kwa kina nini unataka kufanya nini” Hakuongeza neno isipokuwa kuondoka,Sandra kichwa kiliwaka asijue afanye nini,kila kitu aliona hawezi kukifanya lakini mwisho wa yote aliamua. “Nataka kuuza nguo” Kweli baada ya kupata hilo wazo na kukubaliana nalo alianza kutembelea maduka makubwa ya nguo yaliyoko kariakoo na maeneo mengine jijini Dar es salaam na kote huko alijaribu kuangalia bei zikoje na faidi,namna ya upatikanaji wa hizo nguo na baada ya mwezi mmoja alikuwa tayari kufanya hiyo kazi. Alimwambia Eric nae alimsifu kwa hilo wazo na kumsadidia kutafuta fremu kariakoo na baada ya wiki moja alianza biashara,biashara yoyote mwanzo mgumu na ndivyo ilivyokuwa kwa Sandra kwani alipofungua siku zingine alikuwa hauzi kabisa na njaa nayo ikachukua mkondo wake,Sandra hakuwa na uvumilivu hata kidogo ingawa maisha yake hayakuwa ya juu sana,upande wa Eric yeye alikuwa na mambo mengi yaliyomfanya akose muda wa kukaa nchini na huo mwanya ukamrudisha tena Sandra kwenye biashara yake na kutokana na kuwa dukani wengi waliokuwa wakitaka huduma toka kwake walikuwa wakimlipa pesa nyingi. “Yani niikatae laki mbili kisa Eric!” Sandra alikuwa akiwaza hilo baada ya kupigiwa simu na mmoja wa pedeshee aliyekuwa akitaka huduma toka kwake na ndivyo alivyopkuwa akifanya,alikuwa akifanya biashara kwa simu sio kama kipindi cha nyuma kwenda kusimama Kinodoni kusubiri wanaume. Kujiuza kwa simu hakukupelekea Eric asijue afanyalo Sandra.aliumia sana kuona mtu ampendae anashindwa kubadilika na kuachana na biashara ambayo si halali,biashara ambayo ilimuua mama yake,alijitoa kumsaidia Sandra ili aje kuwa mke wake lakini kila afanyalo haoni kama kuna mabadiliko yoyote. “Sandra!” “Eric!” “Nisamehe” “Kwanini urudi tena kwenye hii kazi,duka halikutoshi mama,nifanye lipi ili uachane na hii kazi?” “Nisamehe,sitarudia” Alipomdodosa ndipo alipogundua Sandra anataka faida ya haraka au pesa ya chap chap sio kusubiri mwezi au mwaka mzima. “Sikiliza nimekupa pesa ili uachane na hii kazi lakini huoneshi kuelewa,sasa endelea” “Mh!” “Endelea kwani hayo ndio maisha uliyojichagulia” Ilikuwa aibu ilioje kwani siku hiyo Eric alifika dukani na kukuta duka limefungwa na kwa vile alikuwa na funguo nyingine aliingia na kujifungua na hili lilitokana na taarifa aliyoipata kwamba siku zingine hasa jioni Sandra alikuwa akimaliza na wateja wake mle dukani. “Laki moja ya haraka ipo nikupe kitu” “Fanya 50000/=” “Poa” Yalikuwa maongezi ya huyo jamaa na Sandra mida ya saa moja jioni na baada ya kukubaliana geti lilifungwa tayari kwa shughuli na hapo ndipo Eric alipojitokeza. “Sandra mpaka dukani kweli?” “Sijui nini…hata mimi sielewi” “Unasemaje Sandra,ina maana unafanya hili bila kutambua kama unakosea?..nikufanyie nini we mwanamke?” “USINIACHE,ERIC PLEASE USINIACHE” “Utaniua Sandra,we endelea tu” “SANDRA ALIKUWA HABEBEKI KWANI KILA AFANYIWALO ILI AACHANE NA HIYO BIASHARA BADO ALISHINDWA,ANATAKA PESA YA HARAKA LAKINI KATU HAJIULIZA VIPI AKIPATA MARADHI,LAKINI JE HIZO PESA ZA HARAKA ZIMEMNUFAISHA KWA KIPI KAMA SIO MAUMIVU KWANI KISHATIBU KASWENDE MARA TANO LAKINI HAKOMI AU SIKIO LA KUFA?” MWISHO.
Posted on: Mon, 19 Aug 2013 07:48:58 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015