SIMULIZI LA KAHABA SEHEMU YA 5 MAISHA YA MTAANI Huku mitaani - TopicsExpress



          

SIMULIZI LA KAHABA SEHEMU YA 5 MAISHA YA MTAANI Huku mitaani waliniita majina kama JLo wakati mwingine salma hayek yaani wale waigizaji maarufu duniani kwa urembo nilio nao na mvuto wake , hakuna hata mmoja aliyekuwa na mawazo kama nimeadhirika au la kwa maana yule kijana niliyekuwa nae kama mpenzi alikufa kifo cha ghafla watu walisema amekufa kwa pressure . Mitaani napo nilikamua kinoma , waume za watu walikuja mpaka mlangoni kwangu na magari yao , wananipakia na kunipeleka katika kumbi za starehe na sehemu nyingine nyingi sana wengine walinihonga mali na mambo kibao kisa wamenipenda wanataka ngono Na kwa uhakika hawa wanaume niliwapanga sawia kabisa na hakuna aliyeweza kutambua mimi nina wanaume wangapi na wanaishi wapi wengi walijua ni washirika wangu katika kazi zangu na mambo yangu mengine kwanza sikupenda kuongea na mwanaume wowote chumbani kwangu wote nilikuwa nawaambia tukutane mbali kidogo na nyumbani haswa kati katika ya jiji . Katika hawa wateja wangu kulikuwa na kijana mmoja anayeitwa juma huyu juma alikuwa na rafiki yake mmoja anayeitwa Shy , kijana mwembamba mwenye umbo la wastani , hana ndevu halafu ni mcheshi sana , alifanikiwa kuiteka moyo wangu , sasa nilitaka kumwambia mara kibao kwamba nimemzimia Tatizo ni kwamba anayekuja kunichukuwa pale ni juma , juma huja pale kwa kusindikizwa na Shy , basi juma akanitambulisha katika website moja inayoitwa serengeti nyumbani nikienda kupumzika nilipenda kushinda katika tovuti hii kuchat na marafiki na watu wengine . Huyu shy nae nilimkuta katika site hii usiku wa manane anachat na jamaa zake , ila siku moja nilikutana na kijana mwingine anayeitwa politeman , huyu ndio alinichanganya kabisa , kwanza jina lake na jinsi aliyokuwa anaongea kweli nilizimia mwenyewe bado nikawa na siri kubwa moyoni je hivi tukifanya ngono inakuwaje ? Maisha yaliendelea tu , basi nikimpenda politeman , huyu kijana akawa anakuja mpaka nyumbani kwangu wakati mwingine na huwa nampa computer yangu aitumie tukaenda zaidi nilimshitukia kumbe huyu polite ana urafiki wa kimapenzi na dada mwingine anayeitwa salma siku moja walipanga kwenda kufanya mapenzi lakini polite akakataa ? Sikuamini macho yangu wala masikio siku nyingi kama naota kumbe polite alikuwa na urafiki na dada mmoja anaitwa Maria Chipz ?? Sikuamini , nilimuheshimu sana maria na sikutegemea kama anaweza kufanya hivyo hata siku moja , muda ukaenda kumbe kuna dada mwingine anaitwa REHEMA naye alikuwa anampenda Politeman Miss upanga Naye anampenda Politeman we acha tu Nikamwaga chini sikupenda tabia zake za kitoto kitoto anazowafanyia hao kina dada wengine ingawa nilifanya nae mapenzi kama mara 4 hivi na mara zote hatukutumia kinga na nilikuwa nimeadhirika ila ni siri yangu , polite hajui na wengine wote hawajui lakini ndio maisha hayo Haya ndio hivyo , nami sasa hivi nakaribia kufariki dunia niko zangu kitandani hapa hospitali ya Amana mkoani dar es salaam , kweli maisha ni safari ishi upendavyo na sio watakavyo , mwisho wa yote dunia sio hadaa wala dunia haikuchukii au haitaki kukufanyia chochote kibaya Bali watu ndio hadaa , hata kama ni ndugu yako rafiki yako , hakikisha humpi nafasi akutawale aweze kukumiliki wewe na kukuamrisha chochote kile anachotaka yeye , kama ukifanya hivyo ndio utaishia kubaya kama mimi Bosi wangu alinimiliki sana nikampa penzi , kijana wa mitaani nae alinimiliki mpaka sasa nimeaona faida zake na hasara zake Wacha ningoje siku zangu nife nizikwe niende ahera Kwaheri . MWISHO
Posted on: Mon, 16 Sep 2013 20:10:51 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015