SIMULIZI : NYUMBA YA KIFO (HOUSE OF DEATH)-01 MTUNZI - TopicsExpress



          

SIMULIZI : NYUMBA YA KIFO (HOUSE OF DEATH)-01 MTUNZI : CHARLES J LIGONJA. SIMU : 0714 79 77 78 . Mungu nasema asante sana kwa kunifikisha salama mkoani Kigoma na hatimae kilichonipeleka kule kukimaliza salama na sasa nipo Nzega naendelea na majukumu yangu kama kawaida,sifa na shukrani ni zako baba unitiae nguvu. ILIPOISHIA... “Hayo ndiyo mambo,hamishia kwenye namba yangu au mnasemaje?“ Yule nesi aliungwa mkono na wenzake,alihamishiwa hizo pesa na haraka waliinuka na chupa ya damu na kuipeleka wodini tayari kwenda kumuongezea Angella. ENDELEA..... Rushwa iko ya namna nyingi sana na kila mtu anachukulia kwa namna anayoona yeye inamfaa lakini kwa kifupi rushwa ni kitendo cha mtu kulipia huduma fulani ambayo ana haki ya kuipata bure,kuna wengine wanatoa rushwa ili kukwepa mkono wa sheria lakini kuna wengine hulazimika kutoa hata rushwa ya ngono ili tu aweze kupata huduma au kazi,nd’o maana rushwa ina namna mbalimbali ya kuielezea. Kwenye ofisi zetu hasa za serikali hali imekua mbaya sana,una haki ya kupata huduma fulani lakini huyo wa kutoa hiyo huduma anakuzungusha ili tu uweze kumpa pesa (rushwa). Mara utasikia njoo kesho,mwingine atakuambia faili lako halionekani lakini cha kujiuliza kwanini halionekani wakati yeye ndiye hasa anahusika na kutunza hilo faili na kwanini ukimpa pesa analipata?Maana yake alilificha ili tu uchoke na kumpa pesa ili alitafute,rushwa ziko sehemu nyingi hasa katika maisha yetu ya kila siku,unaenda shuleni unaweza kutana na mwalimu akataka rushwa ili labda akupe cheti chako,unaenda kwenye siasa ili ugombee nafasi fulani unakuta kuna kigogo mmoja anataka rushwa na kama kwa mwanamke basi kuna mawili rushwa ya ngono au pesa ,kuna wale tuliowapa dhamana ya kuingia mikataba mbalimbali huko nako rushwa imeshika hatamu,mtu yuko tayari yeye kupata asilimia kumi na kuipotezea serikali au nchi kwa ujumla mabilion ya pesa,kwa kitaalam huitwa “ten perceny commission“ ,kibaya zaidi hata watu ambao wanatakiwa kuhakikisha afya za watu zinakuwa bora nao wameweka rushwa mbele,madaktari na manesi,inauma sana kuona mtu kukuacha ufe kisa pesa tena mwingine unakuta pesa anayotaka ni kidogo sana ladba shilingi elfu moja ya Tanzania na kutokana na hizo rushwa ndogo ndogo kuna kazi kubwa kuweza kusafisha hiyo hali,nani yuko tayari kufa eti kisa ameshindwa kutoa rushwa tena rushwa yenyewe kidogo na hata ukisema utaenda kuripoti polisi unakuta wote lao moja,wacha tuendelee kutoa rushwa au tufe tu! *********** Manesi walionekana wako busy sana kuingia na kutoka chumba ambacho kwa wakati huo Angella alikuwa amelala huko kitendo ambacho kilimshangaza sana Vaileth ambae tayari aliwapa pesa waliyoitaka ili waweze kumtundikia damu wifi yake. “Kwani kuna nini?“Aliuliza “Ah! Hakuna kitu isipo...kuwa tuna.....unajua mishipa kuipata nayo ngumu eh kazi sa...na!!“ Mmoja wa manesi alijikuta akiongea huku akikatakata maneno. “Mjitahidi basi ili arejee kwenye hali yake na kumwona mtoto wake“ „Ehhh!...nd’o ha..kuna shida“ Hali ile iliendelea kama nusu saa nyingine,huyu anatoka yule anaingia na kila anaetoka kule ndani anakuwa na hali fulani ya wasiwasi,Vaileth alipata wasiwasi sana lakini kila alipouliza aliambiwa mambo yatakuwa mazuri baada ya muda,aliendelea kuvuta subira. “Jamani hakuna namna hapa zaidi ya kutafuta namna ya kuondoka hapa“ “Kwanini?“ “Unauliza nini,ina maana huoni kama kishafariki huyu?“ Dokta Mathias aliongea kwa sauti ya chini iliyojaa wasiwasi. Walishachelewa kwani tayari Angella alishageuza macho,roho iliachana na mwili,kila nesi alishikwa na butwaa na dakika tano badae kila mmoja alitoka mle wodini akiwa mwenye majonzi. “Vipi mbona mmetoka na wakati pesa tayari?“ “Huoni kama tayari ame...“ “Ame...nini,mbona mnakatakata maneno?“ Hakuna aliyekuwa tayari kueleza kama Angella tayari alikuwa amepoteza maisha lakini ndio ukweli wenyewe kwani baada ya muda nesi mmoja alijitosa na kwenda kumfunika Angella na hapo ndipo alipojua kama wifi yake hayupo tena. “Mmemuua wifi yangu?“ “Nani kamuua wifi yako?“ “Wewe,kumbe nini mbona mmeacha kumtundikia damu?“Baada ya sentensi hiyo pale ndani palikuwa hapakaliki,Vaileth alikuwa hashikiki wale manesi wote walikimbia baada ya kuona mambo yameharibika,aliyebaki ni yule aliyekuwa akiingia kwani tayari muda wa kubadilishana shifti ulishafika,masikini Angella alikuwa amepoteza maisha kwa kukosa 50,000/=. Hiyo nd’o hali halisi ya baadhi ya hospitali zetu nyingi,kuna haja ya waliopewa jukumu la kuhakikisha afya zetu zinarejea mahali pake kubadilika kwani hujui huyo unaemfanyia huo unyama ni nani na vipi akifa na kuacha watu lukuki wanaomtegemea yeye. ************** Baada ya muda mfupi Dr. Malaika alirudi na moja kwa moja alikwenda wodini kuona Angella anaendeleaje,alikutana na makubwa tayari Angella alikuwa amepoteza maisha. “What happened to her?“ (Kimempata nini?) “Wamemuua,manesi ...ndio wamemuua“ Hakuelewa lakini badae aliambiwa kila kilichotokea,daktari huyo baada ya kuelezwa ukweli alilia sana na kukumbuka wengi waliopoteza maisha kutokana na huduma mbovu na rushwa. “Mtauana sana kwasababu ya rushwa,ona sasa mmemuua na huyu“ Wakati hayo yanatokea Daud alikuwa njiani akipambana na usafiri na alipoona muda unazidi kwenda hapati gari (daldala)aliamua kukodi teksi lakini kukajitokeza tatizo jingine,kama ulijuavyo jiji la Dar es salaam foleni ni sehemu ya maisha ya wakazi wa huo mji,kutoka ubungo waliamua kutumia barabara ya morogoro ili wakifika magomeni waweze kutumia barabara ya kupitia msimbazi centre badae waingilie maeneo ilipo hotel ya Lamada na kutokeza Amana hospitali,tofauti na matarajio yao hali ilikuwa tofauti kwani foleni ilianzia magomeni kagera na ilikuwa ikienda taratibu sana hivyo basi kipande cha kutumia dakika tano mpaka kumi walitumia saa tatu lakini bado walikuwa hawafiki,alitamani kushuka apande pikipiki lakini katika maisha yake alishaapa kutopanda pikipiki kutokana na siku moja kushuhudia dereva pamoja na abiria wake walivyopondwa vichwa na lori maeneo ya Ubungo Plaza. “Foleni haisogei,sijui mke wangu atanifikiriaje?“ “Kwani hajui kama huu mji unashida ya miundombinu hasa barabara,ndio maana foleni hazikomi?“ “Hapana,yuko hospitali na amepungiwa damu kwahiyo ni bora nikiwa karibu niweke nguvu aweze kupata huduma haraka“ Alimjibu dereva wa taksi aliyejitambulisha kwa jina la Kirusi. “Pole sana ndugu yangu,chukua pikipiki“ “Naiogopa sana pikipiki,kaka bodi mwili!“ “Ni kweli likutokea la kutokea basi mwili unakuwa wa kwanza kuathirika,utafanyaje sasa?“ “Ngoja niwe na subira,ntamueleza ukweli mke wangu“ Aliamua kusubiri lakini bado foleni ilikuwa ikienda taratibu sana. *********** Saa tatu na nusu badae Daud alifika hospitali ya Amana na moja kwa moja alienda wodi ya wazazi kama alivyoelekezwa hapo mwanzo na Vaileth na alipofika alishangaa kuona watu wako kwenye makundi,alipoangalia vizuri alimkuta Vaileth na kumfuata mpaka alipokuwa na kutaka kujua kulikoni. “Yuko wapi mke wangu?“ “Mjibuni nyie wauaji“ “Wamemuua nani?“ “Mkeo,mkeo hayupo tena kaka,sijui hata kale kachanga utakaleaje bila mama yake?“ “Mbona sikuelewi,walitaka pesa nimetuma,wamefanya nini sasa?“ Ilikuwa ngumu sana kueleweka kwa wakati huo,kila mmoja alikuwa analia kivyake,Daud alitamani kumshika mmoja wa manesi aliyekuwa eneo lile na kummaliza kabisa na bila juhudi za watu walifika eneo lile kuja kujulia hali ndugu zao basi Yustina (nesi) ambae ndio kwanza alikuwa ameingia muda huo angepoteza maisha,hali ilikuwa mbaya sana. Masikini mke wake aliyetamani kukodi hata ndege ili awahi kuja kuhakikisha anapata huduma lakini badae kukata shauri kwamba atamwomba samahani kwa kuchelewa alikuwa marehemu muda mrefu. MIAKA MIWILI BADAE. Baada ya mazishi ya mkewe,hali ya Daud ilizidi kuwa mbaya,alikuwa akilia na kujiapiza kulipa kisasi kwa wote waliosababisha mke wake na badae mtoto kufariki dunia. “Lazima niue mmoja baada ya mwingine“ “Usiseme hivyo mwanangu“ “Hakuna haja ya kuwaonea huruma hawa watu“ Haikuwa rahisi kumtuliza na kweli kama alivyosema ilikuwa hivyo kweli kwani siku moja alitoka nyumbani kwake na kwenda moja kwa moja mpaka hospitali ya Amana na kumkuta nesi ambae hakujali yuko kwenye mazinginra gani,alimshika na kumkata kichwa kama mtu anavyochinja kuku. “Anaua jamani,anaua“ Ilikuwa sauti ya mmoja wa shuhuda ambae alikuja kuwa shahidi mahakamani na kupelekea kufungwa mwaka mmoja. COMMENTS na LIKES zina uzito kwenye kazi hii. ITAENDELEA.
Posted on: Mon, 30 Sep 2013 06:51:30 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015