SIMULIZI/SHAIRI: CHURA NAMBA 20 MTUNZI: IBRAHIM Gama SEHEMU YA - TopicsExpress



          

SIMULIZI/SHAIRI: CHURA NAMBA 20 MTUNZI: IBRAHIM Gama SEHEMU YA TATU (BETI 40-60) 40.Yakawa maandishini, Yakawekwa kitabuni, Kutaka mshusha chini, Mwana kaning’ang’ania! 41.Kanishika kama nini, Makekele mote ndani, Polisi bila imani, Mimi wanikaripia! 42.”Kakae nae uani, Mtie maji mwilini, Hili joto ninadhani, Ndiyo huyu analia!” 43.”Ajala kitu nadhani, Afande toka jioni, Njaa inakifitini, Kiumbe chake Jalia.” 44.Kiza totoro angani, Bado nipo msambweni, Hakuna dogo jamani, Polisi ukiingia! 45.”Sasa Bwana Marijani, Ondoka nae nyumbani, Ruksa toka mabatini, Sisi tumekupatia!” 46.”Sababu hapa sioni, Mtoto tumpe nani, Wewe fanya ihisani, Ukiwa msamalia! 47.”Ndugu nihurumieni, Naomba tafadhalini, Mke wangu Jasmini, Kwa wivu kapindukia!” 48.”Hakuzaa masikini, Mtoto twamtamani, Katunyima Rahmani, Huyu vipi namwambia?!” 49.Nilipofika nyumbani, Kuingia ukumbini, Mke kaka kitini, Macho kanitumbulia! 50.”Hicho kimburu cha nani, Ulokiingiza ndani, Washusha yangu thamani, Ndivyo ulivyofikia?” 51.”Na mama yake nadhani, Utamleta nyumbani, Umlaze kitandani, Kwako wala si udhia!” 52.”Mke wangu samahani, Hebu mlani shetwani, Ungejua kulikoni, Hayo usingenambia!” 53.”Kwanza ingia jikoni, Pika uji wastani, Ili anywe Khalfani, Asije akatufia.” 54.Kikawa kitahanani, Kama dereva mgeni, Aloibiwa miwani, Nae haoni sawia! 55.Mwenyewe nikenda pika, Uji ulokamilika, Akanywa akatosheka, Mwengine ukasalia. 56.Nikamueleza yote, Sikubakisha lolote, Mwana tumlee sote, Dhima imetuingia. 57.”Mimi ninakwenda lala, Sina hamu na chakula, Nakuona umefula, Hasira zimekujaa!” 58.”Nitalala sebuleni, Wewe kalale chumbani, Na mwanao wa thamani, Mungu atanilipia!” 59.”Kwa kutokuzaa kwangu, Unanitenda mwenzangu, Amini ilipo chungu, Nayo tamu ipo pia!” 60.”Nasema sikudhania, Wala sikutarajia, Mume wanigeukia, Mwanao waniletea?!” ITAENDELEA KESHO SAA MOJA KAMILI ASUBUHI!!!
Posted on: Sat, 03 Aug 2013 04:00:00 +0000

Trending Topics



BUSINESS PACKAGE worth
Lytecaster Steep Slope Reflector Trim 30-45 Degrees Finish: Gloss
MAJI = Majority Agency for Joint Intelligence All information,
#12161 - Trucks are probably the worst functioning automobile and
FYI I should be writing assignments right now, but whats the fun
Анекдоты о переводах и
- Tattoo Week Rio A Maior Convenção de Tattoo e Piercing do
☼ Good Afternoon Hello Everybody Has Been an Awesome Day. A
=>এই জান শুনো আমার না একটা
LASER PHYSICS AND TECHNOLOGY #9 - FIBER FABRICATION There is a

Recently Viewed Topics




© 2015