SIMULIZI YA KUSISIMUA SEHEMU YA 3 kijana David anaendelea - TopicsExpress



          

SIMULIZI YA KUSISIMUA SEHEMU YA 3 kijana David anaendelea kusimulia kisa cha kuwa mchawi kilichomkuta katika maisha yake kabla ya kuokoka. niliishia pale alipomuuliza yule mtoto aliyempeleka chini mbuyu alikuwa mtoto wa nani na alimfahamu vipi. Je, mtoto huyo alijibu nini? Endelea kutiririka.. Baada ya kumuuliza hivyo, alicheka na kuniambia sikuwa na haja ya kujua jina lake na alikuwa mtoto wa nani ila jambo la muhimu nifahamu kwamba nitakuwa mchawi. Maneno ya yule mtoto yalinishangaza sana nikamwambia alichokuwa akikisema kisingetimia kamwe ndipo dogo huyo alitabasamu na kuniambia nitaona. Baada ya kutoa kauli hiyo nikaamua kukemea kwa jina la Yesu, nilipogeuka nyuma nilishangaa kumuona yule dogo katoweka katika mazingira ya kutatanisha. Kufuatia mtoto huyo kutoweka, nilimshukuru Mungu aliyejibu maombi yangu na kujisemea moyoni kwamba kwake hakuna linaloshindika. Nilichokifanya niliondoka kumfuata ndugu yangu aliyekuwa katungulia mbele, nilipokutana naye aliniuliza nilikwama wapi nikamdanganya kwamba nilikuwa najisaidia kichakani. Niliamua kumweleza hivyo kwani sikutaka ajue kuhusu yule mtoto wa ajabu aliyenitokea, tuliendelea na safari hadi stendi. Bahati nzuri nilipata gari nikamuaga ndugu yangu na kuanza safari ya kwenda Ngara, baada ya kusafiri kwa muda mrefu hatimaye tuliwasili salama. Kwa kuwa niliambiwa jina la kijiji alichozaliwa mama mkubwa, nilipofika Ngara niliwauliza wenyeji wakaniongoza kwenda nyumbani kwao. “Wewe ni mtoto wa marehemu?” David anasema aliulizwa na mzee aliyekuwa akimpeleka nyumbani kwa wazazi mama yake mkubwa. Njiani mzee huyo alinipa pole na kunieleza jinsi msiba huo wa ghafla wa mama yangu ulivyowashtua watu wengi pale kijijini. Maneno aliyonieleza yule mzee yalipa uhakika kwamba ni kweli mama mkubwa alifariki ndipo nilijikuta naishiwa nguvu miguuni nikaanguka chini na kuanza kulia kwa uchungu. Kufuatia hali hiyo, walitokea vijana na watu wazima ambao walininyanyua na kuniongoza hadi nyumbani kwa wazazi wa mama mkubwa. Nilipoona umati wa watu nikaendelea kulia ndipo yule mzee na kijana mmoja walionisindikiza walinisihi ninyamaze. Yule mzee aliwaambia watu waliokuwa wakinibembeleza kwamba waniache nimlilie mama yangu mpaka nafsi yangu itakaporidhika nitanyamaza mwenyewe. Kweli baada ya kulia kwa muda nilinyamaza ndipo nilipewa chakula, nilipomaliza kula nilikwenda kuketi sehemu waliyoketi waombolezaji wengine. Baadhi ya ndugu wa marehemu waliniuliza nilifikaje pale wakati sikuwahi kufika hata siku moja, nikawaeleza wakanipongeza kwa kuwa na kicha chepesi. Kwa kuwa tayari ilikuwa usiku, sikuweza kukutana na baba hadi kulipokucha wakati nanawa usoni ndipo aliniona. Baba ambaye hakupendezwa na kitendo cha mimi kwenda kule msibani alinifuata na kuanza kunifokea na kuhoji nyumba nilimuachia nani. Licha ya kumfahamisha kwamba nilimuacha ndugu yangu ambaye ni marehemu alizidi kunijia juu mpaka mzee mmoja alipomsihi aniache kwa sababu nilifika pale kumzika mama yangu. Je ule mzimu utamrudia? Je ni kwa nn Baba alimkataza? USIKOSE SEHEMU YA 4
Posted on: Wed, 06 Nov 2013 19:08:25 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015