SOMA UJUMBE HUU NI MUHIMU SANA Kwanini tupo hapa duniani? Na baada - TopicsExpress



          

SOMA UJUMBE HUU NI MUHIMU SANA Kwanini tupo hapa duniani? Na baada ya kutoka hapa duniani tunaelekea wapi? Haya ni maswali ya msingi sana kujiuliza. Mtu mwenye busara na hekima hujiuliza maswali haya muhimu. Jibu ni kwamba; uwepo wetu hapa duniani ni mtihani ambao Mungu ameuweka ili yamkini tukishinda twende tukaishi maisha ya milele mbinguni. Katika kitabu cha UFUNUO WA YOHANA sura ile ya pili(2) na ya tatu(3)utaona Neno la Mungu linasisitiza maneno haya "YEYE ASHINDAYE ATAYARITHI HAYA..........." kwa mfano katika Ufunuo wa Yohana sura ile ya pili mstari wa kumi na moja ( Ufu 2:11) , Neno la Mungu linasema "........YEYE ASHINDAYE hatapatikana na madhara ya mauti ya pili." Mauti ya pili ni ZIWA LA MOTO sawsa na Ufunuo wa Yohana ishirini mstari wa kumi na nne(Ufu 20:14). Tuko hapa duniani kwenye majaribu ya kila namna ili pale tunapoyashinda hayo basi tunakuwa na sifa ya kuingia mbinguni; ila pale tunaposhindwa basi tutakabiriwa na adhabu ya moto wa milele. Ndugu zangu tumewekewa kufa mara moja tu na baada ya kifo ni HUKUMU (Waebrania 9:27). Swali ni je tukifa tutakuwa wapi milele? Je ni mbinguni pamoja na Mungu au motoni? Oh! Najua wengi shauku yetu ni kuwa na MUNGU mbinguni mara baada ya kufa. Lakini ndugu yangu hatuwezi kuwa pamoja na Mungu mbinguni mpaka tushinde haya majaribu ya hapa duniani (Ufunuo 3:21). Kumbuka kwa nguvu zako huwezi kushinda dhambi! na hakuna hata mmoja hapa duniani aliyeishi bila kufanya dhambi. Taja manabii wote! WOTE hao walitenda dhambi hii au ile isipokuwa MMOJA TU, YESU KRISTO. YEYE aliishi hapa duniani na kujaribiwa sawasawa na sisi katika mabo yote lakini hakutenda dhambi (Waebrania 4:14-15). Kama ilivyo darasani, pale ambapo tunafeli hesabati kwa mfano, lakini wapo wanafunzi wenzetu ambao mmoja hupata 20, mwingine 10 na mwingine 100; huwa tunamfuata yule anayepata 100 ili atusaidie. Vivyo hivyo katika mambo ya rohoni. Yeye aliyejaribiwa katika YOTE bila kufanya dhambi, ndiye tunayepaswa kumfuata ili atusaidie kushinda dhambi (Yohana 1:12). Tukimfuata yeye, hutupa UWEZO wa kushinda dhambi zote (1Yohana 5:18). Sasa, JIULIZE ni kweli hujawahi kutenda dhambi hata moja? Jibu ni la! katika maisha yapo maeneo haya au yale ambayo tumetenda dhambi. Na kumbuka dhambi moja TU! inatosha kututenganisha sisi na MUNGU. Adam na Hawa walitenda dhambi ngapi? Walitenda dhambi moja TU! walikula matunda waliyokatazwa kuyala. HILO TU LILITOSHA KUWATENGANISHA WAO NA MUNGU. Vivyo hivyo na sisi, pale tulipoona wivu, hasira,kinyongo, tuliponene uongo, utani,au pale tulipoiba hiki au kile; au pale tulipofanya uasherati au uzinzi, au dhambi yoyote MARA MOJA MUNGU ALITUTENGA. Leo tumrudie Mungu wetu naye atatusafisha dhambi zetu zote na kutusamehe KABISA. Bila shaka uko tayari leo kutubu dhambi zako tena kwa kumaanisha kuziacha ili tukifa tukakae na Mungu wetu MBINGUNI. Kama ni hivyo fuatisha sala hii inayoitwa sala ya TOBA ili tupatane na MUNGU wetu.. SEMA "MUNGU WANGU, HAKIKA MIMI NI MWENYE DHAMBI. MAISHA YANGU YAMEJAA DHAMBI, NAKUOMBA LEO UNIOKOE NA KUNIPA UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI. LIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU NA ULIANDIKE KATKA KITABU CHA UZIMA KATIKA JINA LA YESU.... AMEN" Oh! ni shangwe mbinguni kwa ajili yako, kwani Mungu anapendezwa na yule anayetubu dhambi zake kama wewe. Tayari wewe ni mtoto wa Mungu na umeokoka sasa. Cha msingi kukumbuka ni kwamba ili uweze kutunza kile kilicho ndani yako ni vyema kutafuta kanisa linalohubiri wokovu na kusisitiza juu ya kuishi maisha ya utakatifu il ili uweze kutunza kile kilicho ndani yako. MUNGU NA AKUBARIKI SANA.
Posted on: Tue, 06 Aug 2013 12:45:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015