STORI SEHEMU 11...baada ya kumwambia vile alimwelekeza mpaka - TopicsExpress



          

STORI SEHEMU 11...baada ya kumwambia vile alimwelekeza mpaka walipokuwa wakiish maeneo ya msasani kisha alimpa elf 10000 Kama nauli yakujia kisha hakutaka kuendelea kuongea nae tena japokuwa Mgoli alitaman apewe muda wa kuongea nae kwan alikuwa na meng sana. Quris alingia kwenye gari na kuondoka japokuwa marafik zake walikuwa wakimwomb amsameh kutokan na hali ile ya maisha alikuwa nayo Mgoli yanahtaj msaada sana. Mgoli aliondoka pale huku watu wakimshangaa sana japokuwa hakujali hilo yeye aliangalia maslah yake kwan wengne walimuona bwege kulia kwa sababu ya mwanamke. Aligairi kutembea kwa miguu kwani alipewa fedha ile hvyo basi alienda kariakoo haraka na kurudi. Quris alipofika nyumbani alimkuta mama yake na kumwambia wajiandae kumpokea mkwe wao hvyo basi wazazi wake wote walikaa tayari kupokea ugen na waliahirisha safari zote kisha kuandaa chakula kwajili ya mgeni. Ilipofika muda wa jion ndugu wa familia akiwemo mjomb wake Quris aliyekuw akiish kijitonyama pia alipewa mwaliko ule. Mama yake Quris hakujua kuwa mkwe aliyekuwa analetwa pale nyumbani ni Mgoli hivyo basi alizidisha furaha sana yakumwona mkwe wake mtarajiwa. Mgoli alisita kwenda na alikuwa na mawaz sana kuhusu swala lile ila msukumo wa marafiki zake ndio uliofanya mpaka ajiandae kwenda ukweni,alipanda daladala akiianza safari kuelekea ukweni,alikuwa amevaa mavazi ya kawaida sana na yakimaskin ili kutokuficha uhalisia wa maisha yake. Aliposhuka kituo cha daladala aliulizia mtaa alioelekezwa na mpenz wake Quris,alipata kufika mtaa ule na kuanza kutafuta namba ya nyumba aliyoelekezwa. Alifanikiwa kuelekezwa na majirani pale,alishangaa kuona ni nyumba yakifahari sana kwan ilikuwa ni ya ghorofa na uzio mkubwa uliozunguka nyumb hyo,alipofika getini aliogopa hata kugonga mlango kwa kuhofia atachafua ila palikuwa na mlinzi aliyepewa tarifa za kumpokea mgeni hvyo basi alivyomuona anashangaashangaa nje pale aliamua kumuita na kumuliza kuwa niyeye? Kweli alifanikiwa kuingia pale lakin alishangaa kuiona gari ya yule mama,hapo alianza kupata wasiwasi.itaendlea!
Posted on: Wed, 30 Oct 2013 09:31:17 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015