STORY:MKE WA MTU MTUNZI:JUNIOR NICKSON KING SEHEMU YA ISHIRINI - TopicsExpress



          

STORY:MKE WA MTU MTUNZI:JUNIOR NICKSON KING SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA (27) ***************************** Lengo hasa la kutaka kuingia mle ndani ni kumuua mtoto wao ili na wao watoe machozi kama niliyoyatoa mimi baada ya kupoteza wazazi wangu. Baada ya kutoka pale na nikamuuliza mtoto yule kama alikuwa akifahamu kikundi chochote cha vijana watukutu, lengo langu likiwa ni kupata bastola kwani niliamini bila basto kazi yangu ingekuwa ngumu kukamilika. Tukaongozana na mtoto yule mpaka tulipofika sehemu iliyokuwa na jumba bovu ndipo akaniambia nimsubiri, haikumchukua muda mrefu akarudi akiwa na kijana mmoja mwenye mwili mkubwa, basi alipofika nikashangaa anaanza kunirushia makonde na mateke kiustandi mkubwa, akili yangu kwa haraka alitaka kunipima kama mimi ni polisi au lah! alipoona sijajibu mashambulizi ndipo akaniacha na kuniuliza shida yangu kwake. Nilimweleza shida yangu lakini akaniambia kama nahitaji kitu kama hicho nirudi kesho yake majira ya jioni sana. Sikutaka kumhoji kwanini tusimalizane muda ule, nikamuaga na kuondoka. Sikutaka kuendelea kuwa na mtoto yule, nikampa kiasi fulani cha pesa kisha nikamruhusu aondoke zake. Kama tulivyopanga na kijana yule, kesho yake jioni aliweza kunikabidhi bastola ndogo na mimi nikamkabidhi kiasi cha fedha tulichokubaliana. Usiku wa siku hiyo nilipokabidhiwa hiyo bastola akili zangu hazikuwa sawa kabisa nilikuwa nikiwaza ni jinsi gani nitamtoa machozi Kopro yule. Wazo la haraka ambalo lilikuwa ni rahisi kukamilisha mpango wangu ni kujua kama Jackline huwa anamuacha mtoto wake nyumbani pamoja na mfanyakazi au anaenda naye kazini, kama kawaida sikutaka kulaza damu katika kufuatlia hilo. Siku iliyofuata ilikuwa ni jumatatu niliamka mapema sana kwani nilijua lazima awahi kufungua supermarket yake, ndani ya nusu saa nilikuwa jirani na nyumba yao huku macho yangu yakiwa makini kuona kama atakuwa na mtoto. Kwa jinsi akili zangu zilivyokuwa zimeruka sikukumbuka tena ka Jackline huwa anatoka na gari kwenda kazini ambalo lingenizuia kuona kilichoko ndani, wakati huo niliwaza kisasi tu japo na mimi nilikuwa na makosa yangu huko nyuma. Wakati naendelea kukodoa macho ikatoka gari nyeusi aina ya lexus v8, taratibu ikaanza kuondoka eneo lile la nyumba, sasa hapo nikawa njia panda kwani sikujua aliyetoka ni Kopro au Jackline. Nikaendelea kusubiri tena kama dakika kumi lakini hakuna aliyetoka ndani,sikuona sababu ya kungoja eneo lile ikabidi nichukue bajaji ili inipeleke kule supermarket. Bahati nzuri nilipofika nje ya supermarket nikaikuta ile gari ikiwa imepakiwa , moja kwa moja nikatambua Jackline yupo ndani. Kweli binadamu tunabadilika ndani ya siku kadhaa tu, leo ukaonekana mzuri,mbaya,kijana,mzee au mwonekano wowote ule kwasababu umebadilishwa na kitu kimoja tu, fedha au umasikini. Hii kauli ilijidhihirisha nilipoingia mle supermarket kwani nilipishana kabisa na Jackline lakini hakunitambua kabisa na kama unakumbuka nilienda mpaka kwake lakini pia hakunitambua kabisa, sikuwa nafanana kabisa na mwanzo kipindi nampagawisha kitandani . Nilijizungusha mle bila sababu ya msingi lakini sikumuona mtoto wake kitu kilichopelekea nijue amemuacha nyumbani. Nikanunua kitu ambacho hata hakikuwa na umuhimu kwangu kisha nikatoka lengo likiwa ni kuelekea nyumbani kwake ili kutimiza lengo langu, sikuwaza kama nitamkuta Kopro wake wazo ni liwalo na liwe lazima niue kama alivyoua kwa upande wangu. Hapa sikutaka usafiri wa aina yoyote bali nilitembea kwa miguu ili kama nitafanya tukio basi isiwe rahisi kugundulika. Bastola yangu ikiwa kiunoni, nilitembea mwendo wa dakika kadhaa ndipo nikawa naitazama nyumba ile ya kifahari kwa hasira zilizopitiliza. Nikasogea getini na kugonga, cha kwanza mlinzi alipofungua mlango nikamuuliza mzee (kopro) kama yupo akaniambia hawapo wote bali kuna mfanyakazi tu ndani pamoja na . Sikusubiri amalizie sentensi yake kwani nilijua anataka kusema, "pamojs na mtoto" akashangaa teke lenye uzito mkubwa likitua kwenye mbavu zake na kuanguka chini huku akiugulia maumivu makali, nikamfuata pale alipodondokea kisha nikamzi.. Je kipi kitaendelea baada ya mlinzi yule kumuweka chini kwa pigo la mbavu? Itaendelea kesho,,,, maoni yako muhimu. Leo mtanisamehe kwani nimeiandika fupi. CHINGA SAA 11 JIONI ATAKUWA HEWANI.
Posted on: Thu, 05 Sep 2013 05:03:59 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015