STORY: SITAISAHAU DAR ES SALAAM MTUNZI: MKWELI WA KITAA MHARIRI: - TopicsExpress



          

STORY: SITAISAHAU DAR ES SALAAM MTUNZI: MKWELI WA KITAA MHARIRI: COX DAWA YAO +++ilipoishia+++ Nilipouchunguza ule mfuko niligundua moja kwa moja kuwa ile ilikuwa bastola... #Sasa #endelea ****SEHEMU YA KUMI NA SITA(16)**** .... .,... Kiukweli nilipagawa sana na ukicheki muda huo wale polisi waliamrisha kila mtu alale chini na kila kitu alichokuwa nacho akiweke juu ya meza Niliogopa sana nikajua moja kwa moja wale jamaa ni majambazi kwahyo wameniachia msala mimi hapa Ile Bar haikuwa kubwa sana hvyo wale polisi waliingia mpaka ndani na moja kwa moja wakawakamata wale majamaa wawili ambao mimi nilihisi moja kwa moja ni majambazi, Wale Polisi waliwasachi wale jamaa kisha nikasikia polisi mwingine akisema ""walikuwa watatu na mmoja wao alikuwa na bastola, kwahyo mkuu me nahisi huyo mwenzao bado yupo humu humu"" Niliposikia hvyo niliogopa sana kwani kama wangepekuwa wangenikuta mimi nina bastola msala ungeniangukia mimi, Nilitetemeka sana mpaka meno yakawa yanajigonga gonga Ghafla wale Polisi wakaanza kupekua meza moja mpaka nyingine Hatimae wakafika kwenye meza yangu na kuangalia kwenye ule mfuko Ghafla yule polisi akawaita wenzake waje kwenye ile meza yangu, Nilitetemeka sana hadi nikaishiwa nguvu kabisaa, Kumbuka wakati huo wote mimi nilikuwa nimelala chini kama walivyokuwa wametuamrisha wale polisi muda ule walipoingia Wale polisi wengine walipofika pale walininyua mimi juu na kisha polisi mmoja alinipiga kibao ambacho sitaweza kukisahau maishani mwangu, Kiukweli kwa kile kibao nilichopigwa pombe yote ilikata na nikabaki na mawenge. Walininyanyua juu juu na kwenda kuniweka kwenye kundi la wale jamaa wawili, Ndipo polisi mmoja alipotoa pingu na kutaka kutufunga zile pingu mikononi, Kabla hawajatufunga zile pingu ghafla... Itaendelea Saa tatu(3) usiku Gonga LIKE kama umeipenda KAMA KAWA TUPIA MAONI/USHAURI
Posted on: Tue, 02 Jul 2013 08:07:01 +0000

Trending Topics



">
49-5 star #Reviews. Visceral & Terrifying Crime Mystery. All Bill
With over twenty years of working experience in hospitals and
কাছে নয় ,দূরে নয়
PROMOSI BULAN NOVEMBER Biskita mencari kontraktor untuk

Recently Viewed Topics




© 2015