STORY: SITOISAHAU DAR ES SALAAM MTUNZI: MKWELI WA KITAA MHARIRI - TopicsExpress



          

STORY: SITOISAHAU DAR ES SALAAM MTUNZI: MKWELI WA KITAA MHARIRI COX DAWA YAO #ILIPOISHIA..... Mimi na Rahma tulijitahidi kutafuta vile vikoti lakini tulivikosa kwani vilikuwa vichache ****SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE (28) **** .... ..... Nilikosa cha kufanya kwa muda ule kwani tegemeo langu kubwa lilikuwa ni vile vijaketi na kwa wakati huo mimi na Rahma tulikuwa tumeshavikosa Sikuwa najua kuogelea hata kidogo, wakati huohuo mawimbi makubwa makubwa yakaanza kupiga lile pantoni na mawimbi mengine yakaanza kuingia ndani ya pantoni kwa kasi hali iliyosababisha watu tuanze kukimbizana kupanda upande wa juu wa lile pantoni, Kwa bahati nzuri mimi na Rahma tulibahatika kufika upande wa juu wa pantoni, kumbuka muda huo pantoni lilikuwa tayari limezima na muda huo huo maji yalianza kuingia kwenye lile pantoni kwa kasi hali iliyosababisha pantoni kuanza kuzama Sikuwahi kuona tukio kama lile ila leo ndio lilikuwa linatokea mbele ya macho yangu na mimi mwenyewe nikiwa muhusika, Pantoni lilianza kuzama ilihali mimi na Rahma tukiwa upande wa juu, watu wengi walianza kujitosa baharini huku wengine wakiwa na yale majaketi ila wengi wao walikuwa hawana majaketi, Rahma alinikumbatia na kuanza kusali sala zake za mwisho kwani aliamini kuwa pale ndio ulikuwa wakati wake wa mwisho kuishi duniani, Pantoni ilikuwa inazama kwa spidi na hatimae ikawa zimebakia kama sentimeta thelathini(sm 30) Rahma aliendelea kunikumbatia kwa nguvu na hatimae na sisi tukajirusha kwenye maji, Kile kitendo cha sisi kujirusha kwenye maji ilikuwa kama ndo kuiruhusu ile pantoni izame, Tulizama kwenye maji mimi na Rahma na kwakuwa Rahma alikuwa amenishika nilipata wakati mgumu sana, nilianza kunywa maji ya bahari na wakati huo huo Rahma nae aliniachia na kuanza kujivuta kwa juu, Kitendo hicho kilinifanya na mimi nipate angalau nguvu ya kujivuta juu ya maji, nipotokea juu ya maji watu walikuwa ni wengi sana wanaotapatapa kama mimi, na pia wengi wakuwa hawajui kuogelea kama mimi, Niliendelea kunywa maji ya bahari, Ghafla pembeni yangu nikaona mtoto wa umri kama wa miaka sita anaelea, nikajua moja kwa moja tiari ameshakufa Ila kwa mbele yangu niliona watu wanakuja na mtumbi na kuanza kuokoa watu waliokaribu na ule mtumbwi, Nilijitahidi sana kupiga kelele lakini sauti yangu haikuweza kutoka kwani ilikuwa imekauka, Nilijitahidi kuogelea lakini nilijikuta nipo palepale kwani nilikuwa sijui kuogelea Mara niliona ule mtumbwi uliokuwa unawaokoa watu ukigeuza na kurudi tena kulekule ulikotokea huku ukiwa umejaza watu, Nguvu zilianza kuniishia na sikuwaza kuhusu chochote zaidi ya kuokoa uhai wangu, sikuwaza tena kuhusu Rahma kwani tiari tulikuwa tumeshapotezana kwenye lile varangati, Nguvu ziliniishia kabisa na macho yakaanza kufumba.. Itaendelea kesho Gonga LIKE kama umeipenda MUNIWIE RADHI KWA KUTOWEKA STORI HII JANA.. NAWAPENDA SANA
Posted on: Sat, 13 Jul 2013 16:36:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015