SURA YA KUMI NA MBILI UCHAGUZI KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI NA - TopicsExpress



          

SURA YA KUMI NA MBILI UCHAGUZI KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI NA VYAMA VYA SIASA SEHEMU YA KWANZA UWAKILISHI WA WANANCHI 180.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye umri wa miaka kumi na nane au zaidi mwenye akili timamu ana haki ya kupiga kura na haki ya kuandikishwa kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni. (2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), mamlaka ya uchaguzi itazingatia misingi ifuatayo: (a) wananchi wanatumia haki ya kisiasa kwa mujibu wa Katiba hii; (b) watu wenye ulemavu wanapewa fursa za uwakilishi; (c) haki ya kila mtu kupiga kura moja kufuatana na utashi wa uwakilishi na kura sawa; na (d) uchaguzi ulio huru na ambao - (i) ni wa kura ya siri; (ii) hauna matumizi ya nguvu, vitisho, vishawishi wala rushwa; (iii) haukuwa na matamshi au vitendo vinavyoashiria ukabila, ukanda, udini, dharau na kashfa kwajinsia au unyanyapaa kwa walemavu au makundi madogo katika jamii; (iv) unaendeshwa na kusimamiwa na chombo huru; na (v) unaendeshwa bila upendeleo au kuegemea upande wowote, uliyo makini na inayoonyesha uwajibikaji wa watendaji. Ili kutekeleza masharti ya Ibara ndogo ya (1) na (2), (3) mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha: (a) mamlaka zinazosimamia uchaguzi kutangaza majimbo kwa madhumuni ya uchaguzi wa wabunge; (b) uteuzi wa wagombea; (c) uandikishaji endelevu wa wapiga kura; (d) kuendesha na kusimamia uchaguzi na kura ya maoni; (e) kuweka utaratibu wa kuandikisha raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoishi nje ili kuweza kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni; na (f) utaratibu wa kufanya uchaguzi kuwa mwepesi, wazi na unaozingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum. (4) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (2), kwa lengo la kukuza demokrasia, kulinda Katiba na kuhakikisha panakuwepo uchaguzi huru, kila mpiga kura ana haki ya kufungua shauri Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi isipokuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais,anayoamini yamevunja au kukiuka masharti ya Katiba hii...
Posted on: Fri, 30 Aug 2013 09:43:04 +0000

Trending Topics



v>
A BEAUTIFUL DUA (PRAYER) FOR ALL MARRIED COUPLES..... O Allah,

Recently Viewed Topics




© 2015